Kushika sana dini kunaweza kukupeleka kubaya. Rafiki yangu aliacha kazi ya Ualimu baada ya Mkuu wa Shule kumtaka anyoe ndevu

Kushika sana dini kunaweza kukupeleka kubaya. Rafiki yangu aliacha kazi ya Ualimu baada ya Mkuu wa Shule kumtaka anyoe ndevu

17. Sunnah na maana yake mbalimbali
Utiifu umegawanyika sampuli mbili:
1 – Mambo ya wajibu.
2 – Mambo yaliyopendekezwa.
Neno “Sunnah” linaweza kuwa na maana nyingi:
1 – Yale yaliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika ´Aqiydah na ´ibaadah.
2 – ´Aqiydah. Ndio maana vitabu vya ´Aqiydah vinaitwa “as-Sunnah”, kama mfano wa “as-Sunnah” cha ´Abdullaah bin Imaam Ahmad na “as-Sunnah” cha Ibn Abiy ´Aaswim. Vinaitwa pia vitabu vya “al-Iymaan”, kama mfano wa “al-Iymaan” cha Ibn Mandah.
Kuhusu Sunnah kwa mujibu wa Muhaddithuun ni yale yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika maneno, vitendo, kulipitisha jambo au sifa.
Sunnah kwa maana hii yenye kuenea inatofautiana. Ipo Sunnah ambayo ni ya lazima, ipo Sunnah ambayo imependekezwa. Sunnah iliyopendekezwa iko ambayo imekokotezwa zaidi, Sunnah ambayo haiko hivo. Mfano wa Sunnah hiyo ni kama zile swalah zilizopendekezwa zinazoswaliwa kwa mnasaba wa zile swalah za faradhi (الرواتب), Witr na Dhuhaa. Zipo Sunnah zengine ambazo zimefungamanishwa na nyakati, kama mfano wa Rak´ah mbili wakati wa kuingia msikitini na Dhuhaa. Vilevile zipo Sunnah ambazo hazikufungamanishwa katika nyakati zote mbali na zile nyakati mtu amekatazwa kuswali ndani yake.
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 20-21
Imechapishwa: 07/07/2021
Kwa hiyo kufuga ndevu ni Sunnah ya kazima?
 
Tatizo wanashikilia sana elimu ya dini ambayo ikukaa sana akili zinakuwa kama zimeruka vile.
Hata wakristu walioshika sana dini wanakuwa na mambo ya ajabu ajabu
Umesema sahihi Mkuu

Ndiyo maana tumeelekezwa na maandiko "Kila jambo tulifanye Kwa kiasi"
 
Si lazma mkuu kwa maana ni sunna lazima ni swala, funga, zaka n.k
Mkuu inategema na Madhahab Gani?
Niliwahi kuwa Salafiya.na Answar pia..
Usipofuga Ndevu hata swafu ya Mbele ya Swala utaisikia tu utapelekwa safu ya Nyuma..
Na utapigwa Vijembe na kuitwa mwanamke..

Kuna hadithi Nyingi wanazo za kuhalalisha wasemacho kuwa Ni sunna Zenye Faradhi ndani..
Kama hujawahi kuwa hilo dhehabu huwezi kunielewa
 
kwani hakuna shule za waislam huko akaenda kufundisha mpaka awe mkulima?
na ni wapi katika taratibu na kanuni za waalimu(code of conduct) zinakataza kufuga ndevu? mbona tumesomeshwa na kuwaona waalimu wengi tu wa shule za serikali ziwe za msingi hata sekondari ambao wametufundisha/wamefundisha wakiwa na ndevu za kutosha mpaka wamestaafu na hatukusikia wala kuwaona wakitakiwa kuzinyoa?
 
Sio kweli kuwa kushika Sana dini kunaweza kukupeleka kubaya ila kwa dini zile za uongo(ambapo mafikio yake ni jahanam,huko ndiko kubaya kuliko kote)!
kinyume cha kushika Sana dini ya kweli (uislam) ndiko kunakupeleka kuzuri(Jannah)ambapo ndipo mafikio mazuri kabisa ya mwanadamu.
Allah atuongoze katika njia sahihi na tusife ila tumekuwa waislam kamili!
 
Atakuwa anakula ndevu zake sahiv kama chakula.Kuna watu wahovyo sana kutaka kulazimisha mambo yao Kila sehemu Kwa kuhisi ndiyo wenye haki kumbe ujinga TU.
Au kama wale mandina wanaojiita masalia walienda airport bila passport wala nauli et wanataka kwenda kumuona yesu..Mandina wengina juzi hapa Kenya eti wamefunga mwezi mzima bila kula wakabaki mifupa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wenzenu wanataka ilimu akhera sasa nyie mnawalazimisha kwenye ilimu dunia [emoji28][emoji28]
Watu hunishangaza sana, tuna ulimwengu mmoja tu,
Tuna dunia moja tu.

Wanaotaka hiyo ilimu akhera kwanini wasiende kuisoma huko huko?

The same thing (nje ya mada)
Kwa wale wanaofundisha mambo ya ulimwengu wa roho, kama kweli ulimwengu huo upo, kwanini wasiende kukutana kwenye ulimwengu huo wa roho wakafundishana na sio kuuleta kwenye ulimwengu huu?

Hizo ni scams tu,

Habari za roho na akhera ni hadithi za watoto wanaoogopa paka.
 
Sio kweli kuwa kushika Sana dini kunaweza kukupeleka kubaya ila kwa dini zile za uongo(ambapo mafikio yake ni jahanam,huko ndiko kubaya kuliko kote)!
kinyume cha kushika Sana dini ya kweli (uislam) ndiko kunakupeleka kuzuri(Jannah)ambapo ndipo mafikio mazuri kabisa ya mwanadamu.
Allah atuongoze katika njia sahihi na tusife ila tumekuwa waislam kamili!
Kwamba kuna dini ya ukweli na dini za uongo?
 
Back
Top Bottom