Kusinzia Kanisani ni Dalili ya Kuingiliwa na Mapepo

Hivi kuna tofauti ya mapepo na majini!??
Ukizingatia mitazamo ya Kikristo na Kiislamu, ipo tofauti kubwa kati ya mapepo na majini, Ingawa baadhi ya watu wanaona kama mapepo na majini ni sawa. Hebu tuangalie kwa ufupi tofauti iliyopo:

Kulingana na Biblia mapepo ni viumbe wa kiroho, waovu, waliopotoka, waliomuasi Mungu. Ni malaika waliomwasi Mungu (Mathayo 25:41, Ufunuo 12:7–9). Wanaitwa pia roho wachafu (Marko 1:23; Luka 8:2).

Kazi yao ni kuwaingilia watu na kuharibu maisha ya watu kwa magonjwa, udhaifu, kuwatia watu hofu, na kuwazuia watu kumfuata Kristo, au kama tulivyoona katika mada hii, wanaweza hata kumletea mtu usingizi asisikie Neno.

Ndio sababu Yesu aliyafukuza mapepo mara nyingi (Mathayo 8:28–32; Luka 4:33–36). Mapepo yanamjua Yesu ni nani na yanatetemeka mbele Yake (Yakobo 2:19).

Kulingana na Uislamu, Majini ni viumbe walioumbwa kwa moto bila moshi. Wametajwa katika Qur’an kama viumbe wanaoishi pamoja na wanadamu. Wanakula, wanaoa, na wanaishi miongoni mwa wanadamu lakini kwa namna ya kiroho. Wenyewe wanasema kwamba kuna majini waovu na wema. Mimi sina imani hiyo. Naamini tu yaliyoandikwa katika Biblia. Na nimethibitisha wazi mapepo yapo, maana kwa Jina la Yesu nimeyakemea yatoke ndani ya watu waliokuwa wanasumbuliwa na mapepo, yakatoka na kuwaacha huru.
 
Mimi hulala pale tunapoitwa kutoa sadaka ya pili ile ya mwisho wa ibada.
 
OK. Inawezekana alikuwa amechoka kwa sababu Paulo alifululiza sana kuhubiri. Hata hivyo huo ni mfano wa wazi wa hatari ya kusinzia saa ya Neno. Mtu anaweza kudondoka kiroho na kupoteza wokovu. At least Eutiko anaweza kujitetea kwamba alikuwa amechoka. Lakini mtu aliyelala masaa 8-9 usiku wa kuamkia ibada halafu anasinzia ibada ya asubuhi? Tena wakati mahubiri yanapoanza tu. Uchovu gani huo?
 
SI Kasema mwenyewe Njoo wote na wenye kulemewa na mizigo,nami nitawapumzisha, Sasa Mimi nimetua mzigo kwa Bwana,Sasa Mimi ni Nani nisisinzie kwa Baba, Baada ya kuutua mzigo! Setfree hebu Angalia mwenyewe!
Una haki kabisa kulala katika nyumba ya Baba
 
SI Kasema mwenyewe Njoo wote na wenye kulemewa na mizigo,nami nitawapumzisha, Sasa Mimi nimetua mzigo kwa Bwana,Sasa Mimi ni Nani nisisinzie kwa Baba, Baada ya kuutua mzigo! Setfree hebu Angalia mwenyewe!
Wee Kimwakaleli wee, uachage bana kutetea udhaifu!!
Hebu fikiria hivi: Baba yako mzazi anaita kikao cha familia kuongea mambo nyeti, halafu mtoto mmoja analala mbele yake. Hiyo ni nini kama sio utovu wa nidhamu.

Sasa kwakuwa Mungu ni Baba, na mahubiri ni sauti yake kwa wanawe, inafaa kweli mtoto kulala Baba anapoongea?

Kusinzia wakati wa mahubiri siyo “kupumzika,” ni kupuuza sauti ya Baba wa mbinguni. Right?
 
Kama mahubiri hayaeleweki kusinzia lazima.
Hayaeleweki kivipi? Kwani wanaohubiri si wanataja vifungu vingi tu vya Biblia? Na vyenyewe havieleweki? Au wahubiri wako huwa wanaongea Kichina?
 
Hayaeleweki kivipi? Kwani wanaohubiri si wanataja vifungu vingi tu vya Biblia? Na vyenyewe havieleweki? Au wahubiri wako huwa wanaongea Kichina?
Mimi ni Muhubiri na sijawahi Kumuona mtu anasinzia, na wakianza nawaona ninawarudia. Preaching is art not only spiritual
 
Naona yananiingia!Kweli sijui ni ni kuna Jamaa yangu alilala fofo,wimbo wa kitabuni ulipoimbwa aliamka akidhani kapofuka macho!
 
Hayaeleweki kivipi? Kwani wanaohubiri si wanataja vifungu vingi tu vya Biblia? Na vyenyewe havieleweki? Au wahubiri wako huwa wanaongea Kichina?
Kuhubiri ni kipaji kama hauna hicho kipaji hata ukitaja vifungu vyote vya Biblia watu bado watasinzia tu.
 
Kuhubiri ni kipaji kama hauna hicho kipaji hata ukitaja vifungu vyote vya Biblia watu bado watasinzia tu.
Ni sawa, Deinstein 01
Ngoja nikupe ushuhuda wa kweli. Kuna mhubiri fulani maarufu sana. Ana kipaji cha kuhubiri na ana lugha ya mvuto. Saa anapohubiri bado kuna watu huwa wanasinzia. Imebidi aweke watumishi wa kumsaidia kuwashtua wanaosinzia saa ya mahubiri. Sasa ili ujue mapepo yanahudhuria ibadani na kuwaletea watu usingizi, akimaliza kuhubiri na kuanza kuombea wagonjwa na wenye shida, mapepo yanalipuka kwelikweli. Hapo vipi, mkuu?
 
Inategemeana na mahubiri
Kuna mtu akihubiri unaona kabisa anawachosha tu.

Waumini nikama wanafunzi kuna mwalimu akiingia darasani mnaona anawachosha tu anakuwa hana ile sanaa ya ufundishaji.

Wengine ni. Shibe, uchovu, na stress

Mambo ya mapepo hayo ni vitu vya kiimani hata kuthibitika ni ngumu.
 
Pengine upo sahihi ya kuwa mapepo yanaweza kufanya watu wasinzie kanisani ila mimi naamini ya kuwa watu kusinzia kanisani inategemea kipawa cha mhubiri. Japo wengine husinzia kwakuwa wao sehemu yao pekee ya amani ni kanisani ,akienda nyumbani vita na kazini kwake pia hapakaliki.
 
Kumbe mapepo yanaingia hadi church na yanafanya kitu yanataka. Mapepo yanasumbua had mahala patakatifu, nilifikiri tukiingia church yanabaki nje huko kutusubir tukitoka
 
Wahubirio wakifunga anga na kumwomba Roho mtakatifu aachilie nguvu katika neno watu wapate kulielewa sawasawa na mapenzi ya Mungu;hilo pepo la usingizi litatoka wapi?hii sala inapasa kuombwa kwa imani kabla na baada ya kufika kanisani
 
Mmmh!! Ngoja nitarudi inshaalah
 
Kumbe mapepo yanaingia hadi church na yanafanya kitu yanataka. Mapepo yanasumbua had mahala patakatifu, nilifikiri tukiingia church yanabaki nje huko kutusubir tukitoka
Yanaingia tu. Lakini Makanisa yenye upako, hiyo ndiyo raha. Watu wenye mapepo wakiingia Kanisani, mapepo yanakemewa na kuwaacha watu hao huru. Wakitoka Kanisani wanakuwa wamepumzishwa kwelikweli mizigo yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…