Kusinzia Kanisani ni Dalili ya Kuingiliwa na Mapepo

Kusinzia Kanisani ni Dalili ya Kuingiliwa na Mapepo

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Kusinzia ni jambo la kawaida kwa mwanadamu aliyechoka. Lakini kusinzia wakati wa ibada, hasa wakati Neno la Mungu linafundishwa, sio jambo la kawaida kiroho. Ni dalili ya mashambulizi ya kipepo, yanayolenga kuzima roho yako usipokee Neno la uzima.

Ukweli huo unathibitiswa na Marko 1:23. Imeandikwa hivi:
“Na mara palikuwapo katika sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapiga kelele.”

Hiyo inaonyesha kuwa mapepo hayana aibu ya kuingia hata ndani ya nyumba ya Mungu. Kwahiyo mtu kama hayuko macho kiroho, anaweza kuvamiwa na mapepo hata akiwa kanisani.

Kusinzia Kanisani ni mapambano ya roho na mwili. Yesu aliwaambia wanafunzi wake:
“Roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.” (Mathayo 26:41)
Wakati mwingine mwili huchoka, lakini mara nyingi, hali hiyo hutumiwa na adui kukukwamisha usisikie sauti ya Mungu. Pepo hutumia udhaifu wa mwili kufanya usinzie na kuziba masikio ya kiroho.

Kwanini pepo wanawafanya watu wasinzie Kanisani? Hiyo ni njama ya shetani. Katika Luka 8:12, Yesu alisema:
“...Ibilisi huja akaliondoa lile neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka.”

Kusinzia wakati wa mahubiri ni njia ya adui ya kuzuia mbegu ya Neno la Mungu kuingia moyoni. Kumbuka, imani huja kwa kusikia Neno la Kristo. Kwahiyo kama mtu anasinzia saa ya Neno ni wazi hawezi kuwa na imani. Na pasipo imani hatuwezi kumpendeza Mungu. Hiyo ndiyo furaha ya shetani na mapepo yake.

Pepo wanaoleta usingizi ni wa hila, sio wa kumfanya mtu apige makelele kama waliopagawa na mapepo ya magonjwa. Pepo anayeleta usingizi huja kwa utulivu. Anakuletea usingizi wa taratibu, unahisi ni usingizi wa kawaida, kumbe ni mtego wa kukufunga rohoni. Huo ni usingizi wa kiroho. Pepo watakuacha uendelee tu kuwa “mtu wa kwenda kanisani” lakini hutakuwa na nguvu wala tunda la Roho.

Mpaka hapo naamini umeona kuwa kusinzia kanisani siyo jambo la kupuuzia. Ni dalili ya mashambulizi ya kiroho, yanayolenga kukunyima nafasi ya kusikia sauti ya Mungu, kukufanya uwe baridi kiroho na hatimaye uanguke. Kwahiyo ukiona dalili za kusinzia, usikubali usingizi ukutawale: Kemea kwa Jina la Yesu. Dalili zikizidi, funga na kuomba kama tunavyoshauriwa katika Mathayo 17:21. "Pepo wa namna hii hawezi kuondolewa ila kwa maombi na kufunga."
 
Mapepo hayapendi pia usikie au usome mada kama hizi. Hivyo ukisikia sauti inakuambia: "Ah usisome hizi mada za walokole. Ruka, bwana, soma tu mada za siasa na michezo," hiyo ni dalili ya wazi umevamiwa na mapepo. Shetani na mapepo yake hawataki umjue Mungu. hawataki uokoke uende mbinguni. Ndio sababu wanakazana kuudanganya ulimwengu na kuzitia giza akili za watu ili wakatae kumwamini Yesu, mwishowe waangamie motoni.

2 Kor 4:4
"...ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu."

Ufu 12:9
"Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye."
 
Hata Mitume wanatuhimiza kuamka usingizini. Paulo aliandika:
“Amka wewe usinziaye, ufufuke katika wafu, Kristo atakuangaza.” (Waefeso 5:14). Hiyo haihusu usingizi wa usiku bali usingizi wa kiroho, unaoanza mara nyingi kwa kupuuzia Neno, kulisikia bila kulielewa, au kulala wakati linapohubiriwa.
 
Katika Matendo 20:9 kuna habari ya mtu mmoja aliyeitwa Eutiko. Huyu alisinzia wakati Paulo anahubiri, kisha akadondoka toka ghorofani.
Matendo 20:9
"Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi wake akaanguka toka ghorofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa.”

Inawezekana alikuwa amechoka kwa sababu Paulo aliendelea sana kuhubiri. Hata hivyo huo ni mfano wa wazi wa hatari ya kusinzia saa ya Neno. Unaweza kudondoka kiroho na kupoteza wokovu wako.
 
Kama umejazwa Roho Mtakatifu, utakuwa na shauku ya Neno na macho yako ya kiroho yatakuwa 'active' saa ya mahubiri au mafundisho ya Neno. Hivyo unapohisi kusinzia ibadani ni dalili kuwa giza linataka kuingia ndani yako, yaani pepo wa usingizi. Mpinge shetani na mapepo yake, kwa Jina la Yesu. "Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia." (Yak 4:7-10)
 
Umasinzia ibadani japo maspeker yote yale mtu anakoroma mpaka anakumbuka uporo wa jana, lakini akiwa nyumbani karedio kadogo kasabusa kakiwaswa usiku hata sauti ya chini utasikia zima mie nashindwa kupata usingizi😃😃
 
Wakati mwingine sio hata mapepo watu wana Stress ivo wana haki ya kupata utulivu wawapo nyumbani mwa baba yao(kanisani)

Ni haki mtu kulala katika nyumba ya Baba yake maana ni mahali pa amani
SI Kasema mwenyewe Njoo wote na wenye kulemewa na mizigo,nami nitawapumzisha, Sasa Mimi nimetua mzigo kwa Bwana,Sasa Mimi ni Nani nisisinzie kwa Baba, Baada ya kuutua mzigo! Setfree hebu Angalia mwenyewe!
 
Kuna watu wanakunywa breakfast heavy sana, ukifika church ni kuroma tu. Mihogo, uji, ubwabwa plus maharage duu.
Hiyo inaweza kuwa sababu ya kusinzia. Lakini hebu tujiulize: mtu amelala masaa manane au tisa usiku wa kuamkia siku ya ibada Kanisani. Kwanini asinzie tena asubuhi? Tena saa ya mahubiri tu? Mahubiri yakiisha na usingizi umeisha. Kwanini? Tushtuke. Shetani ana njia nyingi za kupata mawindo!
1 Pet 5:8
Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.
 
Mapepo hayapendi pia usikie au usome mada kama hizi. Hivyo ukisikia sauti inakuambia: "Ah usisome hizi mada za walokole. Ruka, bwana, soma tu mada za siasa na michezo," hiyo ni dalili ya wazi umevamiwa na mapepo. Shetani na mapepo yake hawataki umjue Mungu. hawataki uokoke uende mbinguni. Ndio sababu wanakazana kuudanganya ulimwengu na kuzitia giza akili za watu ili wakatae kumwamini Yesu, mwishowe waangamie motoni.

2 Kor 4:4
"...ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu."

Ufu 12:9
"Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye."
Hivi kuna tofauti ya mapepo na majini!??
 
Back
Top Bottom