Kutatua tatizo la ajali nchini kutokana na uharibifu au kufeli breki, LATRA waweke kikomo cha umri wa mabasi na malori kuruhusiwa kuwa barabarani

Kutatua tatizo la ajali nchini kutokana na uharibifu au kufeli breki, LATRA waweke kikomo cha umri wa mabasi na malori kuruhusiwa kuwa barabarani

Lini magari yalofika kwetu ushawahi kusikia recall ndugu, fuatilia ajali kibao za mabasi na semi utakuta nyingi bado mpya
zinakuwapo, ikiwa utakuwa umenunua gari jipya kupitia ma ajenti wa Tanzania kama Toyota, Benz, nk
 
Kwenye maroli na mabasi kiwekwe kigezo cha lazima yaje na mifumo ya usalama kama Hydraulic Retarder, Hill climbing assistance, ABS, Lane departure assistance, trailer anti rolling system.

Kwenye basi za kichina wanaleta zikiwa na Eddy Current Electric Retarder ambayo ufanisi si mkubwa na ikipita sehemu zenye maji magnetic field hazifanyi kazi. Hapo dereva anategemea Foot brake tu. Kwenye roli wanatumia engine stopper wakati sasa technology ni Hydraulic Retarder ndio ina ufanisi mkubwa.

Basi na roli zote za China haziji na Hill climbing assistance na lane departure warning system. Ikiwekwa sheria ya lazima gari iwe na hizi features lazima muagizaji aweke option kwa mtengenezaji, hizo trucks na Bus za China kwenye Europe market wanapeleka na safety features hizo
Mmmh, Mkuu umemamliza. Una ufahamu ningependa nijifunze kwako!
 
Mmmh, Mkuu umemamliza. Una ufahamu ningependa nijifunze kwako!
Karibu sana mkuu, kwenye basi za abiria ndio tumejisahau tuna zipa madaraja kulingana na seat arrangements,viburudisho na choo baada ya safety na technical features sio priority. Mchina unaponunua gari hizo safety features ni option sio standard.

Mfano basi za mwendokasi ni China product lakini zimekuja na mfumo wa hydraulic retarder ambazo ni mfumo salama kwenye brake. Hizi basi za kawaida zina eddy current electric retarder na madereva wengi kwenye hali ya mvua brake za basi huwa zinafail na kusababisha ajali.
 
Kuna mahali nilisoma kwamba unapoendesha gari yenye umri zaidi ya miaka 15 kwenda safari ya mbali, umri wa hiyo gari unaweza kuchangia wewe kupata ajali. Yaani, kadiri gari ilivyo ya umri mkubwa ndivyo ambavyo ina uwezekano mkubwa wa kupata hitilafu na kusababisha ajali hata vifo.

Tanzania ni mojawapo ya nchi duniani utashangaa kuna malori na mabasi yenye umri wa miaka zaidi ya 30, lakini bado yanatumika barabarani. Imefika wakati ambapo serikali kupitia LATRA iweke sheria kwamba kwa mabasi, gari yeyote yenye umri zaidi ya miaka 10 haipaswi kutumika tena kubeba abiria. Kwa malori, gari yeyote yenye umri zaidi ya miaka 20 lisiruhusiwe tena kutembea barabarani

Tukifanya hivi tutaepusha ajali nyingi zisizopaswa kutokea. Haya malori na mabasi yanayofeli breki kila wakati mara nyingi ni machakavu ya zamani ambayo mifumo yake imeanza kufeli, na wamiliki wanaunga unga tu ili kuyaweka barabarani. Yatolewe barabarani na kuuzwa kama vyuma chakavu.

Kuna nchi duniani gari yenye umri zaidi ya miaka 10 hairuhusiwi kutembea barabarani, na katika nchi hizo hutasikia hata siku moja ajali eti lori lilifeli breki na kuua watu

Na ikiwezekana, hizi basi za China za Yutong na Zetong sijui, zisiruhusiwe kuwa barabarani kwa safari za mikoani kama zina umri wa zaidi ya miaka mitano
Mkuu unapendekeza Tu lakini hujui uhalisia wa maisha ya watanzania walio wengi .mkuu naendesha gari ina miaka kabla sijazaliwa yaani hata mimi nimeikuta mimi na miaka 34
 
Nitaomba Moderators warekebishe kwenye title
Toka 2019 huelewi kinachoendelea kuhusu Sumatra? Huna uhalali wa kuandika mada humu maana hata kusoma, kusafiri wala kusikiliza vyombo vya habari miaka 6 hujihusishi.
 
Karibu sana mkuu, kwenye basi za abiria ndio tumejisahau tuna zipa madaraja kulingana na seat arrangements,viburudisho na choo baada ya safety na technical features sio priority. Mchina unaponunua gari hizo safety features ni option sio standard.

Mfano basi za mwendokasi ni China product lakini zimekuja na mfumo wa hydraulic retarder ambazo ni mfumo salama kwenye brake. Hizi basi za kawaida zina eddy current electric retarder na madereva wengi kwenye hali ya mvua brake za basi huwa zinafail na kusababisha ajali.
Hivi kuna watu pale TBS wanaelewa haya mambo lakini?
 
Toka 2019 huelewi kinachoendelea kuhusu Sumatra? Huna uhalali wa kuandika mada humu maana hata kusoma, kusafiri wala kusikiliza vyombo vya habari miaka 6 hujihusishi.
Nina uhakika katika kipindi hicho nimesoma mambo mengi sana kukuzidi. Ila sijasoma habari za SUMATRA kuwa LATRA kwa kuwa niko selectie katika kusoma.

Ni sawa na wewe unamwambia Professor wa macho Muhimbili kwa nini huelewi kwamba siku hizi kuna tiba mbadala ya upele wakati imeandikwa sana magazetini. Anaweza asijue
 
Back
Top Bottom