Kusoma sana sio kigezo cha utendaji: Nehemiah Mchechu ana degree moja

kinadharia ndiyo kiuhalisia siyo. Kujua unachofanya ndicho kinakupa confidence.
hiyo confidence labda bar tu na vyuoni si field.
Sasa kujua si ndo lazima shule iwe kubwa mzee.....vinginevyo utakuwa na uelewa wa kawaida tu, unaelewa kwa nini kule mahospitalini kuna baadhi ya wagonjwa huwa wanapewa rufaa kuwaona madaktari bingwa, kama swala ni utendaji tu si wangewatibu hao hao madaktari wa kawaida, kwa hiyo mchawi shule tu.....​
 
Mkuu, shule kubwa ni lazima ufanane na performance, laa sivyo huo ni ubatili mtupu.
Peformance hata la saba anaweza ku-perform, unaperform vipi kwenye swala la kitaaluma na huna shule. Unajua kwa nini mahospitalini baadhi ya wagonjwa huambiwa wakawaone madaktari bingwa, shule hapo ndo ina determine mkuu siyo hicho unachoita sijui utendaji, huna shule utabaki kufanya mazingaombwe tu.
 
Mtu

Yoyote mwenye elimu ni msomi, ila kigezo cha elimu hiyo aliyonayo/aliyoipata inaleta manufaa gani kwa kada yake au eneo lake la ubobezi, jamii inayomzunguka na nchi kwa ujumla hapo ndio huwa panazua mjadala
Upo sahihi sn wengi wanasoma ajili ya mishahara ipande na kusubiri uteuzi lakini yeye mwenyewe ukimuuliza alisoma kwa sababu zipi hajui
 
Hao madaktari wanaosahau viwembe ndani ya matumbo ya wagonjwa baada ya operation kuisha hao bila ni mabingwa?

Vp wale waliomfanyia mgonjwa operation ya kichwa badala ya mguu??
 
Hao madaktari wanaosahau viwembe ndani ya matumbo ya wagonjwa baada ya operation kuisha hao bila ni mabingwa?

Vp wale waliomfanyia mgonjwa operation ya kichwa badala ya mguu??
Kufanya operation ni shule inahusika haijalishi kuna makosa yamefanyika ya kusahau mkasi......mambo ya kibinadamu hayo.
 
Huu ushauri awapelekee sua kwanza.

Wale jamaa kila siku hakuna hela,ikifika june unashangaa fungu linarudi hazina.
 
🤣🤣Mkuu hapana
Mie nilitoka vyema sana
Nikaamua nilitumikie taifa huku uraiani
Kuna wale Wenye pass
Hata kwenye magroup ya wasap ukichangia hoja wanareact hatari
Unagundua ni inferiority complex
Unakaa kimya,kuepusha malumbano
Basi ni fani na fani, fani yangu ya sheria, LL.B, wenye 1st Class hakuna kesi wanashinda, wenye pass, they are doing great!.

P
 
Kwani Msechu ana nini cha ziada?
 
Hahaaa, duh! Sikutegemea hii coment, mbavu sina. 😄
 
Ila tukumbuke pia watu kama hawa ambao wana degree moja lakini uelewa wao na competence huwa ni mkubwa,

Unaweza kuta tangu ahitimu ana practice kitu alichosomea, anafuatilia trends na mabadiliko mbali mbali yanayotokea katika kada yake au eneo lake la ubobezi, anafuatilia tafiti mbalimbali zinazofanywa katika eneo lake la kazi, na anahudhuria semina, warsha na makongamano yanayohusu sekta aliyopo hivyo uelewa wake na skills zinakuwa zinaongezeka kwa sababu ya kuongeza maarifa kila baada ya kupindi fulani baada ya kuhitimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…