Ni nzuri kati ya hizo mbili ila still nayo ina processor dhaifu,
Hio tecno ina core 4 za cortex A7 (core za mwaka 2011) ambazo zishapitwa na wakati na zipo slow.
Hio Oppo ina core 8 za cortex A53 ambazo ni za around 2014 hiza zina uafadhali ila still nazo ni dhaifu.
Cortex A7, A53, A55 na A510 hizi ni core ndogo na zimetengenezwa kuchukua eneo dogo na kula umeme mdogo kazi yake ni kuzisaidia core kubwa, kuzitumia zenyewe kifaa kinakua dhaifu.
Core kubwa kama A73, A73, A75, A76, A78, A710, A715, X1, X2 etc hizi ndio zinapiga kazi kwa nguvu.
Kwa simu ya kisasa yenye perfomance nzuri inakua na angalau core 2 kupanda kubwa na core kadhaa hizo ndogo kwa ajili ya kutunza chaji.
Hivyo kama unanunua simu used ama hata mpya vyema hakikisha ina core kubwa, itakusaidia kwenye matumizi ya kila siku.