Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 6,607
- 14,076
Kwa kuwapata walimu sahihi.kwani uelewa mzuri wa dini unapatikana wapi?
Ninachomaanisha ni hiki: Kwa mafundisho ya dini ya Kiislamu elimu yako inabidi iwe na sanadi( chain ya mapokeo). Ni lazima kuwe na mapokeo mpaka yafiki kwa Mtume. Yaani Sheikh huyu kasoma kwa huyu..huyu kasoma kwa huyu..
Na kwa bahati nzuri kwenye Uislam hiyo sanadi imehifadhiwa. Na ndiyo maana ukikaa na masheikh wakubwa ukiwa unasumbua utaulizwa umesoma kwa nani?
Kwa sababu kwenye Uislam wapo tu ambao walizuka tu unafahamu wao kwenye dini na kuleta tafrani kwenye jamii hizo hizo za kiislam. Lakini hawakuachwa! Wameandikwa kwenye vitabu na wakaelezwa wanafunzi wao wengine wakakimbilia wapi! Au baada ya kifungo walienda miji ipi mbali na hapo alipoondoka.
Sasa hao ukifuatilia mtiririko wao wa elimu ni wa kimagumashi. Na ndiyo miongoni mwao hao wanaleta matatizo ndani ya jamii ya kiislamu na nje ya jamii ya kiislamu.