Hapo unakosea pia Mkuu, wakati wa mwendazake kelele zilipigwa sana kwamba anaingilia mihimili mingine, Mahakama na Bunge, Mama akiingilia ishu ya covid-19 hatokuwa tofauti na mwendazake, ila kwa hili mtamshangilia kwa sababu tu atakuwa amewafurahisha nyinyi. Nafikiri kila muhimili uachwe ufanye shughuli zake bila kuingiliwa. BTW hao CDM wamekosa njia kabisa za kisheria kuwatoa hao Covid-19? Kisingizio chao ni kuwa wamekata rufaa Baraza kuu, kwa nini hilo baraza kuu lisikae na kuwavua moja kwa moja uanachama? Utasema watakimbilia mahakamani, wakienda mahakamani ni vizuri zaidi maana katiba ya CDM inasema mwanachama yeyote akienda mahakamani kukishtaki chama na akishindwa kesi anakuwa kajifukuzisha uanachama.