Kutambulishwa ukweni na kutolewa mahari sio uhakika wa ndoa

Kweli mahari sio ndoa.
Nilizaa na demu wakaniletea zengwe ukweni hawanitambui mpaka nitoe mahari nioe na kumkomboa mtoto.
Nikatuma madingi dingi yangu mzazj nae akiwepo,kufika huko wapandishiwa dau na vijembe vya kutosha wakapigwa.
Ding kurudi home kamaindi kinona,akaniambia tumepigwa hela ndefu wakati demu mwenyewe ni mfupi afadhali angekuwa mrefu,nikaamua kumtema na kusamehe mahari mana demu alikuwa na nyodo pia.
 
Mashart kama yapi, yasije kujikuta na mie [emoji16][emoji16][emoji16]
Vipi mliwekeana range yaan asizidishe kiasi flani?
Yes tulikaa pamoja kujadili nikamwambia mahari usinitajie kubwa (kwa imani ya dini yetu mahari anataja binti mwenyewe) kwahiyo nikampanga fresh na akakubali, tena nakumbuka nilimwambia anitajie laki tano.
Maana nilikuwa nishatengeneza kibanda cha wakala cha tigopesa bado kununua laini tu, na kilakitu alikuwa anajua.
Na kipindi hicho nilikuwa nimepunguzwa kazini yaani sina kazi na yeye anajua kuwa kazi nimeachishwa.
Baada ya kwenda kuchukua majibu naambiwa binti anataka milioni moja, na mkaja wa baba na mama laki nne Jumla milioni moja na laki nne. Wadau mnaweza kuibeza hii pesa na kusema sio nyingi ila kwa Mazingira yake na nilivyojitoa Kwake kwamtu mwenye akili asingetaka hiyo pesa, angetaka hata nimuoe bure kwa maisha yake yalivyo magumu.
Halafu cha ajabu sijawahi kumla na msimamo wake ulikuwa hadi nimuoe ndio tukutane, na kwamsisitizo wazee wake wakaandika mpaka kwenye barua ya majibu kuwa nisimguse binti yao, wakati tayari ameshazalishwa (single mother) na baba wa mtoto amemkimbia, na kwa huruma mimi ndiye nilikuwa nimebeba majukumu ya mtoto wake kwa kumlipia ada, nauli ya shule ya kilasiku, na nikamkatia bima ya afya.
Nikaona hapa hapanifai.
 

Dingi alipatwa na hasira kuona mtoto wake hajui kuchagua anazozoa tu videmu vifupi visivyoeleweka![emoji28][emoji28][emoji28]wala sio kutajiwa mahari kubwa aliona tu umechagua utopolo
 
Mahari ni Ndoa dogo...waulize wazee wako kabla hawaletewa dini za wazungu..? Shida mko brainwashed kiwango cha mwisho...ukishalipia mahari chukua mkeo mkaishi kisha nenda serikalini kuchukua cheti cha ndoa.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kwahy ulitaka mahari iwe laki tano ukijumlisha na mazaga yote yaan mkaja wa mama, baba sijui blanket la babu nk

Cc Kipapi
 
Laki tano nyingi
Mkuu kwahy ulitaka mahari iwe laki tano ukijumlisha na mazaga yote yaan mkaja wa mama, baba sijui blanket la babu nk

Cc Kipapi
 
Kuna binti namfahamu tunasali nae na ni rafiki wa mdogo wangu...alitolewa mahari 3 zikarudishwa (sababu hakutulia)..akaamua kumrudia Mungu mwaka Jana kaolewa na mkarismatiki mwenzie.

Kuna Dada namfahamu alitolewa mahari na sendoff ikafanywa..alikuja Achwa kwenye mataa siku ya ndoa dah!!..

Una aina 'fulani' za wadada unaowafahamu, wanafanana!
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Huyo dada hatari
 
Hahaha dingi noma
 
Hizo hazikua akili za huyo binti, kuna watu walimshauri.
 
Hizo hazikua akili za huyo binti, kuna watu walimshauri.
Inawezekana ikawa hivyo, ila ndio sababu ya mimi kuachana nae.
Ikiwa mwanzo tu watu wamemshauri ujinga amekubali, je ndani ya ndoa akishauriwa ujinga atakataa?
 
Ila nawe ulipelekaje mbele tarehe pasipo kuongea nae? Au ulipoongea nae ndio akakuwakia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…