Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kuna mahali nilisoma kwamba unapoendesha gari yenye umri zaidi ya miaka 15 kwenda safari ya mbali, umri wa hiyo gari unaweza kuchangia wewe kupata ajali. Yaani, kadiri gari ilivyo ya umri mkubwa ndivyo ambavyo ina uwezekano mkubwa wa kupata hitilafu na kusababisha ajali hata vifo.
Tanzania ni mojawapo ya nchi duniani utashangaa kuna malori na mabasi yenye umri wa miaka zaidi ya 30, lakini bado yanatumika barabarani. Imefika wakati ambapo serikali kupitia LATRA iweke sheria kwamba kwa mabasi, gari yeyote yenye umri zaidi ya miaka 10 haipaswi kutumika tena kubeba abiria. Kwa malori, gari yeyote yenye umri zaidi ya miaka 20 lisiruhusiwe tena kutembea barabarani
Tukifanya hivi tutaepusha ajali nyingi zisizopaswa kutokea. Haya malori na mabasi yanayofeli breki kila wakati mara nyingi ni machakavu ya zamani ambayo mifumo yake imeanza kufeli, na wamiliki wanaunga unga tu ili kuyaweka barabarani. Yatolewe barabarani na kuuzwa kama vyuma chakavu.
Kuna nchi duniani gari yenye umri zaidi ya miaka 10 hairuhusiwi kutembea barabarani, na katika nchi hizo hutasikia hata siku moja ajali eti lori lilifeli breki na kuua watu
Na ikiwezekana, hizi basi za China za Yutong na Zetong sijui, zisiruhusiwe kuwa barabarani kwa safari za mikoani kama zina umri wa zaidi ya miaka mitano