SI Kasema mwenyewe Njoo wote na wenye kulemewa na mizigo,nami nitawapumzisha, Sasa Mimi nimetua mzigo kwa Bwana,Sasa Mimi ni Nani nisisinzie kwa Baba, Baada ya kuutua mzigo! Setfree hebu Angalia mwenyewe!Wakati mwingine sio hata mapepo watu wana Stress ivo wana haki ya kupata utulivu wawapo nyumbani mwa baba yao(kanisani)
Ni haki mtu kulala katika nyumba ya Baba yake maana ni mahali pa amani
Lazima usinzie, mbali na kuchoma,anayehubiria ndio mwenye nguvu hakuna kujadili!Dah imajini pepo linapata uwezo wa kuingia kanisani?😂😂 Hizi imani nyingine bwanaa
wengine ni uchovu tuu ama shibe
Hiyo inaweza kuwa sababu ya kusinzia. Lakini hebu tujiulize: mtu amelala masaa manane au tisa usiku wa kuamkia siku ya ibada Kanisani. Kwanini asinzie tena asubuhi? Tena saa ya mahubiri tu? Mahubiri yakiisha na usingizi umeisha. Kwanini? Tushtuke. Shetani ana njia nyingi za kupata mawindo!Kuna watu wanakunywa breakfast heavy sana, ukifika church ni kuroma tu. Mihogo, uji, ubwabwa plus maharage duu.
Hivi kuna tofauti ya mapepo na majini!??Mapepo hayapendi pia usikie au usome mada kama hizi. Hivyo ukisikia sauti inakuambia: "Ah usisome hizi mada za walokole. Ruka, bwana, soma tu mada za siasa na michezo," hiyo ni dalili ya wazi umevamiwa na mapepo. Shetani na mapepo yake hawataki umjue Mungu. hawataki uokoke uende mbinguni. Ndio sababu wanakazana kuudanganya ulimwengu na kuzitia giza akili za watu ili wakatae kumwamini Yesu, mwishowe waangamie motoni.
2 Kor 4:4
"...ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu."
Ufu 12:9
"Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye."
EutikoTikiko au Eutiko? Hao ni watu wawili tofauti