Kusinzia Kanisani ni Dalili ya Kuingiliwa na Mapepo

Kusinzia Kanisani ni Dalili ya Kuingiliwa na Mapepo

Kwa kweli siamaini kwa unayo yasema maana siamini kama kweli imani ya mtu inakontroliwa na kitabu tena kilichotungwa na binadamu wenzetu ili kutawala wenzao. Mara nyingi ninapopatwa na hali kama hii hasa pale mwanzoni nilipoanza kuwa na hii hali, nilikuwa narudi nyumbani na kumuomba Mwenyewezi Mungu nikiwa peke yangu na napata ahueni. Sijuwi kama utanielewa kwa huu ushuhuda ufuatao; ni hivi, siku za nyuma nilikuwa napatwa na changamoto sana kimaisha, hasa uchumi. Nilikuwa namuhusisha sana mchungaji wangu (huyu ana kipaji cha kusaidia watu kupitia maombi) na hata kwenye jumuiya nilishirikisha wenzangu kuniombea, lakini wapi. Baadaye nikajiona kuwa nina ji-overexpose matatizo yangu kwa watu wasionihusu bila sababu au imani isiyo yangu (Ukristu na Uislam, tumeletewa). Nikashikwa na hasira na kuanza kumuomba na kumlalamikia Mungu wangu moja kwa moja na nikawa nafanikiwa kutatua changamoto zangu. Kuanzia hapa nikaachana kabisa na mambo ya kwenda kanisani na jumuiya kuswali kwani nina amini Mungu anaongea nami muda wowote na sihitaji kwenda kujumuika na watu ili anisikie.
Sijakuelewa mbongo_halisi
Unasema Biblia ni kitabu kilichotungwa na binadamu wenzetu, halafu wakati huohuo unasema unaamini Mungu anaongea nawe wakati wote. Sasa umemjuaje huyo Mungu kama sio kupitia Biblia unayoikataa?
Waebrania 10:25
wala tusiache kukusanyika pamoja[kanisani], kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri muonavyo siku ile kuwa inakaribia.
 
Ukiwa na njaa au madeni lazima usinzie wala siyo mapepo, za kuambiwa changanya na za kwako...

Cc: Mahondaw
 
Ukiwa na njaa au madeni lazima usinzie wala siyo mapepo, za kuambiwa changanya na za kwako...

Cc: Mahondaw
Kanisani saa ya mahubiri ni saa ya kupata chakula cha kiroho na kushibishwa. Mtu anayesinzia wakati huo, kama hana mapepo basi ni dalili kuwa hana njaa ya kiroho.
Mt 5:6-10
Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.

Maneno ya Mungu usiyachanganye na akili zako Smart911
 
Kanisani saa ya mahubiri ni saa ya kupata chakula cha kiroho na kushibishwa. Mtu anayesinzia wakati huo, kama hana mapepo basi ni dalili kuwa hana njaa ya kiroho
Mt 5:6-10
Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.

Maneno ya Mungu usiyachanganye na akili zako Smart911
Njaa mbaya na wala siyo mapepo...
 
Ukiwa na njaa au madeni lazima usinzie wala siyo mapepo, za kuambiwa changanya na za kwako...

Cc: Mahondaw
Saa ya mahubiri inawezekana Mungu anataka kukuambia njia za kupata pesa au kulipa madeni. Ukisinzia utazisikiaje njia hizo?
 
Uzuri wa Biblia ni kwamba kila mja anatoka na mistari yake anayoitaka na kujaza tafsiri zake zilizomkaa kichwani na zinaenda mjini...
 
Kwanini unakataa uwepo wa mapepo kanisani? Hujahudhuria ibada za makanisa ambayo pepo wanakemewa na kuwatoka wengi?
Za kuambiwa changanya na za kwako, ukishiba vizuri hakunaga kitu kama mapepo...
 
Saa ya mahubiri inawezekana Mungu anataka kukuambia njia za kupata pesa au kulipa madeni. Ukisinzia utazisikiaje njia hizo?
Ni mpaka uwe umeshiba, an empty stomach siyo kabisa...
 
Mchungaji anawadanganya hivyo ili msilale wakati anaomba sadaka
 
Uzuri wa Biblia ni kwamba kila mja anatoka na mistari yake anayoitaka na kujaza tafsiri zake zilizomkaa kichwani na zinaenda mjini...
Sio kweli, SankaraBoukaka. Kama unafikiri ni kujiwekea tu mistari unayotaka, weka hapa mistari yako kuhusu mada hii, uone ntakavyoizuia isiende mjini 😎
 
Tembea mtaani ndugu, uone kama 'Ombaomba' wanalala. Kila saa utaona wanatikisa kibakuli
Hawapo kwenye nyumba za ibada, hawamsikilizi mtu aliyeshiba tayari, wapo wakitafutia matumbo yao...
 
Hawapo kwenye nyumba za ibada, hawamsikilizi mtu aliyeshiba tayari, wapo wakitafutia matumbo yao...
Sasa ukienda kanisani si unaenda kutafuta chakula cha kiroho, kwanini usinzie saa ya kuingiza kitu rohoni?
 
Sasa ukienda kanisani si unaenda kutafuta chakula cha kiroho, kwanini usinzie saa ya kuingiza kitu rohoni?
Hao viongozi wanaokupa vyakula vya roho wanategemea wakukamue kwa sadaka baada ya hapo wanenda kula biriani na juice ya baridi...
Wewe unasinzia na njaa zako unasingizia mapepo...
 
Hao viongozi wanaokupa vyakula vya roho wanategemea wakukamue kwa sadaka baada ya hapo wanenda kula biriani na juice ya baridi...
Wewe unasinzia na njaa zako unasingizia mapepo...
Kutoa sadaka ni hiari. Mtu hatakiwi kulazimishwa. Tena ni heri kutoa kuliko kupokea(Mdo 20:35).
2 Wakorintho 9:7
"Kila mmoja na atoe kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu."

Kama hapo unaposali, unalazimishwa kutoa sadaka, basi hapo nakuruhusu uchanganye na za kwako. Kimbiaaa
 
Back
Top Bottom