Kusomesha mtoto kwa pesa nyingi halafu kuja kulalamika hakuna ajira( za kitumwa ) ni ujinga uliopitiliza

Kusomesha mtoto kwa pesa nyingi halafu kuja kulalamika hakuna ajira( za kitumwa ) ni ujinga uliopitiliza

Mto Songwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2023
Posts
6,683
Reaction score
14,060
Acha tuambizane ukweli kuhusu hali zilizopo ndani ya jamii zetu hata kama tusipopenda kusikia ukweli sawa tu.

Huu mtindo wa wazazi wa kitanzania kusomesha watoto kwenye shule zenye kuhitaji pesa nyingi na kuacha za kawaida huku hali ya maisha ikiwa haisomeki ni wa kishamba.

Mzazi anaye gharamia pesa nyingi kwa elimu ya mwanae hata kuuza mali zake au kujibana ili mwanae asome shule za ghali halafu baadae anaanza kulilia ajira za kitumwa mwanae apate hata kuhonga ni mtindo wa ajabu.

Ni bora hizo pesa uwekeze bank mwanao asome shule ya kawaida akimaliza unampatia akaanzishe maisha yake.

Au mnunulie asset yoyote mwanao wakati anasoma shule ya kawaida akimaliza itamsaidia huko maishani mwake.

Watoto wa masikini sana walio jipiga piga shule za kawaida kusoma mpaka kumaliza hao kidogo unaweza sema ndio wanapaswa kulalamika kukosa ajira sio yule ambaye mzazi kapoteza pesa zake kwenye elimu kwa ajili ya kuja kulilia ajira za kitumwa.

Wazazi wa sasa wekezeni pesa za watoto wenu bank na kwenye asset mbalimbali halafu peleka shule ya kawaida ili usije kulilia ajira za kitumwa kwa mshahara wa masikitiko.

Hii haiwahusu wale wenye connection za wakubwa huko serikalini maana wao hata wakipeleka watoto wao shule za gharama uhakika wa ajira upo.
 
Jamaa ana hoja nzuri sana.

Watu wanajifanya hawajaiona

Ajira hakuna bado mtu analipa milioni mbili ama tano kwa mwaka mtoto afundishwe elimu ya msingi.

Halafu anaenda kugombania ajira
 
Kuna ukweli hapa.

Ila Umesahau kuwakumbusha pia kuhusu masomo ya kusoma/kozi za masomo ambazo zitamuwezesha mtoto kujiajiri kirahisi hata akikosa hiyo ajira yenyewe.

Inshort watoto wajue dunia inaelekea wapi.
 
Kuna ukweli hapa.

Ila Umesahau kuwakumbusha pia kuhusu masomo ya kusoma/kozi za masomo ambazo zitamuwezesha mtoto kujiajiri kirahisi hata akikosa hiyo ajira yenyewe.

Inshort watoto wajue dunia inaelekea wapi.
Ukweli upi hapo aliouandika?
Hivi kuna mtu anayeweza sema kwa uhakika dunia inaelekea wapi?
 
Jamaa ana hoja nzuri sana.
Hoja gani hiyo isoyokuwa na ukweli au ushahidi?
Au ndio tuseme hiyo shule uliyosoma ulienda kusomea uongo?
Watu wanajifanya hawajaiona
Wewe umeiona halafu umeweka nini sasa?
Ajira hakuna bado mtu analipa milioni mbili ama tano kwa mwaka mtoto afundishwe elimu ya msingi.
Ulitaka iwe vipi? Una mbadala au Ushauri wa kutengeneza ajira unazoziona zitalipa?
Halafu anaenda kugombania ajira
Kuna tatizo gani kugombania ajira? Ushasikia wapi ajira haigombaniwi?
 
Mzazi anapeleka mtoto UK chuo halafu anataka kuhonga mtoto aje kuajiriwa manispaa Tabora...
Kama ana shule nzuri why asiajiriwe huko huko UK?
Mzazi Wa Hivyo ni mpuuzi.
 
Jamaa ana hoja nzuri sana.

Watu wanajifanya hawajaiona

Ajira hakuna bado mtu analipa milioni mbili ama tano kwa mwaka mtoto afundishwe elimu ya msingi.

Halafu anaenda kugombania ajira
Aisee...
Watu ni masikini Sana humu...

Hivi mkuu Kama wewe na mke wako mna biashara tu ya kuku ..mayai.

Milioni 2 ni hela kwa mwaka. Tena unalipa kwa 4 terms installments.

Au ni mtumishi tu wa serikali.. Mwl. Milioni ndo mnatupigia kelele hapa!??
 
Kama vipi mkubwa anzishana Uzi wa wazazi wanaowalisha watoto wao wa kike misosi ya gharama kubwa halafu mwisho wa siku wanaolewa na sisi mabodaboda au mapopoma kama GENTAMYCINE
 
Back
Top Bottom