Kusoma sana sio kigezo cha utendaji: Nehemiah Mchechu ana degree moja

Hata GENTAMYCINE nae ana Degree Moja tu ya Mawasiliano ya Umma na Uandishi wa Habari ( SAUT Mwanza 2006 - 2009 niliyotunukiwa na Genius Vice Chancellor wangu wakati huo Padre Dk. Charles Kitima Katibu Mkuu wa TEC )na sina mpango wa sijui Masters au Doctorate, ila nashangaa nakubalika na naogopwa kwa Madini yaliyoko Mtimani ( Kichwani ) mwangu huku Wengine wakiniita Profesa na Daktari wa Falsafa.
 
All in all, hakupaswa kusema kuwa hiyo degree moja aliyo nayo inamtosha; huwezi kujitathmini mwenyewe, watu wanaokuangalia/kukusikiliza ndio waseme kiwango ulicho nacho kinatosha. Zaidi ya hapo, kauli kama hizo zinaweza kuleta madhara kwa jamii, ikiwemo kukatisha tamaa kwa vijana kuendelea na elimu, kwani anayetoa kauli ni mtu mkubwa na anaeshimika na anachukuliwa kama kioo katika jamii!
 
Ni kweli hakupaswa kusema Ivo....anatuvunja moyo vijana tunaojiendeleza kielimu.Ukweli ni kuwa Kuna tofauti kubwa kati ya degree na masters, labda kama masters unayosoma unasomea vyuo ambavyo ni vya kawaida utabaki vile vile, ila Kuna value kubwa sana unaadd unaposoma masters.Ila kwa mtu mwenye position kubwa kama yake kusoma masters ni muhimu.
 
Kwa aina ya elimu ya Tanzania hata certificate(miezi 9) inatosha kabisa kuongoza idara/taasisi na hata nchi, ni elimu ya kijinga sn kukaririshana tu wala hakuna ujuzi wowote, masters na PhDs za Tanzania hazina lolote, zaidi ya sifa za kijinga mtaani, MO, GSM, Hersi, Rostam wote wana bachelors lakini wanafanya vizuri sn kwenye biashara zao mpk Ramaphosa kaamua MO awe mshauri wake wa uchumi.
 
Hapana jamaa yupo sahihi sn anatufundisha kuwa kile ulichonacho unapaswa ukitumie vizuri kikupe matokeo, maofisini watu wana masters kazi kubwa ni kubishana mambo ya mpira, mademu n.k siku inaisha hakuna ufanisi yaani hakuna tofauti ya mwenye certificate na masters, tunashindana kuongeza vyeti lakini ujuzi ni zero kichwani, tuna taka matokeo na siyo wingi wa vyeti.
 
Issue ni wingi wa vyeti au matokeo? mi sipingi masters je zinaongeza ufanisi wowote? fanya research ni aibu tupu kwenye ofisi za umma, watu wana soma masters iliwapande vyeo na siyo kuongeza ufanisi.
 
Sawa, na nafasi?

Ingekuwa ukiwa na kipawa unapanda nafasi wengi wangepanda

Sent using Jamii Forums mobile app
Suala la nafasi inategemewa unaaminiwa na nani, maana kama hawa waliaminiwa wakiwa na degree moja ina maana waliona kitu ndani yake, sidhani kama sasa inaweza kuwa hivyo sana sana watakuambia nenda kasome kwanza halafu tukufikirie
 
Ni kweli inategemea na mtu atakavyoipokea ila tukija kwenye suala la utendaji je ni sahihi kutomuamini mtu kwenye position nyeti sababu tu hana masters?

Maana tumeona siku hizi kigezo kimojawapo ni kuwa na masters lakini tukija kwenye suala la perfomance bado wengi tunakwama hapo
 
Profesa Maruma.
Kajibu ,"I was not feeling well", baada ya kubanwa kisawasawa na Tanzania kufilisihwa mabilioni.
 
Samia hata form 4 alizingua lakini amewashinda wote kwenye Uongozi
 
Kuna tofauti kati ya akili au degree za mchongo, ukinganisha na kipawa cha akili kutoka kwa Mungu kupitia vinasaba kutoka kwa wazazi hasa mama. Kwahiyo mtu mwenye kipawa cha akili lazima ataonekana wa tofauti iwe kijijini, kanisani au ofisini
 
Kuna tofauti kati ya akili au degree za mchongo, ukinganisha na kipawa cha akili kutoka kwa Mungu kupitia vinasaba kutoka kwa wazazi hasa mama. Kwahiyo mtu mwenye kipawa cha akili lazima ataonekana wa tofauti iwe kijijini, kanisani au ofisini
Nakubaliana na wewe kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…