Kutakuwa na tatizo katika usahihishaji wa mtihani wa somo la Elimu ya Dini ya Kiislam Kidato cha Nne

Kuna marks na grading
Unaweza pata marks 90 ila ukawekewa grade D
 
Kwani uwa inasahishwa na nani mkuu?
Mleta hoja hakujiridhisha na taarifa kabla ya kuleta hoja yake hapa, na pengine hafahamu hiyo mitihani huwa inasahihishwa na kina nani!

Na hili limekuwa tatizo kwa watu wengi wakidhani mitihani ya dini kama bible au Islamic husahihishwa na waalimu wa masomo ya kawaida, kumbe sivyo
 
Mtoa mada usijali.

NECTA huw wanatoa vitabu vinavyoelezea jinsi mwanafunzi alitakiwa kujibu maswali ya mtihani husika.
Na pia huelezea maswali yaliyoleta utata kwa watahiniwa.
Ni ripoti nzuri sana.

Walimu wetu wangekuwa wanafatilia zile ripoti/vitabu vya NECTA watoto wangeimarika sana kwenye kujua namna bora ya kujibu maswali ya mitihani ya Taifa
 
The end determines the beginning..wewe ulikua kilaza tu..kule kwingine ulibahatisha..necta ulikua pekeako ukakosa wa kuegelezea ndio mana ulifeli.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Uzuri ni kwamba sikufeli pekeyangu....aliefaulu kwa alama kubwa alipata "C".
Na huyo alikuwa anafundisha elimu ya dini pia.

Sijawahi kuwa kilaza...na sitakuwa kilaza.

'The end determine the beginning...', Ni msemo wenye mashaka.

Aliyepata "A" mwisho haina maana kuwa alipata "A" mwanzo.

Kuna aliyepata "A" mwanzo but mwisho akapata "D".

Kuna sababu ya yote hayo kutokea...

Usahihishaji Mbovu au Buddhist walikuwa kazini siku hiyo.
 
Mi naona hayo masomo ya dini serikali iyafute kabisa maana yamekuwa chanzo cha migogoro ya mara kwa mara baina ya Serikali na wanafunzi wa dini hizo. Wanaotaka kusoma dini wakasome kwa utaratibu wao.
 
Waalimu wa dini wengi tu hata ukienda private schools huwa sio walimu kitaaluma. Mtu kasoma mpaka wapi hata hana profession ya ualimu anakuja analipwa hela kidogo yeye akiwa na akili ya kujitolea na wakati huo kukubali kwa kuwa hana kazi. Huyo ndio anasahihisha wanafunzi wake na kuwapa alama za juu wakienda NECTA wanakosea. Unahisi ukimchukua Padre asiyejua kufuata syllabus akakufundisha Bible Knowledge utapata hata C?

Kuhusu shule za Kiislamu zenyewe hapo ndio nashangaa pia nazo zinakosa kufaulisha hili somo. Waseme shida iko wapi
 
Masomo ya dini mitihani na usahihishaje wake hufanywa na hao hao wanaowafundisha.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ile shule ya mbeya haijatoa A kwenye somo la dini ya kiislamu mbna top 4 wote wametoka kwao au wote ni Christian

Sent from my TECNO CC7 using JamiiForums mobile app
 
Mi naona hayo masomo ya dini serikali iyafute kabisa maana yamekuwa chanzo cha migogoro ya mara kwa mara baina ya Serikali na wanafunzi wa dini hizo. Wanaotaka kusoma dini wakasome kwa utaratibu wao.
Hili ndio suala la msingi..masomo wafundishane huko madrasa au Sunday school..wajaziane maks wenyewe.

Serikali haina dini nashangaa kuundekeza huu upuuzi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂😂😂Hwataki mfaulu sana mtakuja chukua vyeo vyao vya ushkhe, natabia tu
 
Siku hizi madrasa au kukalilishana kiarabu tukizani tunapack dini kichwani kumeonekana ni swala lisilo both kwa wazazi na wanafunzi wenyewe.Wamegundua elmu akhela haina mpango wowote na unaongeza ma Complicators wa maisha tu vivyo hivyo na upande wa dini ya Kikristo watu wameona michosho hata kwenda kanisani kwa sababu kunasababisha kupoteza hela kwa hicho kinachoitwa sadaka na zaka.We haingii akilini kanisa linajengwa kwa michango ila ikifika muda muumini anataka kujenga nyumba kanisa na viongozi wake wanasema fumbeni macho tuombee mpate nyumba PUMBAFUU makanisa yamekuwa ni ya watu wenye stress za maisha na wazee
 
Masomo ya dini mitihani na usahihishaje wake hufanywa na hao hao wanaowafundisha.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Issue ni kwamba wanaolalamika ni wengi...
Na lalamiko ni moja, kuwa wanahisi wanakoseshwa makusudi.

Inabidi hilo liangaliwe kwa jicho pevu...
Hatakama wanaosahihisha ni hao walimu wa dini.
 
Kwa hiyo unahisi walisahisha Maaskofu na mapadree au? Sasa hujuma inatokea wapi?
 
I see!!!
 
Mnakaririshwa madude ya ajabu ajabu. Mara sijui unaanza kusoma kutokea kulia kwenda kushoto, Sasa kwa nini msifeli.
 
We ile lugha ya mtume usiichukulie poa bila mijeredi huwezi kuishika,uliza walimu wa madrasa watakwambia bora kichina ni rahisi kuliko kiarabu
Kiarabu ni lugha nyepesi kuliko hata Kiswahili ambacho ni mtoto wa kiarabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…