Kushika sana dini kunaweza kukupeleka kubaya. Rafiki yangu aliacha kazi ya Ualimu baada ya Mkuu wa Shule kumtaka anyoe ndevu

Kushika sana dini kunaweza kukupeleka kubaya. Rafiki yangu aliacha kazi ya Ualimu baada ya Mkuu wa Shule kumtaka anyoe ndevu

Inaongelea dini gani ?

Kwenye Uislamu kama ndevu unazo ni lazima kuzifuga kama huna kabisa, hii Sheria haikuhusu.

Kufuga ndevu ni Sunnah za mitume wote.
Ukitaka kuongelea kitu hakikisha una elimu nacho,si lazima kila sehemu kujitia ujuaji wa kijinga.
Kwanza unajua nn maana ya sunnah?
Maana ya Sunnah ni kitu ambacho ukikifanya unapata thawabu na ukikiacha hupati dhambi.

Yaani ni kitu ambacho ni hiyari ya mtu kukifanya na sio razima.
 
Kwahiyo usecular hautaki ndevu ama? basi watunge sheria tu kuwa kufuga ndevu ni marufuku. Tz.

Mleta mada umeshindwa kumuelewe mwenye matatizo ni nani kwenye hiyo hadithi yako. Jamaa yupo sahihi 100% na hivyo ndivyo wanaume wanavyotakiwa wawe sio kuyumbishwa yumbishwa.
 
kwenye hili mwalimu mkuu ni mkuda. sema mwalimu naye kakurupuka kuacha kazi. hakuna sehemu ktk sheria za utumishi wa kawaida zinakataza ndevu
 
Ukitaka kuongelea kitu hakikisha una elimu nacho,si lazima kila sehemu kujitia ujuaji wa kijinga.
Kwanza unajua nn maana ya sunnah?
Maana ya Sunnah ni kitu ambacho ukikifanya unapata thawabu na ukikiacha hupati dhambi.

Yaani ni kitu ambacho ni hiyari ya mtu kukifanya na sio razima.

Wewe ndio hujaelewa. Tupunguze jazba jamani.
 
Hakuwa na Fedha, na Wazazi wake walikuwa hoehae kama Wazazi wengi wa Watanzania.

Ni mambo ya Imani aliyachukulia serious

Sijui saivi ana hali gani, maana imepita miaka tangu atuache Chuo 🙌
Ukute aliishia kuwa gaidi
 
Kwanza unajua nn maana ya sunnah?
Maana ya Sunnah ni kitu ambacho ukikifanya unapata thawabu na ukikiacha hupati dhambi.

17. Sunnah na maana yake mbalimbali
Utiifu umegawanyika sampuli mbili:
1 – Mambo ya wajibu.
2 – Mambo yaliyopendekezwa.
Neno “Sunnah” linaweza kuwa na maana nyingi:
1 – Yale yaliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika ´Aqiydah na ´ibaadah.
2 – ´Aqiydah. Ndio maana vitabu vya ´Aqiydah vinaitwa “as-Sunnah”, kama mfano wa “as-Sunnah” cha ´Abdullaah bin Imaam Ahmad na “as-Sunnah” cha Ibn Abiy ´Aaswim. Vinaitwa pia vitabu vya “al-Iymaan”, kama mfano wa “al-Iymaan” cha Ibn Mandah.
Kuhusu Sunnah kwa mujibu wa Muhaddithuun ni yale yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika maneno, vitendo, kulipitisha jambo au sifa.
Sunnah kwa maana hii yenye kuenea inatofautiana. Ipo Sunnah ambayo ni ya lazima, ipo Sunnah ambayo imependekezwa. Sunnah iliyopendekezwa iko ambayo imekokotezwa zaidi, Sunnah ambayo haiko hivo. Mfano wa Sunnah hiyo ni kama zile swalah zilizopendekezwa zinazoswaliwa kwa mnasaba wa zile swalah za faradhi (الرواتب), Witr na Dhuhaa. Zipo Sunnah zengine ambazo zimefungamanishwa na nyakati, kama mfano wa Rak´ah mbili wakati wa kuingia msikitini na Dhuhaa. Vilevile zipo Sunnah ambazo hazikufungamanishwa katika nyakati zote mbali na zile nyakati mtu amekatazwa kuswali ndani yake.
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 20-21
Imechapishwa: 07/07/2021
 
Ukute aliishia kuwa gaidi
Hahaha.........unajua baadhi ya wenzetu wako serious sana na mambo ya Imani, bahati mbaya wenzao walio neutral akina JK na akina Makamba walisoma hadi Shule za Kanisa na kufanikiwa hadi kushika madaraka makubwa ya Nchi.

Wangesema washikirie huo mtazamo wa Imani sidhani kama wangefika pale walipo.

Maandiko yanasema "Mshike sana Elimu usimwache aende zake...."
 
Tatizo wanashikilia sana elimu ya dini ambayo ikukaa sana akili zinakuwa kama zimeruka vile.
Hata wakristu walioshika sana dini wanakuwa na mambo ya ajabu ajabu
 
Back
Top Bottom