Kushika sana dini kunaweza kukupeleka kubaya. Rafiki yangu aliacha kazi ya Ualimu baada ya Mkuu wa Shule kumtaka anyoe ndevu

Dini ya kweli ni ipi na dini ya uongo ni ipi?
sifa za dini ya kweli;
1.Ni lazima ieleze ukweli juu ya maumbile
2,Ni lazima iwe na kanuni na Sheria zinazoendana na maumbile yote
3,Ni lazima itosheleze mahitajio ya mwanadamu ya kimwili na kiroho
4,Ni lazima iwe na mfumo wa maisha uliokamilika
5,iwe ya walimwengu wote na nyakati zote
6,Ni lazima ianishe na kusimamia haki zote za mwanadamu


kinyume chake dini isiyo na sifa hizo maanayake haijitoshelezi na ya uongo
 
Nahisi jamaa alikua tu ameichoka hiyo kazi akapata kisingizio [emoji28][emoji28]
 
1. Ukweli wa maumbile! how?

Ni maumbile yote kwa ujumla kuanzia ulimwengu ulivyo na viumbe or..
 
Safi sana! Kupelekeshwa si jambo jema! Halafu mimi nadhani kuna mambo inabidi tukubali kuwa yamepitwa na wakati.

Kwanza mihutasari inaandaliwa ikiwa na lengo miongoni mwa malengo ni kuthamini utamaduni wa jamii. Haya niambie ni utamaduni gani wa mtanzania ambao ndevu ni marufuku? Au je hakuna utamaduni wa watanzania miongoni mwa jamii ambao ndevu kwao ni jambo muhimu miongoni mwa yenye umuhimu? Majibu utapata kwamba hakuna kuheshimu utamaduni wa watanzania bali kuutweza na kuufutilia mbali!

Pili ndevu ni swala la kimaumbile na imekuwa fasheni kwa watu wengi sasa. Haya na tuambiwe wakina Rick Ross na Roma Mkatoliki ile fasheni yao ya ndevu ina madhara gani kwa jamii. Propaganda ya ugaidi imeharibu kila kitu na bahati mbaya viongozi wetu hawataki kabisa kushtuka na ndiyo maana hata vazi la taifa bado ni kigugumizi hadi leo!

Siyo ndevu tu, mimi sioni mantiki ya kumzuia mtu (mwalimu) kuvaa jinsi, msuli, kanzu, shuka, malapa, kobazi, katambuga, dera, mgolore, tisheti na mavazi mengine eti kwa kigezo cha maadili ya utumishi. Mbona mavazi hayo ndiyo mavazi ya wanajamii wetu tena watu wa heshima tu wanavaa huko kwenye jamii sasa kwanini huku iwe nongwa!?

Wenzenu walizuia zamani kwa sababu zilizoendana na mazingira ya wakati huo nyinyi badala muangalie mazingira ya wakati wetu tulionao, bado mnatumia hukumu ya kale kwa mazingira ya sasa
 
Acha bana.. dini ya ukweli, dini ya uongo... Uthibitisho "Trust me bro"
 
Huyo jamaa alikuwa sahihi , kufuga ndevu kuna tatizo gani.?


MTU mweusi haelewi nini nini !! MTU Kama imani yake inamwambia hivyo kufuga ndevu ni sunah basi muacheni afuge tu.


Mashuleni sahivi kuna masomo ya dini wanakuja mashekh na maustadhati kufundisha na wamefuga ndevu na hatusikii kelele.
 
Bora alipata msaada wakurudi chuo wengine wamepotea kwakweli Mungu atusaidie
 
1. Ukweli wa maumbile! how?

Ni maumbile yote kwa ujumla kuanzia ulimwengu ulivyo na viumbe or..
Ukweli kuhusu maumbile,nn lengo la mwanadamu kuwepo Duniani,lengo,dhima
na maumbile ya vyote vilivyomo mfano mbingu,ardhi,nyota,wanyama,mimea n.k
 
Ukweli mchungu.
Mod hakujua kusoma wala kuandika mpaka anakufa, na wafuasi wake Wana litambua Hilo,
Lakin mod amewatrick Kwa kuwaogopesha Sana watu, it was psychological manipulation
Jahanamu kuchomwa Moto milele, jahna mabikira kama wote + Mito ya pombe
 
Mimi ndo wange niponda mawe😃😆
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…