Kusinzia Kanisani ni Dalili ya Kuingiliwa na Mapepo

Inategemea ni Kanisa gani:
Kwa Katoliki kuna kusimama, kupiga magoti, kuimba, kupeana amani, kula mkate, kutoa sadaka, nk: Saa ngapi unasinzia?
 
Usitoe hukumu ya jumla,
Kuna mtu anaingia kazini night shift, asubuhi anaenda kanisani akiwa hajapata muda wa kupumzika,
Wengine chai yao wakila ubwambwa, maharangwe ya kiporo na chai halafu uende kanisani huyu naye atapitia changamoto ya usingizi.
Unadhani akikutana na mtu aliyesimama Madhabahu kufundishia neno amepoa lazima atasinzia lakini akutane na akina Mch Eliona Kimaro, Mwl Mwakasenge, hawezi kupitiwa na usingizi wa machovu.
 
sio kweli ,ila hizo ni fikira za watu wanaofikiria mambo kwa upeo wa chini sana,kuna watu wanasikiliza mahuburi kwa umakini sana lakini ni wakaidi kwenye hilo neno la Mungu kwa maana ni wazizi wazumaji ,na ngiriba ngiriba nyingi za uchafu mwingi . Na kuna wengine mnaweza kuwahukumu kwa kutumia vigezo hivi vya upeo wa chini lakini ni watiifu kwa neno la Mungu. Jambo ambalo ni la msingi kutokulala usingizi ni kuishi kama neno na Mungu na sio hizi porojo za kusema kulala katika kusanyiko la watu walio katika utulivu ni kwamba mtu yupo possessed. Kuna watu ambao kama kazi zake ni
 
Kusinzia ni jambo la kawaida kwa mwanadamu aliyechoka. Lakini kusinzia wakati wa ibada, hasa wakati Neno la Mungu linafundishwa, sio jambo la kawaida kiroho. Ni dalili ya mashambulizi ya kipepo, yanayolenga kuzima roho yako usipokee Neno la uzima.

Ukweli huo unathibitiswa na Marko 1:23. Imeandikwa hivi:
“Na mara palikuwapo katika sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapiga kelele.”

Hiyo inaonyesha kuwa mapepo hayana aibu ya kuingia hata ndani ya nyumba ya Mungu. Kwahiyo mtu kama hayuko macho kiroho, anaweza kuvamiwa na mapepo hata akiwa kanisani.

Kusinzia Kanisani ni mapambano ya roho na mwili. Yesu aliwaambia wanafunzi wake:
“Roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.” (Mathayo 26:41)
Wakati mwingine mwili huchoka, lakini mara nyingi, hali hiyo hutumiwa na adui kukukwamisha usisikie sauti ya Mungu. Pepo hutumia udhaifu wa mwili kufanya usinzie na kuziba masikio ya kiroho.

Kwanini pepo wanawafanya watu wasinzie Kanisani? Hiyo ni njama ya shetani. Katika Luka 8:12, Yesu alisema:
“...Ibilisi huja akaliondoa lile neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka.”

Kusinzia wakati wa mahubiri ni njia ya adui ya kuzuia mbegu ya Neno la Mungu kuingia moyoni. Kumbuka, imani huja kwa kusikia Neno la Kristo. Kwahiyo kama mtu anasinzia saa ya Neno ni wazi hawezi kuwa na imani. Na pasipo imani hatuwezi kumpendeza Mungu. Hiyo ndiyo furaha ya shetani na mapepo yake.

Pepo wanaoleta usingizi ni wa hila, sio wa kumfanya mtu apige makelele kama waliopagawa na mapepo ya magonjwa. Pepo anayeleta usingizi huja kwa utulivu. Anakuletea usingizi wa taratibu, unahisi ni usingizi wa kawaida, kumbe ni mtego wa kukufunga rohoni. Huo ni usingizi wa kiroho. Pepo watakuacha uendelee tu kuwa “mtu wa kwenda kanisani” lakini hutakuwa na nguvu wala tunda la Roho.

Mpaka hapo naamini umeona kuwa kusinzia kanisani siyo jambo la kupuuzia. Ni dalili ya mashambulizi ya kiroho, yanayolenga kukunyima nafasi ya kusikia sauti ya Mungu, kukufanya uwe baridi kiroho na hatimaye uanguke. Kwahiyo ukiona dalili za kusinzia, usikubali usingizi ukutawale: Kemea kwa Jina la Yesu. Dalili zikizidi, funga na kuomba kama tunavyoshauriwa katika Mathayo 17:21. "Pepo wa namna hii hawezi kuondolewa ila kwa maombi na kufunga."
Maisha yetu haya japo twaishi mwilini, kila siku tuna vita inayoendelea katika ulimwengu wa roho.
Katika Efeso6:12-13 twasoma;
[Efe6:12]Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
[Efe6:13]Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
 
Amen
 
Mafundisho ni boring.

Utaona katika Kanisa mara nyingi anakuwepo mtu maalum kuwathibiti watoto wasifanye fujo.

Inaonyesha tu Dini imefikia ukingoni na kwamba labda kweli ni lazima Kristu arudi tena kama ilivuoahidiwa katika Biblia.

Haya Bungeni Wabunge wanasinzia.
Halihusiani na mapepo.

Ingawa psychiatrists have interesting things to say when they discuss about schizophrenia.

Wanasema kwamba sometimes schizophrenic anasinzia.

Halafu, please note,there are different styles of preaching. Mahubiri siyo sawa katika madhehebu yote.

Catholic priest anaamini kwamba when you are preaching,it is imperative you be calm. Kwa hiyo utaona kwamba katika Kanisa Katoliki wao wana utulivu.

Lakini katika makanisa mengine ,Kanisa la Gwajima kwa mfano, wanaamini kwamba when someone is preaching,it is imperative that he should be hyperexcited.

Sasa,it follows that watu watasinzia katika makanisa mengine.
 
Kusinzia ni jambo la kawaida kwa mwanadamu aliyechoka. Lakini kusinzia wakati wa ibada, hasa wakati Neno la Mungu linafundishwa, sio jambo la kawaida kiroho. Ni dalili ya mashambulizi ya kipepo, yanayolenga kuzima roho yako usipokee Neno la uzima.

Ukweli huo unathibitiswa na Marko 1:23. Imeandikwa hivi:
“Na mara palikuwapo katika sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapiga kelele.”

Hiyo inaonyesha kuwa mapepo hayana aibu ya kuingia hata ndani ya nyumba ya Mungu. Kwahiyo mtu kama hayuko macho kiroho, anaweza kuvamiwa na mapepo hata akiwa kanisani.

Kusinzia Kanisani ni mapambano ya roho na mwili. Yesu aliwaambia wanafunzi wake:
“Roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.” (Mathayo 26:41)
Wakati mwingine mwili huchoka, lakini mara nyingi, hali hiyo hutumiwa na adui kukukwamisha usisikie sauti ya Mungu. Pepo hutumia udhaifu wa mwili kufanya usinzie na kuziba masikio ya kiroho.

Kwanini pepo wanawafanya watu wasinzie Kanisani? Hiyo ni njama ya shetani. Katika Luka 8:12, Yesu alisema:
“...Ibilisi huja akaliondoa lile neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka.”

Kusinzia wakati wa mahubiri ni njia ya adui ya kuzuia mbegu ya Neno la Mungu kuingia moyoni. Kumbuka, imani huja kwa kusikia Neno la Kristo. Kwahiyo kama mtu anasinzia saa ya Neno ni wazi hawezi kuwa na imani. Na pasipo imani hatuwezi kumpendeza Mungu. Hiyo ndiyo furaha ya shetani na mapepo yake.

Pepo wanaoleta usingizi ni wa hila, sio wa kumfanya mtu apige makelele kama waliopagawa na mapepo ya magonjwa. Pepo anayeleta usingizi huja kwa utulivu. Anakuletea usingizi wa taratibu, unahisi ni usingizi wa kawaida, kumbe ni mtego wa kukufunga rohoni. Huo ni usingizi wa kiroho. Pepo watakuacha uendelee tu kuwa “mtu wa kwenda kanisani” lakini hutakuwa na nguvu wala tunda la Roho.

Mpaka hapo naamini umeona kuwa kusinzia kanisani siyo jambo la kupuuzia. Ni dalili ya mashambulizi ya kiroho, yanayolenga kukunyima nafasi ya kusikia sauti ya Mungu, kukufanya uwe baridi kiroho na hatimaye uanguke. Kwahiyo ukiona dalili za kusinzia, usikubali usingizi ukutawale: Kemea kwa Jina la Yesu. Dalili zikizidi, funga na kuomba kama tunavyoshauriwa katika Mathayo 17:21. "Pepo wa namna hii hawezi kuondolewa ila kwa maombi na kufunga."
Inawezekana kwani hata mimi mara nyingi nikifikiria kwenda kanisani nashikwa na hasira na usingizi mzito, sielewi kwanini yaani.
 
20250702_161728.png
 
Inawezekana kwani hata mimi mara nyingi nikifikiria kwenda kanisani nashikwa na hasira na usingizi mzito, sielewi kwanini yaani.
Asante mbongo_halisi kwa kuwa mkweli. Sio wengi wenye ujasiri wa kukiri hali hiyo hadharani. Hilo lenyewe ni hatua ya kwanza ya ushindi wako!

Hali ya kushikwa na hasira na usingizi mzito saa ya kwenda ibadani, siyo ya kawaida. Ni ishara ya vita vya kiroho. Adui (shetani) hataki uende kanisani kwa sababu anajua kuna kitu cha kipekee Mungu amekuandalia kule: huenda ni uponyaji, huenda ni ujumbe wa kukutoa kifungoni, au ni majibu ya maombi yako.

Hiyo hali unayopitia ni kama kamba ya kipepo inayokufunga na kukuzuia usiende kwenye nuru. Kumbuka, Yesu alishalipa gharama ya ushindi wako. Ukisimama kwa maombi, ukiikataa hiyo hali kwa imani, utaona mabadiliko.

Ukisikia hali hiyo tamka maneno kama haya kwa imani:

“Kwa Jina la Yesu, nakataa usingizi wa kiroho, nakataa roho ya hasira. Shetani huwezi kunizuia kwenda Kanisani. Lazima niende nyumbani mwa Baba Mungu, katika Jina la Yesu. Amen.”

Halafu chukua hatua: nenda kanisani hata kama mwili haujisikii kwenda.

Kumbuka tena: hasira na usingizi havitoki kwako; ni mashambulizi ya adui. Lakini sasa kwakuwa umeujua ukweli; ukweli huu ukuweke huru katika Jina la Yesu, amen(Yohana 8:32).
 
Muda mwingine ni uchovu tu, mtu hujalala vizuri ukifika kanisani unauchapa alafu useme ni pepo hell no!
 
Uzi mzima umejaza post zako si tutachangia wapi
Duh, Sisyphus
Umeambiwa na nani uzi umejaa? We sema tu hujapata hoja ya kuchangia. Anyway nashukuru kwamba umesoma uzi huu. Mungu akusaidie kuyapinga mapepo yakitaka kukuletea uzingizi Kanisani
 
Hiyo inaweza kuwa sababu ya kusinzia. Lakini hebu tujiulize: mtu amelala masaa manane au tisa usiku wa kuamkia siku ya ibada Kanisani. Kwanini asinzie tena asubuhi? Tena saa ya mahubiri tu? Mahubiri yakiisha na usingizi umeisha. Kwanini? Tushtuke. Shetani ana njia nyingi za kupata mawindo!
1 Pet 5:8
Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.
Ebu Niambie Ushauri Wako kwangu, Mimi nilitoka Daresallam na Basi la Usiku kwenda Moshi Rombo, Nimefika Rombo Asubuhi na Asubuhi hiyo hiyo sijabadili nguo Wala kuoga nikaenda Misa ya Kwanza Asubuhi/ nipo kanisani nikawa nafuatilia Misa vizuri tu, Lakini Wakati Mwingine Usingizi Unataka kunipitia/ Je hayo nayo Mapepo au Uchovu?
 
Inatakiwa wawepo wahudumu wa kuwapiga watu makofi wanaposinzia
 
Ebu Niambie Ushauri Wako kwangu, Mimi nikitoka Daresallam na Basi la Usiku kwenda Moshi Rombo, Nimefika Rombo Asubuhi na Asubuhi hiyo hiyo sijabadili nguo Wala kuoga nikaenda Misa ya Kwanza Asubuhi/ nipo kanisani nikawa nafuatilia Misa vizuri tu, Lakini Wakati Mwingine Usingizi Unataka kunipitia/ Je hayo nayo Mapepo au Uchovu?
Kama una uchovu kwa nini uende ibadani
 
Ebu Niambie Ushauri Wako kwangu, Mimi nilitoka Daresallam na Basi la Usiku kwenda Moshi Rombo, Nimefika Rombo Asubuhi na Asubuhi hiyo hiyo sijabadili nguo Wala kuoga nikaenda Misa ya Kwanza Asubuhi/ nipo kanisani nikawa nafuatilia Misa vizuri tu, Lakini Wakati Mwingine Usingizi Unataka kunipitia/ Je hayo nayo Mapepo au Uchovu?
Inaweza kuwa uchovu. Lakini umesema ulitoka na basi la usiku, ukafika asubuhi. It means ulilala kwenye gari usiku huo. Sasa kwanini ulale tena kwenye misa? Ingekuwa asubuhi hiyo umealikwa kula kiti moto naamini usingesinzia 🙂
 
Asante mbongo_halisi kwa kuwa mkweli. Sio wengi wenye ujasiri wa kukiri hali hiyo hadharani. Hilo lenyewe ni hatua ya kwanza ya ushindi wako!

Hali ya kushikwa na hasira na usingizi mzito saa ya kwenda ibadani, siyo ya kawaida. Ni ishara ya vita vya kiroho. Adui (shetani) hataki uende kanisani kwa sababu anajua kuna kitu cha kipekee Mungu amekuandalia kule: huenda ni uponyaji, huenda ni ujumbe wa kukutoa kifungoni, au ni majibu ya maombi yako.

Hiyo hali unayopitia ni kama kamba ya kipepo inayokufunga na kukuzuia usiende kwenye nuru. Kumbuka, Yesu alishalipa gharama ya ushindi wako. Ukisimama kwa maombi, ukiikataa hiyo hali kwa imani, utaona mabadiliko.

Ukisikia hali hiyo tamka maneno kama haya kwa imani:

“Kwa Jina la Yesu, nakataa usingizi wa kiroho, nakataa roho ya hasira. Shetani huwezi kunizuia kwenda Kanisani. Lazima niende nyumbani mwa Baba Mungu, katika Jina la Yesu. Amen.”

Halafu chukua hatua: nenda kanisani hata kama mwili haujisikii kwenda.

Kumbuka tena: hasira na usingizi havitoki kwako; ni mashambulizi ya adui. Lakini sasa kwakuwa umeujua ukweli; ukweli huu ukuweke huru katika Jina la Yesu, amen(Yohana 8:32).
Kwa kweli siamaini kwa unayo yasema maana siamini kama kweli imani ya mtu inakontroliwa na kitabu tena kilichotungwa na binadamu wenzetu ili kutawala wenzao. Mara nyingi ninapopatwa na hali kama hii hasa pale mwanzoni nilipoanza kuwa na hii hali, nilikuwa narudi nyumbani na kumuomba Mwenyewezi Mungu nikiwa peke yangu na napata ahueni. Sijuwi kama utanielewa kwa huu ushuhuda ufuatao; ni hivi, siku za nyuma nilikuwa napatwa na changamoto sana kimaisha, hasa uchumi. Nilikuwa namuhusisha sana mchungaji wangu (huyu ana kipaji cha kusaidia watu kupitia maombi) na hata kwenye jumuiya nilishirikisha wenzangu kuniombea, lakini wapi. Baadaye nikajiona kuwa nina ji-overexpose matatizo yangu kwa watu wasionihusu bila sababu au imani isiyo yangu (Ukristu na Uislam, tumeletewa). Nikashikwa na hasira na kuanza kumuomba na kumlalamikia Mungu wangu moja kwa moja na nikawa nafanikiwa kutatua changamoto zangu. Kuanzia hapa nikaachana kabisa na mambo ya kwenda kanisani na jumuiya kuswali kwani nina amini Mungu anaongea nami muda wowote na sihitaji kwenda kujumuika na watu ili anisikie.
 
Back
Top Bottom