Kutembea na mfanyakazi wa ndani (house maid) hakuna tofauti na mwalimu kulala na mwanafunzi ni kujizalilisha kabla ya kuzalilika

Kutembea na mfanyakazi wa ndani (house maid) hakuna tofauti na mwalimu kulala na mwanafunzi ni kujizalilisha kabla ya kuzalilika

Ndugu zangu nawasihi simameni kama wazazi!
Unapopoewa dhamana ya kumlinda mtoto wa mtu hakikisha unatimiza majukumu hata kama kuna udhaifu wowote!

Mimi enzi nafundisha shule ya kujitolea enzi hizo nimemaliza chuo!
Kuna kabinti kalinitamkia waziwazi Ikanahitaji penzi langu! Lakini nilikumbuka maneno ya mzazi wangu kwamba unapopatiwa majukumu simama kama mzazi hata kama kuna udhaifu!

Yule binti nilimsihi atulie asome kwanza mambo hayo yapo tu, nikamsihi awe na aman na nilipongeza kwa ujasiri wa kueleza hisia zake! Nikamwambia sasa kasome kwa bidii ngono haiui na wala haishishi (haitoshekeki)

Binti alielewa kwa vile niliongea naye kwa hekima kama mzazi alinielewa vizuri!

Sasa kizazi cha Leo imekuwa kawaida!
1. Mwenye nyumba kutembea na mfanyakazi house boy/girl
2. Imekuwa kawaida mwalimu kugeuza vimada wanafunzi
3. Huko mtwara kuna DC anatuhuma za kutembea na mwanafunzi

Haya ni mambo ya ajabu sana kwasababu!
1. Ukisimama kama mzazi hata binti wa kazi akikaa uchi utamkumbusha kuvaa
2. Ukisimama kama mzazi hata ukitegwa kimalaya unaelekeza kama mzazi

Binti wa kazi hata akikufunika shuka chumbani mkeo akiwa hayupo ukisimama kama mzazi huwezi katu katu kumgeuza mkeo!

Hata kama mkeo hakutimizii mwanaume anaejielewa huenda kuchepuka huko na wanawake ...kuliko kutembea na binti wa kazi au mwalimu kulala na wanafunzi!

Simameni kama wazazi jamani
Inategemea
 
Back
Top Bottom