Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
- Thread starter
- #21
Ukizingatia mitazamo ya Kikristo na Kiislamu, ipo tofauti kubwa kati ya mapepo na majini, Ingawa baadhi ya watu wanaona kama mapepo na majini ni sawa. Hebu tuangalie kwa ufupi tofauti iliyopo:Hivi kuna tofauti ya mapepo na majini!??
Kulingana na Biblia mapepo ni viumbe wa kiroho, waovu, waliopotoka, waliomuasi Mungu. Ni malaika waliomwasi Mungu (Mathayo 25:41, Ufunuo 12:7–9). Wanaitwa pia roho wachafu (Marko 1:23; Luka 8:2).
Kazi yao ni kuwaingilia watu na kuharibu maisha ya watu kwa magonjwa, udhaifu, kuwatia watu hofu, na kuwazuia watu kumfuata Kristo, au kama tulivyoona katika mada hii, wanaweza hata kumletea mtu usingizi asisikie Neno.
Ndio sababu Yesu aliyafukuza mapepo mara nyingi (Mathayo 8:28–32; Luka 4:33–36). Mapepo yanamjua Yesu ni nani na yanatetemeka mbele Yake (Yakobo 2:19).
Kulingana na Uislamu, Majini ni viumbe walioumbwa kwa moto bila moshi. Wametajwa katika Qur’an kama viumbe wanaoishi pamoja na wanadamu. Wanakula, wanaoa, na wanaishi miongoni mwa wanadamu lakini kwa namna ya kiroho. Wenyewe wanasema kwamba kuna majini waovu na wema. Mimi sina imani hiyo. Naamini tu yaliyoandikwa katika Biblia. Na nimethibitisha wazi mapepo yapo, maana kwa Jina la Yesu nimeyakemea yatoke ndani ya watu waliokuwa wanasumbuliwa na mapepo, yakatoka na kuwaacha huru.