Kusinzia Kanisani ni Dalili ya Kuingiliwa na Mapepo

Sijakuelewa mbongo_halisi
Unasema Biblia ni kitabu kilichotungwa na binadamu wenzetu, halafu wakati huohuo unasema unaamini Mungu anaongea nawe wakati wote. Sasa umemjuaje huyo Mungu kama sio kupitia Biblia unayoikataa?
Waebrania 10:25
wala tusiache kukusanyika pamoja[kanisani], kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri muonavyo siku ile kuwa inakaribia.
 
Ukiwa na njaa au madeni lazima usinzie wala siyo mapepo, za kuambiwa changanya na za kwako...

Cc: Mahondaw
 
Ukiwa na njaa au madeni lazima usinzie wala siyo mapepo, za kuambiwa changanya na za kwako...

Cc: Mahondaw
Kanisani saa ya mahubiri ni saa ya kupata chakula cha kiroho na kushibishwa. Mtu anayesinzia wakati huo, kama hana mapepo basi ni dalili kuwa hana njaa ya kiroho.
Mt 5:6-10
Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.

Maneno ya Mungu usiyachanganye na akili zako Smart911
 
Njaa mbaya na wala siyo mapepo...
 
Ukiwa na njaa au madeni lazima usinzie wala siyo mapepo, za kuambiwa changanya na za kwako...

Cc: Mahondaw
Saa ya mahubiri inawezekana Mungu anataka kukuambia njia za kupata pesa au kulipa madeni. Ukisinzia utazisikiaje njia hizo?
 
Uzuri wa Biblia ni kwamba kila mja anatoka na mistari yake anayoitaka na kujaza tafsiri zake zilizomkaa kichwani na zinaenda mjini...
 
Kwanini unakataa uwepo wa mapepo kanisani? Hujahudhuria ibada za makanisa ambayo pepo wanakemewa na kuwatoka wengi?
Za kuambiwa changanya na za kwako, ukishiba vizuri hakunaga kitu kama mapepo...
 
Saa ya mahubiri inawezekana Mungu anataka kukuambia njia za kupata pesa au kulipa madeni. Ukisinzia utazisikiaje njia hizo?
Ni mpaka uwe umeshiba, an empty stomach siyo kabisa...
 
Mchungaji anawadanganya hivyo ili msilale wakati anaomba sadaka
 
Uzuri wa Biblia ni kwamba kila mja anatoka na mistari yake anayoitaka na kujaza tafsiri zake zilizomkaa kichwani na zinaenda mjini...
Sio kweli, SankaraBoukaka. Kama unafikiri ni kujiwekea tu mistari unayotaka, weka hapa mistari yako kuhusu mada hii, uone ntakavyoizuia isiende mjini 😎
 
Tembea mtaani ndugu, uone kama 'Ombaomba' wanalala. Kila saa utaona wanatikisa kibakuli
Hawapo kwenye nyumba za ibada, hawamsikilizi mtu aliyeshiba tayari, wapo wakitafutia matumbo yao...
 
Hawapo kwenye nyumba za ibada, hawamsikilizi mtu aliyeshiba tayari, wapo wakitafutia matumbo yao...
Sasa ukienda kanisani si unaenda kutafuta chakula cha kiroho, kwanini usinzie saa ya kuingiza kitu rohoni?
 
Sasa ukienda kanisani si unaenda kutafuta chakula cha kiroho, kwanini usinzie saa ya kuingiza kitu rohoni?
Hao viongozi wanaokupa vyakula vya roho wanategemea wakukamue kwa sadaka baada ya hapo wanenda kula biriani na juice ya baridi...
Wewe unasinzia na njaa zako unasingizia mapepo...
 
Hao viongozi wanaokupa vyakula vya roho wanategemea wakukamue kwa sadaka baada ya hapo wanenda kula biriani na juice ya baridi...
Wewe unasinzia na njaa zako unasingizia mapepo...
Kutoa sadaka ni hiari. Mtu hatakiwi kulazimishwa. Tena ni heri kutoa kuliko kupokea(Mdo 20:35).
2 Wakorintho 9:7
"Kila mmoja na atoe kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu."

Kama hapo unaposali, unalazimishwa kutoa sadaka, basi hapo nakuruhusu uchanganye na za kwako. Kimbiaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…