Kutakuwa na tatizo katika usahihishaji wa mtihani wa somo la Elimu ya Dini ya Kiislam Kidato cha Nne

Kipi muhimu sasa kwenye maisha?
 
Kusahihisha mitihani ni jukumu la walimu wateule, lakini linapokuja suala la matokeo ni jukumu la Baraza kupitia syndicate ya watu wachache. Watu hawa kwa kiasi kikubwa ndio huamua, kupanga na kupangua vile wanavyoona inafaa.
Ndio maana si ajabu kusikia walimu walioenda kusahihisha wakisema mwaka huu somo X wanafunzi wamefanya vibaya Sana, lakini yakija matokeo wanafunzi wamefaulu kwa kiasi cha kupaa mno.
Binafsi nadhani, ni wakati sasa kufanya mabadiliko ya kimkakati katika mambo kadhaa yanayohusu mitihani. Sina shaka na sifa za watendaji wa baraza, lakini umakini na kujiridhisha katika masuala yanayoweza kuibua taharuki yafanyiwe kazi ipasavyo.

Ndimi, mwalimu wa Chekechea
 
Kwani Islamic linatakiwa kufindishwa na mwalimu mtaalam kwa kifata silabasi au hata ustaadh anaweza fundisha huko madrasa?
 
[emoji23][emoji23][emoji23]walisahihisha Walokole
 
Jamaa yangu alisimamiaga paper necta, madogo baada ya kupiga paper one, hawakurudi kupiga paper two, walipoulizwa kila mmoja anasonya tu!!!
 
Enzi za Ndalichako akiwa akiwa Katibu Mkuu(NECTA) Waislamu waliwahi kuandamana kwenda NECTA kupinga matokeo ya namna hii.

Baadae ripoti ilitoka na kubainika kulikuwa na walakini..
Unaweza kutuwekea hapa hiyo ripoti ili tuamini sio umbea
 
Kipi muhimu sasa kwenye maisha?
Muhimu ni kuwekeza juhudi kwenye kuoambana na maisha kuwa mwema na mwenye huruma na kuzungumza na Mungu wako bila kumfokea wala kwenda huko kwa kina Mwamposa au misikitini.REFFER wazungu ndo waliotuletea dini ila mambo kwenda church wameachana nayo wamewekeza jitihada na matumizi ya akili leo wamekuwa blessed kushinda sisi mabingwa wa kunena kwenye ma sinagogi ya kina Suguye.
 
Nahisi kuna shida eneo hilo
 
Aisee...
 
Mtihani wa dini wa Taifa mwaka 2012, hakuna swali ambalo sikulifahamu, nilijibu maswali yote tena kwa kujiamini. Matokeo yalipotangazwa....Nilikutana na "F" ya Islamic knowledge.
Inategemea ulichokuwa umefundishwa au kujifundisha ni nini na jibu sahihi ni nini. Vinaweza vikawa ni vitu viwili tofauti, dini sio sayansi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…