Kutana na Luludiva; superstar anayeishi nyumba ya tope

Kutana na Luludiva; superstar anayeishi nyumba ya tope

Mimi Nikitoboa Kwenye Maisha, Wazazi Wangu hawataishi Kijijini…..!!!

Na ile Nyumba Ya Kijijini Itabaki kuwa Sehemu ya Makumbusho ya Hustles walizopitia wazazi wangu na Mimi nikazishuhudia.

Ila Tamaduni za kwetu, Kuzikwa ni Kijijini uliko zaliwa…..

Hiyo Nyumba Ya Lulu Mbona Nzuri Sanaa….

Ila Ni Tanzania Pekee ambako, Unagharamia matibabu Kwa zaidi ya Tsh Millioni 100 ya mzazi wako, Halafu wanakucheka kwa kutokuwa na Nyumba. Uchaguzi wa ni Maisha Gani Tunayataka Watanzania Bado Unatusumbua Sanaa..
 
Sio kwa mastaa wabongo bro we ukiona interviews zao utachoka yani mtu anahojiwa kuhusu gharama za Nguo na nywele anavyojikuta sasa utasema tajir sihuyu hapa eti hapa juu mpaka chini nimevaa million 10 mwisho wa siku kodi zinawashinda kulipa Kwenye nyumba zao zakupanga wanaishi maisha ya stress sana,,,
Ujinga mzigo
 
.
Screenshot_2021-12-24-11-25-55-37.jpg
 
Enjoy life is too short,yaani nishindwe kula /kunywa vizuri kisa nyumba?huo ushauri kawapelekee ndugu zako, wanaokuhusu ,
Maisha ya wengine waachie wanyewe, kwa sababu hawajawani kukufuata kukuomba chochote
 
Hivi huyu Lulu Diva ni superstar wa kitu gani?
Actress, musician au ni mchekeshaji?
Kwa hakika sijui mnijuze
Nakubaliana na wewe...yaani Mayele ananulikana na wengi kuliko huyo sijui Luludiva...hata Boco ni maarufu zaidi ya huyo
 
Sa afadhali hata yeye ana kwao, tena na Nyumba ya Tope ipo.. kuna wengine Tunamponda huku tumezaliwa kwenye Nyumba za Upangaji na mpaka leo tuko Kwenye Nyumba za Upangaji.. infact hatuna kwetu!!
Dah 🤣🤣🤣
 
Usiwaamini sana hawa bongo movie hapo either yupo location anajiandaa kutoa movie mpya.
 
Mara nyingi vijijini kwetu huwa ni sehemu ya ukoo, hivyo ni ngumu sana kujenga wakati unajua fika pataleta shida. Tunajenga ikiwa tu una pesa za kutosha

Kwanza alipozikwa mama yake inasemekana ni ujombani yaani ni alipozaliwa mama yake, yeye lulu alikua anaishi na mama yake mjini ikiwa ni pamoja na kumuuguza, sasa jiulize angeenda kujenga kwa wajomba zake kweli?, Hata ivyo maisha ya watu tuwaachie jamani lulu mwenyewe ameanza mziki miaka ya juzijuzi tu, ata mziki wake unaonekana bado haujampa mafanikio makubwa. Watu wanajua kujudge maisha ya wengine!! Ikumbukwe kuwa historia zetu hazifanani jamani, Lulu amepambana sana kumuuguza mama yake aliyekua amelala chini, sio rahisi kumuuguza aliyelala chini kwa kipindi kirefu ni gharama mno, ikizingatiwa yeye ndoye mtoto wa pekee kwao na baba yake alishatangulia mbele ya haki.

Mungu ampe faraja kuu[emoji24]
Pumizka kwa Amani mama Lulu.
 
Back
Top Bottom