Kutambulishwa ukweni na kutolewa mahari sio uhakika wa ndoa

Kutambulishwa ukweni na kutolewa mahari sio uhakika wa ndoa

Dingi aliamua kukuchana, pisi uliyoichagua/unayotaka mbovu, haina viwango!

Nawapenda wazee wa namna huyo very direct.
Kweli mahari sio ndoa.
Nilizaa na demu wakaniletea zengwe ukweni hawanitambui mpaka nitoe mahari nioe na kumkomboa mtoto.
Nikatuma madingi dingi yangu mzazj nae akiwepo,kufika huko wapandishiwa dau na vijembe vya kutosha wakapigwa.
Ding kurudi home kamaindi kinona,akaniambia tumepigwa hela ndefu wakati demu mwenyewe ni mfupi afadhali angekuwa mrefu,nikaamua kumtema na kusamehe mahari mana demu alikuwa na nyodo pia.
 
Sikuachwa mkuu tena hakuna sababu ya maana. Mama mkwe alikuwa anataka niende nae Moshi baada ya kusikia ninaenda kusalimia kwetu maandalizi ya kwenda kwetu yalikuwa tayari kabisa. Nikasema naomba niende nyumban kwanza nikirudi twemde moshi wakasema ( mama na mwanae) kama unaenda kwenu nenda moja kwa moja nikaondoka bila kugeuka nyuma.
Nimeupenda ujasiri wako...Je bado haujaolewa nije kukuwowa Mimi....
 
Yes tulikaa pamoja kujadili nikamwambia mahari usinitajie kubwa (kwa imani ya dini yetu mahari anataja binti mwenyewe) kwahiyo nikampanga fresh na akakubali, tena nakumbuka nilimwambia anitajie laki tano.
Maana nilikuwa nishatengeneza kibanda cha wakala cha tigopesa bado kununua laini tu, na kilakitu alikuwa anajua.
Na kipindi hicho nilikuwa nimepunguzwa kazini yaani sina kazi na yeye anajua kuwa kazi nimeachishwa.
Baada ya kwenda kuchukua majibu naambiwa binti anataka milioni moja, na mkaja wa baba na mama laki nne Jumla milioni moja na laki nne. Wadau mnaweza kuibeza hii pesa na kusema sio nyingi ila kwa Mazingira yake na nilivyojitoa Kwake kwamtu mwenye akili asingetaka hiyo pesa, angetaka hata nimuoe bure kwa maisha yake yalivyo magumu.
Halafu cha ajabu sijawahi kumla na msimamo wake ulikuwa hadi nimuoe ndio tukutane, na kwamsisitizo wazee wake wakaandika mpaka kwenye barua ya majibu kuwa nisimguse binti yao, wakati tayari ameshazalishwa (single mother) na baba wa mtoto amemkimbia, na kwa huruma mimi ndiye nilikuwa nimebeba majukumu ya mtoto wake kwa kumlipia ada, nauli ya shule ya kilasiku, na nikamkatia bima ya afya.
Nikaona hapa hapanifai.
Mkiambiwa muoe Bikra hamuelewa
Cc:Joka jeusi
 
Nimeshuhudia. Binti kitaa alipata mchumba kijana fulani kutoka huko Mbeya alikuwa ndio Kwanza kaajiriwa na kazi yake ilikuwa nzuri kijana alikuwa anapokea mshahara mrefu so pale mtaani story kubwa ilikuwa ni kwamba binti kaokota almasi mchangani soon life lake na la wazazi wake litabadilika.

Kijana akapeleka barua nyumbani kwa binti ili vikao na mambo mengine yaweze kuchukua nafasi! Mama yake binti akajitoa ufahamu akataja mahari milioni tano! Halafu akakomaa hataki kushusha mahari! Kijana hakuwa mbishi Sana ila shida ikaja kwa ndugu wa yule kijana kudadeki wanaona kijana wao anapigwa hivi hivi. Ndugu wakapinga, wakamwambia kijana akaze hakuna mahari kama hiyo Kwanza binti mwenyewe sio wa viwango hivyo!

Yule binti na kijana wanataka jambo lao liende ila mama wa binti kakaza na ndugu wa kijana wamekaza ikabidi ngoma isogezwe mbele ili mazungumzo zaidi yafanyike.

Kuja kushtuka yule kijana ashaoa mwanamke mwingine, ikawa aibu kwa mama wa binti na ukizingatia hakujua kumbe time yote binti yake alikuwa mjamzito! Ikabidi mimba itolewe maisha yaendelee!
 
Wazazi wengine huwa hawawazi mbali, anakomaa na milioni tank utadhani anauza bidhaa kumbe ni suala la tamaduni tu
 
Mabinti wa Kihaya mbona hawaolewi Sana Kama walivyo wachaga?
 
Wazazi wengine huwa hawawazi mbali, anakomaa na milioni tank utadhani anauza bidhaa kumbe ni suala la tamaduni tu
Tulishangaa Sana maana binti mwenyewe elimu form 4, bikira tunajua hana, maadili ya kuungaunga tu, uzuri kawaida yaani Sasa calculation za milioni 5 zilikuwa vipi?
 
Mabinti wa Kihaya mbona hawaolewi Sana Kama walivyo wachaga?
Wachaga ni opportunistic Sana .
Yaani wanauwezo wa kuona mbali Sana na kuiona future ya mtu. Akikaa na mwanaume yoyote anakuwa na uwezo wa kumsoma akili yake na mawazo yake hasa kuhusu ndoa na utafutaji wa pesa.

Makabila mengine yanataka uwe na pesa tayari
 
Sure. Kuna jirani yangu kaoa Muheza (mdigo) mwanamke yeye anataka hela tu na kazi hataki
 
Sikuachwa mkuu tena hakuna sababu ya maana. Mama mkwe alikuwa anataka niende nae Moshi baada ya kusikia ninaenda kusalimia kwetu maandalizi ya kwenda kwetu yalikuwa tayari kabisa. Nikasema naomba niende nyumban kwanza nikirudi twemde moshi wakasema ( mama na mwanae) kama unaenda kwenu nenda moja kwa moja nikaondoka bila kugeuka nyuma.
Wewe mkorofi wewe
 
Nimewahi mimi binafsi,, nilitoa mahari, na kumvalisha pete baada ya miezi mitatu alinipigia kwa jeuri na kunitusi kisa nimepeleka mbele tarehe ya harusi hapo ndipo ukawa mwisho wa uchumba wetu, mama yake alichanganyikiwa alitaka wamuombee msamaha ila mimi sikuhitaji suluhu nae tena.
Duh what a feeling😒😒!, ungemsamehe tu mkuu nadhani ilikua tu ile excitment ya harusi afu unamwambia umesogeza tar dah, ila naye alizingua hapo.
 
Kuna dem uko instagram anaitwa manka katolewa mahar ila bado anaendelea kuinesha makalii yake IG. Namhurumia sana kijana aliyevalisha pete ilo bomu
 
[emoji23][emoji23][emoji23]umejibu vizuri
Wanaume wa humu hovyo kweli ukiandika asichotaka kusikia hasa ka mwanamke anakutukana, Mara umezeeka single mother, woooi inabidi umjibu anachotaka kusikia Ili apate amani ana apunguze stress za vyuma
 
Back
Top Bottom