Kutafuta views, followers na trending kusitufanye kuvuka mipaka ya maadili, huyu mtoto hakupaswa kukaririshwa haya matusi

Kutafuta views, followers na trending kusitufanye kuvuka mipaka ya maadili, huyu mtoto hakupaswa kukaririshwa haya matusi

Sheria isipowekwa nakwambia ipo siku utakuta video za pornography ndo zinapostiwa tuuu ....
Serikali yetu as long as haujaikosoa au kukosa Chama basi fanya kila unachotaka hakuma shida. Uharifu hauwezi kuisha. Huko Youtube ni aibu tupu
 
Kwakweli sijui wazazi wengine wanawaza Nini.. Mungu saidia vizazi vyetu
 
WIZARA ya watoto ipo, polisi wapo wanashindwa kukamata wazazi na mtoto wao kuwapeleka mahakamani? Mtoto anaongea hivi kwenye vyombo vya habari anaangaliwa tu! Basi hatuna serikali!
 
Na usikute huyo mtoto tyr washampitishia mdudu… wazazi wengine sijui wanaleaje watoto?? Hapo yupo mtu mzima anamrekodi..!!
 
Cha ajabu utakuta huyo dogo anapata followers wa kutosha kwa huo upuuzi, mamlaka zichukue hatua haraka sana!
 
Na mtengeneza content akai-pin kabisa.... Akiamini ndiyo jiwe lake la nguvu la kukusanya views..

Screenshot_2025-03-01-16-13-45-732_com.zhiliaoapp.musically-edit.jpg
 
Nikikutana na vitu kama hivi huwa nasikia maumivu makali sana. Kwanini tuwashirikishe watoto kwenye upuuzi wetu?
Wazazi kuna mahali walipwaya katika malezi siku nyingi sana. Very disturbing 😕
 
Tusitafute views kwa kuwahusisha watoto na vitendo na maneno ambayo hayazingatii Parental Guidance.

Huyu mtoto anaongea matusi makubwa sana ambayo ni kwa watu wazima tu ndiyo wanapaswa kuyatamka.
View attachment 3254752
Hayo maneno itakuwa wamechomeka tu, angalia lips zake zinaenda tofauti na maneno. It's bad kuwachafua watoto kiasi hicho kwani wanachafua wazazi/walezi wa mtoto pia. This clip is as fake as fvck.
 
Back
Top Bottom