Muhimu ni kuwekeza juhudi kwenye kuoambana na maisha kuwa mwema na mwenye huruma na kuzungumza na Mungu wako bila kumfokea wala kwenda huko kwa kina Mwamposa au misikitini.REFFER wazungu ndo waliotuletea dini ila mambo kwenda church wameachana nayo wamewekeza jitihada na matumizi ya akili leo wamekuwa blessed kushinda sisi mabingwa wa kunena kwenye ma sinagogi ya kina Suguye.
Nimeshindwa kukuelewa hao wazungu wamekuwa blessed kwa sababu ya kuwekeza kwenye matumizi ya akili au kwa kuwa wema na wenye huruma na kuzungumza na Mungu bila kumfokea?
Grading mara nyingi inalenga kuinua watu na sio kufelisha watu. Grading hufanywa na computer na computer haitambui kama hili in somo la dini au la Physics. Ngoja niishie hapa
Sikuzote vilaza hutafuta mtu wa kumtupia lawama..jitahidi msome..kama somo hilo kuna wanao pata A unaweza kusemaje usahihishaji mbovu.
Msituchoshe na uvilaza wenu.
Kwanza serikali iache kabisa kuhusika na haya masomo ya dini waache shule za dini husika zijitungie na kusahihisha mitihani yao kupitia mabaraza yao ya dini.
Achana na huyo jamaa hajui kitu. Mwanzoni walisema shule za kiislam zinafelishwa imekuja FEZA waturuki waislam inaingia Top ten. Shule za kiislam za kibongo akina Qiblaten bado hali mbaya
Hili jambo ni fikirishi sana, Mimi binafasi wakati nilipofanya mtihani wa kidato cha nne, na ni zaidi ya 15 years nyuma katika somo nililifanya kwa uhakika zaidi na nikiwa na tamaa ya kupasi vizuri kuliko yote ilikua ni Islamic Religion, La kushangza niliishia kuja C huku nikiwa siamini kilichotekea, Yani somo nililolifanya kwa ufanisi zaidi niliishi kupata grade sawa na masomo niliyojibu kwa kubahatisha bahatisha.
Pengine watahiniwa Lugha ni changamoto. Somo na vitabu vyake unafundishwa kwa Kiarabu, Kiswahili na Kiingereza halafu unafanyiwa tafsiri.
Je waalimu waumini wanaojitolea , ma ustadh, imamu na masheikh wanaofundisha wameiva ktk tafsiri.
Pia je wanafunzi nao wanamudu lugha zote tatu kwa ufasaha yaani Kiarabu, Kiswahili, Kiingereza ili wamuelewe mfundishaji pia wanapojibiidisha kwa kuchukua masomo ya ziada ktk vitabu vya dini maktaba ?
Inawezekana wasahishaji wameiva sana ktk somo la dini na wanazuoni wahadhiri wahitimu wa vyuo vya Al Azhar Egypt, Iran, Lebanon walipewa vilemba na masheikh wakubwa au ma ayatollah kuwatambua kuwa ni ma guru wa elimu ya dini kiasi wakipitia mitihani ya wanafunzi hawaridhishi kabisa na majibu, maelezo,ufahamu, nukuu zilizopo ktk majibu ya mitihani hiyo ?
Tamati je kuna ombwe / gap kubwa kati ya wanazuoni waliohitimu katika vyuo tajwa ulimwenguni vya dini ya Kiislamu na yale wanayofundishwa wanafunzi wa shule za Tanzania.
Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania
(NZIMA)-SIMULIZI YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF (1939 -2020) - HISTORIA YETU part 1
KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)
Sheikh Abdallah Seif Linganaweka anatujuza kuwa Wenyeji wa Lindi jina Lao la asili ni Wakudewe kwa sasa almaaruf wanafahamika kama waMachinga wa pwani ya Lindi.
Babu yake Babu Abdallah Seif alikuwa mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga mwenye watumwa baada ya kuwazidi wanyonge majirani kuja kuwatumikisha kujaza vyakula. Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi. Baada ya kuja mkoloni Muingereza nchini Tanganyika, aliua ufalme na kubakiza uchifu. Sehemu za pwani ziliathirika kwanza kwa kupoteza ufalme mapema kabla ya watu wa bara.. Pwani wakabakia na usheikh na uchifu... usiokuwa na nguvu kama falme za asili za maeneo yao Lindi / Kilwa kabla ya kuja ukoloni...
Sheikh MbogaBure mjuzi wa lugha ya Kiarabu, dini pia mmoja wa waanzilishi wa madhehebu ya Shia Tanzania amuunganisha Mzee Abdallah Seif kupata scholarship kwenda Baghdad, Iraq mwaka 1968 kusoma zaidi dini...
Kijana Abdallah Seif mwaka 1968 alipokwenda Kijijini ashutumiwa kupotea kwa kuukumbatia u-Shia mojawapo ya madhehebu ya dini ya KiIslamu, wakati wengine wote ni Sunni. Lakini babu yake msomi wa dini madhehebu wa Sunni anayetambulika Lindi na Kilwa hakuwa anatoa shutma zozote alikuwa msikivu na kumtia moyo Abdallah Seif asome zaidi na ili kuifahamu dini vizuri zaidi.
Kilichomsukuma Sheikh Abdallah Seif kuvutiwa na u-Shia ni namna masheikh wa ki-Shia walivyokuwa wazi (tabligh) kukaribisha maswali tofauti na madhehebu mengine ya KiIslam ambapo kijana hakuruhusiwa kuhoji na pia kuuliza maswali ilikuwa inachukuliwa ni utovu wa nidhamu kwa waalimu au masheikh wake.
Safari ya Sheikh Abdallah Seif wenzie vijana wakiwemo kina Sheikh Isihaka Pingili kwenda Iraq kwa meli iliwachukua mwezi mzima kupitia bandari mbalimbali za Zanzibar, Tanga, Mogadishu, Bahrain na kuishia Basra nchini Iraq na kutua katika chuo cha Hawza mji wa Najaf Iraq
Ujio wao Basra, Iraq ulileta tafrani kwa mwenyeji wao Mpakistani mfanyabiashara mkubwa nchini Iraq enzi hizo na kupelekea Saadam Hussein kumshutumu mfanyabiashara huyo tajwa kuleta majasusi wa kiAfrika ikumbukwe ndiyo kwanza Saddam Hussein na chama chake cha Baath walikuwa wanajaribu kushika hatamu za kuongoza nchi baada ya mapinduzi nchini Iraq. Mpakistani huyo alinyongwa mwaka 1969 pamoja na wafadhili wengine kama kuna Bakri Sadr waliowezesha ujio wa vijana wa kiAfrika kuingia Iraq kwa dhumuni la kusoma dini.
Kutokana na hilo ikabidi Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine wa kiAfrika waondoke Iraq mwaka 1970 kwenda Lebanon kwenda kuendelea na azma yao ya kusoma dini.
Sheikh Abdallah Seif wakakaa Lebanon kuanzia mwaka 1970 mpaka 1978 ambapo mara nyingine masomo ya dini yakaingia changamoto baada ya vita baina ya Wapaletina waliokuwa kambi za ukimbizi Lebanon na waLebanon wenye nchi na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mwaka 1978 Ikabidi Sheikh Abdallah Seif na wenzie wahamie nchi ya jirani ya Iran kwenda katika mji wa Qom city kuendelea na masomo yao ya dini. Iran ilikuwa imetulia nchi ya amani chini ya utawala wa mfalme (Shah) Mohammed Reza Pahlavi Historic Personalities of Iran: Mohammad Reza Shah Pahlavi miaka 7 waliakaa Iran wakiendelea kusomeshwa.
Wakati wa likizo Iran wengine wenda Ufaransa kuchuma zabibu mashambani au kufanya kazi sehemu za utalii wa ndani wa Iran au kuchukua mabusati ya kushona ya Iran yanayosifika Uarabuni kote kwenda kuyauza ktk nchi mbalimbali za Arabuni ndivyo mwanafunzi kama Sheikh Abdallah Seif na wenzie vijana walivyojiongezea fedha za kujikimu na kupeleka kiasi cha pesa nyumbani Tanzania.
Hatimaye mwaka 1980 baada ya ukisoma kwa miaka 11 nje ya Tanzania ,walitunikiwa shahada ya baccalauréat ya masomo ya dini na kurejea Tanzania. Kwa miaka hiyo 11 ughaibuni pia waliweza kusoma elimu ya secular kiwango cha sekondari kwa njia ya posta masomo ya nchi ya Uingereza kwa msaada mkubwa wa swahiba wa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria Jenerali Yakubu Gowon. Swahiba huyo alikuwa mfanyabishara wa vituo vya mafuta na makazi yake Uingereza.
Mahojiano haya yanakuja kwa hisani kubwa ya Ammar Dachi yaliyemshawishi Mzee Abdallah Seif kufunguka historia ya mapito yake, ukoo , ilmu na utafiti wa mafuta 1955 na pia ujio wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania
HISTORIA YA ABDALLAH SEIF (1939 -2020) Part - 2
Sheikh Alhaj Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mnan’gole sehemu za Dimba mkoa Lindi Tanzania anaendelea kusimulia kazi kubwa aliyofanya ya kujitolea ya kueneza dini.
Sheikh Abdallah Seif anasisitiza umuhimu wa ilmu na elimu kwa wanazuoni wote wa KiIslamu.
Anasema ili sheikh awe mwanazuoni aliyekamilika kufundisha chuoni lazima kusoma ilmu ya dini kwa angalau miaka 15.
Anakumbuka alivyokuwa mjini Qom Iran akisoma chuoni alionana na wazee wa miaka 70 wakijiendeleza na kuwaambia wao vijana kuwa inahitajika miaka 35 ili kuielewa dini nje ndani kwa ufasaha. Wazee hao walicheka waliposikia vijana Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine toka Afrika wakisema wanataka kusoma dini kwa miaka 5 mpaka 10 tu ilihali wametoka Afrika na kuwaambia bila kupepesa macho kuwa ili wawe wabobevu wafikirie miaka angalau 15 ya ilmu ya dini ngazi ya chuo.
Hivyo akiwa amepikika kwa elimu tosha ya kidini baada ya kufanya kazi kwa takriban miaka 11 nchini Tanzania, mwaka 1990 sheikh Abdallah Seifu alikwenda Nampula jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique kufanya kazi ya dini.
Kisha sheikh Abdallah Seif alishuka mpaka mji mkuu wa Maputo Mozambique na alisaidia kufungua taasisi rasmi inayotambulika na serikali na kupewa leseni iliyosajiliwa Maputo Mozambique kwa ajili ya taasisi ya Shia Ithna-Asheri Muzdalifah . Sheikh Abdallah Seif anazungumza lugha za Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na Kireno.
Source : Asadiqmedia
RAMBIRAMBI NA WASIFU - Marhum Sheikh Abdallah Seif
Kuna waziri mmoja wa miaka ya nyuma alikomalia suala la matumizi ya namba badala ya majina ktk mitihani. Ilipokubalika idadi ya waislamu wanaofaulu ikaanza kuongezeka. Inawezekana na kwenye Islamic knowledge kukawa na shida fulani.
Baraza la mitihani waangalie.
Imekuwaje hakuna wastani mzuri katika somo la Elimu ya Dini ya Kiislam kwenye matokeo ya kidato cha nne?
Kuna walakini katika usahihishaji.
Serikali ifanye uchunguzi.
Ili ukweli ubainike. Kama ni watoto wote waliofanya somo hilo hawana uwezo wa kupata A tujue. Ripoti itolewe na iwe wazi kwa kila mtu kuisoma. Ili wazazi waondoa malalamiko yao baada ya kujua kwamba watoto wao hawana uwezo wa kufaulu grade A ya somo hilo.
Asante
Ungekuwa unajua namna mitihani inavyotungwa na kusahihishwa usingeleta hii mada yako hapa.
Nikwambie tu kama mtihani una maswali 10, basi utapitiwa na watu wasiopungua 14.
Walimu 10 wanaofundisha hilo somo watasahihisha kila mtu swali lake kwa Chain. Karàtasi ikitoka hapo inapita kwa Checker anakagua kama maswali yote yamepitiwa na alama alizopewa in sahihi. Karatasi inapita kwa mtu wa kutotal alama. Baada ya hapo inaenda computer kujazwa. Baada ya kutoka computer kuna watu tena wanahakiki kama alama za computer ni sawa na zilizo kwenye karatasi. Mchakato n mrefu mno kuonewa sio rahisi kama unavyodhani
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.