Kutana na Luludiva; superstar anayeishi nyumba ya tope

Mwache kwanza dada wa watu atulie, kupoteza mzazi sio masihara mkuu.
Vipi na wewe hujajenga kwenu? [emoji13][emoji13]... Nadhani hapa mnatakiwa mjifunze kwamba Mola akiwapa kidogo kwenye maisha punguzeni majigambo, kujionesha kuwa mna mapesa na maisha ya juu. Sote kama binadamu kwa nyakati tofauti huwa tunapitia hizi changamoto za kuuguza wapendwa wetu, tena kwa muda mrefu, yote ni mipango ya Mungu. Lakini ukiwa kila dakika ni kuwaonyesha walimwengu kwamba wewe ni milionea na maisha umeyapatia basi jiandae kurushiwa mawe siku moja maana si wote huwa wanafurahia mafanikio ya wengine. Mwisho hiyo nyumba ya udongo wala siyo lazima kabisa kuivunja na kujenga mpya ya tofali kama hujajipanga. Hiyo hiyo ya udongo inapigwa plasta, floor, rangi, boresha madirisha inakuwa Safi kabisa, yaani hata milioni 10 haziishi, tena waweza karabati kidogo kidogo tuu, leo milioni mbili unatulia, kesho tena milioni tatu unatulia mwisho unamaliza huku maisha ya mjini yanaendelea. Tukumbuke sote, hasa wale ambao bado wanaamini kurudi makwao kuzikwa wao au ndugu zao, ni muhimu sana kuandaa sehemu ya kufikia.
 
Mimi sioni cha ajabu hapo. Lulu Diva ni mpambanaji tu kama walivyo watu wengi nchi hii.

Alianza kuigiza, mambo yakagoma, akawa video vixen na sasa hivi anakomaa na kuimba.

Sasa sioni popote kama kuna sababu ya kushangaa.
Kuigiza kuligoma vip mkuu? Mbona hata jana nimemuona huku DStv kwenye (Huba, Jua kali sijui) akitakia watu Christmas njema
 
Ila na wewe mleta uzi kwanini unafuatilia maisha yasiyokuwa yako? Wazungu hawajengi nyumba wengi wao wanaishi kwenye nyumba za mbao na wamepangishwa napenda maisha halisi ya kijijini
Tatizo hamtaki kusikia ukweli, mnasingizia eti unafuatilia maisha ya watu [emoji12][emoji12]
 
Hivi sasa anaigiza mkuu..
Tena in muigizaji mzuri anajitahidi
Ukitaka kumuona angalia tamthilia inaitwa jua Kali..anaigiza sambamba na Gara B
Yes, anaigiza vizuri sana, anajua kuuvaa uhalisia, kaitendea haki nafasi ya receptionist kwenye Jua Kali
 
Tatizo hamtaki kusikia ukweli, mnasingizia eti unafuatilia maisha ya watu [emoji12][emoji12]
Kwani nyumba ya kuishi haipo? Au wewe unataka jumba kubwa kama tembo, mtu mwenyewe anaishi Dar ajenge huko na Dar nani amjengee?
 
Mara nyingi vijijini kwetu huwa ni sehemu ya ukoo, hivyo ni ngumu sana kujenga wakati unajua fika pataleta shida. Tunajenga ikiwa tu una pesa za kutosha
Acha kudanganya watu, wazazi wako hawakuwa na mji wao huko kijijini?? Ukoo ni muunganiko wa familia mbalimbali.
 
[emoji1666][emoji1666][emoji106][emoji106]
 
nani huku anaweza jenga kwa wajomba. Au hapo ni kwa mume wa mamake
Mimi kwao na baba yangu kwavile Ni marehemu siwezi kutumia nguvu zangu kujenga sembuse ujombani,, humu wengi watoto ama la wamebahatika kuzaliwa ktika familia zisizo na mkanganyiko na migogoro,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…