Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 31,559
- 42,179
Kwanza mkuu Oppo ni waanzilishi wa kuweka ram kubwa na storage Kubwa pamoja na viprocessor vidogo.habari zenu wana JF, hivi karibuni nimeshuhudia poromosheni kubwa ya simu za kampuni ya oppo hasa zile za A series , unakuta internal storage 128, RAM 6, Qualcomm and octa core processor , ambapo simu zenye specifications hizo ziliuzwa bei kubwa sana lakini sasa zinauzwa 95,0000 hadi 100,000 je tatizo nini na kuna mapungufu gani katika simu hizo? Kwa wataalamu tujuzeni tuelewe.
Natanguliza shukrani zenu wakuu uzi utembee huu
Mfano wa simu hizo za Bei rahisi ni kama Oppo A83 unakuta storage 128GB lakini processor ni Helio P23 ambayo ni kimeo. Kama wewe ni wale ambao kigezo cha ubora wa simu ni ukubwa wa storage umeenda na maji.
Pili storage zinakuwa sio za kisasa, ukiangalia hio hio Oppo A83 inatumia Emmc storage.
Tatu specs nyengine za kawaida vitu kama Display unakuta ni 720p tu.
Hivyo toka mwanzo hio simu ni lowend iliwekwa tu memory kubwa kudaka watu wasioelewa simu, sasa hivi imekua used ndio maana imeshuka sana thamani.