Kushika sana dini kunaweza kukupeleka kubaya. Rafiki yangu aliacha kazi ya Ualimu baada ya Mkuu wa Shule kumtaka anyoe ndevu

Tatizo watu wanachukuwa utamaduni na kufanya ni dini. Vilemba na ndevu ni utamaduni sio dini. Ni kwamba wenye utamaduni fulani ni wa dini fulani hii inachanganya wanaopenda kuiga
Kuna hii ya siku hizi ya kitu kinaitwa sijui hakika. Wanasomewa watoto na unachinja mbuzi na mifupa inakusanywa na kuzikwa. Huu ni utamaduni wa waarabu lakini watu wameiga. Kuna dada yangu alichinja mbuzi 9 kwa ajili ya watoto wake , akijua eti watakuwa na maadili, loh wote wamekuwa ovyo kabisa .
 
aisee!
sunna zenye faradhi ndio nini asee? hizi dini zina watu wehu
 
Hahah, kazi kweli. Halafu kuna watu huwaambii kitu kuhusu haya mambo. Hao hao wanawachukia hadi ndugu zao eti kisa sio wa dini yao.
Nakumbuka Miaka fulani kwenye miaka ya 2012 na 2013
Nilikuwa Tanga Msikiti mmoja hivi kipindi Naswali na nina miaka miwili Tangu nisilimu..

Nilishangaa Kuna Dhehebu moja wamekaa nje na Fimbo na Mikasi wanasubiri Waislmu watoke nje wawapunguzie kanzu zao na Wakikataa wawatandike Fimbo Siku hiyo sikutoka Msikitini mpaka Jioni 😅😅😅
 
Mtu mweusi hana kimbilio lingine zaidi ya dini. Sasa kwa vile hatuna akili basi ndio tunakua vituko zaidi.
 
Dhehebu gani Hilo🤣🤣🤣
 
Dhehebu gani Hilo🤣🤣🤣
SIku hiyo Nilikuwa nimechelewa nikasema msikiti ni msikiti tu nikaingia Kuswali Msikiti wa Ibadhi..😅😅

Bwana kumbe Answar na Salafi wanawawinda siku nyingi na wanawindana..
Siku hiyo mimi nimejichanganya bhna wamemaliza kuswali kwao wakaja kukaa nje ya msikiti niliokuwa nimeingia kuswali (Ibadhi)..
Wakiwa na Fimbo na mikasi ya kupunguza Suruali na Kanzu..

Sema serikali iliingilia kati siku hizi sisikii Ugomvi sana naona siku hizi wanabishana kwenye majukwaa Tu..

Na juzi kati nilisikia Waliitisha mkutano Madhehebu yote wakawa na mdahalo wa Kielimu..
 
Kuna jamaa aliacha Chuo tukiwa first year baada ya kusema eti Mkopo wa Bodi ya Elimu ya Juu una riba, na Dini yao pia hairuhusu Riba.

Wakati huo Wanafunzi wa Engineering wanapewa Mkopo asilimia 100
Hii kitu nimesikia Sheikh mmoja leo asubuh anasema riba dhambi yake ni kubwa kuliko mtoto kuzini na mzazi wake tena sehem takatifu(alisema kwa jina la dini) mfano baba na bintiye au mama na mtoto wake wa kiume, Asee nilishangaa sana kumbe riba ni big deal.
 
Ni uelewa mbaya wa dini.

Kwani lazima uwe na ndevu nyingi?! Hata ukiacha sehemu kidogo ya ndevu inaswihi. Kwa maana umeacha ndevu na unazo ndevu.
 
Ni uelewa mbaya wa dini.

Kwani lazima uwe na ndevu nyingi?! Hata ukiacha sehemu kidogo ya ndevu inaswihi. Kwa maana umeacha ndevu na unazo ndevu.
kwani uelewa mzuri wa dini unapatikana wapi?
 
Nina rafik yangu alikua mkristo nilimshawishi kipind flan awe muisam akakataaga.. sas alikuja kubadili mwenyewe jamaa amebadilika aisee Ana iman kali sana kias kwamba kuna vitu ving ameviacha mpk amefirisika
 
Kuna vijana wawili waliacha kibaha boys PCB, wakisema hii elimu inaukafiri,

They were more than smart guys, nataman nijue sasa wako wapi
[emoji1787][emoji1787] dah
 
Kuna jamaa aliacha Chuo tukiwa first year baada ya kusema eti Mkopo wa Bodi ya Elimu ya Juu una riba, na Dini yao pia hairuhusu Riba.

Wakati huo Wanafunzi wa Engineering wanapewa Mkopo asilimia 100
Katika Uislam kuna dua ya kuomba kuruzukiwa ufahamu" Ewe Mwenyezi Mungu niruzuku mimi elimu na fahamu yake". Ninachomaanisha ufahamu nao ni riziki.

Unaweza ukawa umesoma lakini ukakosa riziki ya ufahamu. Kama wengine wanavyokosa hii riziki ya maisha ijapokuwa wamesoma. Sasa kwenye dini hawa watu nao wapo.

Ukipima uchumi wa nchi ambao mhusika anaishi unachangiwa na vitu vingi. Unachangiwa na mambo ya halali na mambo yasiyo ya halali. Na uchumi huo huo pengine ndiyo unawezesha Taasisi zako za kidini ziweze kujiendesha.

Kwa mfano kama huyo jamaa mwalimu, yeye ameangalia kwenye ufugaji wa ndevu. Ila amejaribu kutafakari mshahara anaoupokea kutoka serikalini jamhuri inapata namna gani pesa mpaka yeye anapata kwa kupitia mshahara? Serikali inakusanya kodi kwenye maviwanda ya bia huko, kwenye baa n.k

Kwa hiyo mambo mengine ni ufahamu. Uislamu unakutaka uumche Mungu kadri ya uwezo wako ulipoishia. Mambo mengine ndiyo mifumo ilivyo. Bila hiyo mifumo huwezi kuishi. Mwisho wa siku unaweza ukawa gaidi sasa.
 
Kwanza hivi vipaza sauti vilikuwepo enzi za mtume? Kama hapna ni nani ameruhusu matumizi yake maana mnatupgia kelele na serikal imenyamaza tu
 
Kuna vijana wawili waliacha kibaha boys PCB, wakisema hii elimu inaukafiri,

They were more than smart guys, nataman nijue sasa wako wapi
Hao nao wana upungufu wa ufahamu wa kuielewa dini.

Kwa sababu kwenye uislam neno elimu kwenye mafundisho ya dini limewekwa ni open ending. Mtu anasema elimu ina ukafiri ina ukafiri kivipi?

Na ndiyo maana nchi nyengine wanadhibiti masheikh wenye ufahamu kama huu wanawaharibu vijana bure tu!

Ukikutana na masheikh wa namna hiyo sweka peleka ndani.
 
Alikuwa kachoka laki 7, hata mimi ningesepa japo kuwa na ndevu si lazima kwenye dini.
Jamaa atakua aliacha kazi kwasababu zake zingine

Pengine mchizi alikuwa na mishe alizokuwa ana run nje ya taaluma yake ambazo zilikua zinamuingizia kibunda kuliko ualimu.

Hii ya ndevu akili yangu imegoma kabisa kushawishika na sababu hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…