Kwamba hawa nao tumawapa majukwaa ya kisiasa na kuwashangilia?
Kwamba tuna hata wenye kujidhania kuwa ni wenye hoja kuliko hata wenye CV zao zinazojulikana kimataifa?
Kwamba tumefikia hatua ya kuwaacha hata wapuuzi kuwanyanyapaa wenye akili zao?
Na Bado tupo tupo tunakenua? Ama kwa hakika haya ni matokeo ya wazi ya ombwe litokanalo na uongozi ulio dhaifu. Watu aina hizi walipaswa kukemewa pasipo na kuwaonea haya.
Udhaifu, iliwaudhi mno aina za kina Yobo. Tusipende mno kusifiwa hata tusipostahili. Udhaifu si tusi, bali dhana sahihi ya ukosoaji yenye lengo zaidi la kujenga.
Kwanini wanakofanikiwa kwenye harakati zao, huko viongozi wao huhama vyama na hata wakabadili washirika bila ya unyanyapaa wa kipuuzi kama wa huku kwetu?
Laila alijiunga na KANU, akawa na Ruto, Kibaki, Kenyatta, Mudavadi, Wetangula, Musyoka, nk na matokeo yake huko mwenye nchi mwabanchi? Ila sisi tumeshindwa kuelewa kutokuwa na maadui wa kudumu kuna faida kubwa kwa nchi zaidi ya faida binafsi.
Kwetu walikuja kina Lowassa(r.i.p), Sumaye, Ngombale(r.i.p) nk ambayo ilikuwa ni hatua njema mno. Tulipiga hatua mbele kiasi gani kipindi hicho? Ni mamburula peke yao wenye kuthubutu kuyabeza mafanikio ya kipindi hicho.
Kwanini iwe dhambi kwa Mbowe, Lissu au Msigwa au awaye yote kuhamia CCM wakati wowote? Au kwa Nape, Januari, Mpina au awaye yote kuhamia CHADEMA au ACT Wazalendo? Hatuwezi kuyaweka maslahi ya nchi yetu mbele?
Utayasikia mamburula mburula, "hatumtaki huyo!" Kwani wewe ni nani ndugu? Au hata kwa CV yako ipi basi yenye kuweza kutushawishi hivyo na wengine basi?
Kwamba kama vipi mkaanzishe chenu au mhame chama? Looh! Kwanini hayo yasiwahusu ninyi?
Shughuli ni watu. Hii nchi haiwezi kukombolewa ndani ya wimbi la ujinga ndugu zangu.
Habari ndiyo hiyo.