Nimekusoma nikajikuta nacheka kama mazuri, kila siku kulia lia kama tuliambiwa CCM ni charity organisation!
Umeniamsha usingizini, kumbe huu wimbo wa CCM wameiba kura unatakiwa kufa automatically, kama CCM kuiba kunawawezesha wao kufikia malengo yao ni wazi wataendelea kuiba no matter what!.
Kama wakiendelea kuiba, nasi tukiendelea kulia wanaiba, kumbe CCM ndio wenye faida kwa sababu wanakuwa tayari wameshayafikia malengo yao, huku sisi wakulia lia ndio tunaendelea kutwanga maji kwenye kinu kila siku!.
Hapa tukubaliane tu ukweli mchungu, kama hatuwezi kuwazuia CCM kutuibia kwa vitendo, na sio kwa kulia lia kama ilivyozoeleka, bora tuwaache waendelee kututawala wapendavyo.