Kutafuta views, followers na trending kusitufanye kuvuka mipaka ya maadili, huyu mtoto hakupaswa kukaririshwa haya matusi

Kutafuta views, followers na trending kusitufanye kuvuka mipaka ya maadili, huyu mtoto hakupaswa kukaririshwa haya matusi

Kama Dr gwajima yupo humu atagiwe aone aanze kufuatilia.
 
Content creator wa tanzania hawa
Inasikitisha kwakweli

Uyu dogo bado mdogo sana
 
Vijana wengi siku hizi wamejiingiza huko mitandaoni kusaka likes na followers sijui ndio wanalipwa kwa dizaini hiyo.

Kuna clips za ajabu ajabu nyingi mno, madogo wanakalilishwa kama hivyo na jitu zima linarekodi na kutia mbwembwe za vicheko ili apate likes...
 
Muheshimiwa waziri Dkt. Gwajima D naomba usilifumbie macho hili suala elekeza walimu wa Halmashauri zote wamtambue huyu mtoto kama ni mwanafunzi kwenye shule yao ahojiwe ni nani aliemrekodi hii video, kisha mtu huyo achukuliwe hatua za kisheria maana ni wazi kabisa kaelekezwa kuongea maneno haya, hiyo ni Child abuse, record hizi zinavyobaki mitandaoni huenda zikaharibu maisha yake ya baadae.
 
Back
Top Bottom