Kushika sana dini kunaweza kukupeleka kubaya. Rafiki yangu aliacha kazi ya Ualimu baada ya Mkuu wa Shule kumtaka anyoe ndevu

kwani uelewa mzuri wa dini unapatikana wapi?
Kwa kuwapata walimu sahihi.

Ninachomaanisha ni hiki: Kwa mafundisho ya dini ya Kiislamu elimu yako inabidi iwe na sanadi( chain ya mapokeo). Ni lazima kuwe na mapokeo mpaka yafiki kwa Mtume. Yaani Sheikh huyu kasoma kwa huyu..huyu kasoma kwa huyu..

Na kwa bahati nzuri kwenye Uislam hiyo sanadi imehifadhiwa. Na ndiyo maana ukikaa na masheikh wakubwa ukiwa unasumbua utaulizwa umesoma kwa nani?

Kwa sababu kwenye Uislam wapo tu ambao walizuka tu unafahamu wao kwenye dini na kuleta tafrani kwenye jamii hizo hizo za kiislam. Lakini hawakuachwa! Wameandikwa kwenye vitabu na wakaelezwa wanafunzi wao wengine wakakimbilia wapi! Au baada ya kifungo walienda miji ipi mbali na hapo alipoondoka.

Sasa hao ukifuatilia mtiririko wao wa elimu ni wa kimagumashi. Na ndiyo miongoni mwao hao wanaleta matatizo ndani ya jamii ya kiislamu na nje ya jamii ya kiislamu.
 
Salafi/Answar sunna wengi wao ni wakurupukaji tu kwenye mambo mengi.
 
Muache atunze chawa sasa
 
Ishasemwa zama hizi kushika dini ni kama kushika kaa la moto, utaonekana umepitwa na wakati, hujielewi, umepotea kumbe ni vice versa. Imradi haombi chumvi kwa mtu dont judge.
 
Narudia tena!
Salaf/Answar sunna wengi wao ni wakurupukaji kwenye mambo mengi. Na wengi wao wana jazba.

Kuna miaka ya nyuma walileta utaratibu wa namna hiyo kwenye msikiti wa Chuo UDSM. Halafu ni wanafunzi. Wafanyakazi wa Chuo ambao ni waislamu wakawanyoosha vizuri tu. Wakawaambia huu msikiti kama umewashinda ondokeni.

Na mtu ambaye kila akija akawa analeta ikhtilafu sanaa badala ya kutoa elimu ni Abou Aymani. Wanafunzi wakisalaf wote wakapigwa marufuku wasimualike Abou Ayman asitoe darasa hata kidogo hapo!
 
Kwani kulima kuna ubaya gani? Na huyo ndugu yake aliyemsomesha ana matatizo ya akili!
 
Kuna vijana wawili waliacha kibaha boys PCB, wakisema hii elimu inaukafiri,

They were more than smart guys, nataman nijue sasa wako wapi
Watakuwa wamesajiliwa na BOKO HARAM
 
Kuna jamaa aliacha Chuo tukiwa first year baada ya kusema eti Mkopo wa Bodi ya Elimu ya Juu una riba, na Dini yao pia hairuhusu Riba.

Wakati huo Wanafunzi wa Engineering wanapewa Mkopo asilimia 100
Sasa kama Allah na Mwamedi hawapendi mikopo tufanyeje?
 
Nina rafik yangu alikua mkristo nilimshawishi kipind flan awe muisam akakataaga.. sas alikuja kubadili mwenyewe jamaa amebadilika aisee Ana iman kali sana kias kwamba kuna vitu ving ameviacha mpk amefirisika
Yaliyomfilisi na majini mkuu. Usicheze na majini
 
Kumbe Bado haya Mambo yanaendelea?
Mi nilidhani yalikemewa yakaachwa..

Kuna Kiongozi wa Kisalafi Abu Fadhil kassim Mafuta huyu jamaa Ndo Kiongozi wao na wanamuamini sana kwa miaka mingi..Mitafaruku Mingi naona kama yye ndo aanzisha..

Ila waislamu wangepunguza Vurugu za wao kwa wao..
 
Sijui ni matope au akili Mimi sijui labda tukamuulize.
Jamaa hayuko tayari kuikosa pepo kisa ualimu
Ndio ujiulize hapo mwenye akili ni yupi hapo, yule anayekubali kuikosa pepo ya milele kwa maisha mafupi ya Dunia au yule anayekubali kuikosa Dunia na mazuri yake kwa pepo ya milele isiyokwisha
 
Sasa kama Allah na Mwamedi hawapendi mikopo tufanyeje?
Sasa Wazazi hawana uwezo wa kukulipia ada ya Chuo Kikuu, fortunately Serikali inakupa Mkopo wa asilimia 100 bado unakataa Kwa kigezo cha riba.

Uzuri zaidi Rais aliyetoa Mkopo huo ni Ustaadhi JK, Rais wa awamu ya 4

Wanasema ukifa na Kiu baharini itakuwa uzembe.

Kalaga baho 😜
 
Sawa lakini Dini yetu hairuhusu Riba,ni Haram na Ukafiri
 
Nina rafik yangu alikua mkristo nilimshawishi kipind flan awe muisam akakataaga.. sas alikuja kubadili mwenyewe jamaa amebadilika aisee Ana iman kali sana kias kwamba kuna vitu ving ameviacha mpk amefirisika
Njia rahisi ya kumtawala binadamu mpatie umasikini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…