Kushika sana dini kunaweza kukupeleka kubaya. Rafiki yangu aliacha kazi ya Ualimu baada ya Mkuu wa Shule kumtaka anyoe ndevu

Kushika sana dini kunaweza kukupeleka kubaya. Rafiki yangu aliacha kazi ya Ualimu baada ya Mkuu wa Shule kumtaka anyoe ndevu

Sasa Wazazi hawana uwezo wa kukulipia ada ya Chuo Kikuu, fortunately Serikali inakupa Mkopo wa asilimia 100 bado unakataa Kwa kigezo cha riba.

Uzuri zaidi Rais aliyetoa Mkopo huo ni Ustaadhi JK, Rais wa awamu ya 4

Wanasema ukifa na Kiu baharini itakuwa uzembe.

Kalaga baho 😜
Doh 😁 sasa baharini mkuu ufanyeje?
 
Duniani kote wanafikiria namna ya kuzipata rasilimal za africa, lakini waafrika wanawaza namna ya kwenda mbinguni, hapo hapo nikaachana na usabato rasmi [emoji23]
kwa hiyo wewe huitaki mbingu? maisha ya duniani ni mafupi sana mkuu, kulinganisha na yale ya milele pamoja na Bwana.


YESU ANAOKOA
 
Sawaa, wanakazaniwa kusoma Madrasa na hapo hapo wanasoma secular, kwani kuna shida!

Mfungo wa Ramadhan ukikaribia au kuanza ndio mada za kukashifu Uislamu zinaanza

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ
109:1 Al-Kafirun (The Disbelievers)
Sema: Enyi makafiri!

لَا أَعْبُدُ مَا تَعْبُدُونَ
Siabudu mnacho kiabudu;
109:2 Al-Kafirun (The Disbelievers

وَلَا أَنْتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ
109:3 Al-Kafirun (The Disbelievers
Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.

وَلَا أَنَا عَابِدٌ مَا عَبَدْتُمْ
109:4 Al-Kafirun (The Disbelievers
Wala sitaabudu mnacho abudu.

وَلَا أَنْتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ
109:5 Al-Kafirun (The Disbelievers
Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.

لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ
109:6 Al-Kafirun (The Disbelievers
Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.
Nani alimuuliza ?
 
Laiti kama mimi ningelikuwa na mamlaka ningelipiga pini kundi la Salafi kama walivyofanya Misri. Misri ukiwa na usalafi kama wa Qassim Mafuta wanakukamata ndani.
Hammaz unamjua Shaykh Muhammad Raslaan (Allah Amhifadhi) wa Misri? Salafiyya hawana shida. Wanawarudisha Waislam katika Dini yao na kulingania Uislam sahihi. Wanawatakia kheri mno ndugu zao. Si watu wa vurugu kama unavyodai. Huko Misri ulikopataja waleta fujo ni "Ikhwanul Muslimeen" ambao hasa ni Masufi. Masalafi katika Da'awah yao sio watu wa kuminyana na watawala, ni watiifu katika yasiyo haramu na hawatoki nje ya twaa ya mtawala na wana subra katika dhulma ya mtawala. Hukuti wakihangaika na siasa.

Kama kuna wanaominywa katika baadhi yao basi ni kwa sababu ya waleta vurugu miongoni mwa Waislam wengine kama "Ikhwanul Muslimeen" ambao huamsha hasira za watawala na hali inakuwa ngumu zaidi. Ila Masalafi hawana vurugu na watawala. Na ni watu wa amani sana.

Sheikh Qassim Mafuta (Allah Amhifadhi) sio mfitinishaji na sio kuwa hana mchango katika Jamii, mchango wake katika kuielimisha jamii ya Waislam ni mkubwa. Sio kuwa kazi yake ni Ruduud tu kama unavyosema. Labda huwa unamsikiliza Ruduud zake tu. Na hata hizo Ruduud, kwa Rahma za Allah, zina maslahi makubwa kwa Waislam. Kuna wengi, kwa fadhila za Allah na Rahma zake, wameachana na misimamo hatari ya kikhawaarij na makundi ya kigaidi na fikra za watu kama Osama Bin Laden, kina Aboud Rogo na kadhaalika kupitia hizo hizo Ruduud. Kwa Rahma za Allah kuna watu wameacha Uzushi katika Dini, wameacha ushirikina, jazba za wanaharakati na kadhalika baada ya kupambanukiwa na hizo Ruduud na Allah akawaongoza katika Haqq. Pia Haqq inabainishwa na watu wanasimamishiwa Hoja. Haqq inatenganishwa na Baatwil.

Na sio kuwa eti kuna Ruduud peke yake na hakuna kengine. Masalafi ni watu wanaoipa umuhimu mkubwa mno Elimu ya Dini na kuihimiza.

Allah Awahifadhi Sheikh Qassim Mafuta na Walinganizi wengine wa Kisalafi.

Sifa zote njema zinamstahiki Allah, Yeye Ndiye Mwenye Kuongoza.
 
Wanaofunga macho na kusali kwa imani kali nawaonea huruma, ila wanaofunga macho kwa unafiki nawapa 5 ya nguvu. Tumia dini kinafiki kwa shughuli zako za maendeleo na si vinginevyo! Angalia wazungu walivyotumia unafiki " walituachia Biblia na kusepa na madini yetu".
 
Ni jirani yetu huko nyumbani kwetu, pia kuna kaurafiki kwa mbali baina yetu. Likizo sometimes tulikuwa tunajisomea pamoja kwakuwa tulikuwa darasa moja.

Jamaa akawa teacher wa Serikali baadaye. Sasa nasikia walimu wana miiko mingi kutokana na mazingira yao ya kazi, sometimes wanakuwa walezi.

Sasa jamaa hakuacha sunnah ya Mtume akafuga ndevu vizuri. Mkuu wa shule akamwambia Mr nyoa hizo ndevu hii shule ni secular, jamaa akakataa.

Alipoona anazidi kuhimizwa kunyoa uchebe na sometimes kutishiwa kufutwa ajira akamwahi boss wake akaandika 24 hrs resignation letter, mkuu wa shule akaipitisha, na Mkurugenzi akamaliza kazi.

Jamaa sasa kwa moyo mweupe analima kijijini. Kaka yake aliyemsomesha wamegombana baada ya jamaa kupiga kalamu chini lakini anasema hawezi kurudi.
Hii story ni ya kweli au ni man made Story??. Kama ni ya Kweli tunaomba Jina la Huyo Mwalimu na Namba yake ya Simu ili apatiwe Ajira Mpya sasaivi popote nchini.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Kuna jamaa aliacha Chuo tukiwa first year baada ya kusema eti Mkopo wa Bodi ya Elimu ya Juu una riba, na Dini yao pia hairuhusu Riba.

Wakati huo Wanafunzi wa Engineering wanapewa Mkopo asilimia 100
Kuna vijana wawili waliacha kibaha boys PCB, wakisema hii elimu inaukafiri,

They were more than smart guys, nataman nijue sasa wako wapi
Hizi dini ni utumwa tosha
 
Back
Top Bottom