Kutoana kafara kwenye familia, na Siri ya wazazi wetu

Dawa ya kuzuia chuma ulete shambani ni ipi?
 
Sehemu ya Tisa.

Mapenzi yanauma,
Mapenzi yanauma acheni.

Hii sehemu ukitumia hisia bila akili unaweza kujikuta unapotea,unapoteza au ukapotezwa.

Sasa endelea...............................

Moses alivurugwa,aliongea peke yake,alihisi kuna namna imetumika hakutaka kuamini kama mambo yale yaliyomtokea ilikuwa ni kawaida,aliuona mkono wa mtu,aliona kabisa kuna mtu kashikilia remote,anamuongoza anaamua ni lini awe na furaha,ni muda gani apitie magumu.

Moses kijana mtanashati,kijana mwenye haiba na muonekano wa kiume,mcheshi ,mwelewa ,lakini mtafutaji na msaka noti kutoka kanda ya ziwa,mtu smart kichwani.

Wapo wanaosema watoto wanaopatikana pindi wazazi wakiwa na umri mkubwa huwa wapo smart kichwani, japo sina hakika Kwa hili.

Moses hakuwa mtumishi wa pombe na sikuzote hakuamini katika pombe,hakuwahi kuijua ladha ya pombe na hakutaka kuijua.

Baada ya kusafisha mabaki ya vioo vilivyokuwa pale chini alifunga mlango na kutoka kwenda kutafuta chakula mtaani,
Huku akijilazimisha kama mgonjwa ili Tu tumbo liwe na chochote kitu kisha akarudi ndani kwake na kujilaza huku akibaini ni mida imeenda sana,aliwaza vitu vingi,hata simu yake iliyozimika Kwa kuishiwa chaji hakujua, aliwaza mbali mno.

Kila akiangalia picha iliyo kwenye fremu akiwa kwenye suti nzuri ya kupendeza huku mkewe kipenzi akiwa pembeni yake alijikuta anacheka peke yake huku akishindwa kupata definition kamili kuhusu ndoa.

Ndoa ni nini?

Nini waligundua watu wa kale na kuruhusu kitu kinaitwa ndoa?

Ndoa ina faida gani?

Mbona kama kuna namna wanaume tulizungukwa ?

Yaani umchukue mtu asiye ndugu yako uishi naye,mtu hujui historia yake ,halafu anakutesa na kukuumiza Kwa kiasi hiki?

Moses alijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu.

Ndoa ina faida lukuki Kwa mwanaume lakini Moses hakuziona masikini.
Na Kwa hali aliyokuwa nayo asingeziona hata mara moja.

Alipata usingizi saa ngapi haikujulikana, hatimaye ilikuwa ni siku nyingine mpya , Moses aliamka na kuanza kuzunguka nyumba yake ,haikuwa nzuri kivile,haikuwa ya gharama kihivyo.

Ila ilitosha kutambulisha juhudi za kijana mpambanaji,ilikuwa nyumba nzuri pale kijijini ni mfano wa kuigwa na iliwapa wivu baadhi ya vijana wenye kudhani Moses hakustahili kupata ile nyumba.

Wakati akizunguka Moses alipata wageni muda ule,wageni wawili anaowajuq Vema lakini ilimshangaza wale watu kuna muda ule asubuhi na mapema,

Alikuwa ni kijana mshirika mwenzie kwenye biashara,lakini pia alikuwa na Mzee wake yaani Baba yake mzazi.

Walisalimiana huku Moses akigundua Baba yake ni mwenye huzuni hayupo kama alivyomzoea.Moses alijichangamsha huku akificha machungu yake.

Pole sana mwanangu, pole nayajua unayopitia, Mimi ni Baba yako hupaswi kunificha chochote,najua hapa mkeo hayupo nina uhakika,lakini mwanangu unaamua kunificha Mimi baba yako? aliuliza Baba yake na Moses.

Baba,Mimi sijakuficha kwasababu Kwa mara ya Kwanza nilikwambia,ila kwasasa sikutaka kumsumbua yeyote,huu si ugonjwa wala si msiba ni Jambo ambalo naweza kupambana nalo mwenyewe,ikiwa itashindikana nitawaambia tu wala sitawaficha.alijibu kiufupi Moses.

Oyaa kaka,tusamehe Sisi tusamehe Sana muda wote hauji kazini,haupo karibu na Sisi tulidhani umeamua kututenga labda kwasababu Una pesa nyingi kwenye mzunguko wa biashara yetu,tulijua ni Gia ya kutaka kuhustle kivyako,ila kumbe Una majanga,pole bro,pole sana,na nikuahidi kitu kimoja biashara zinaenda,tena zipo vizuri wote tunaamini wewe ni Movie sterling kwenye biashara yetu,hivyo kila kitu kitaenda sawa.ila Mimi nikushauri tu mwanangu,tutafute pesa tu ,Shemeji atarudi tu ,niamini Mimi Shemeji yangu zawadi anarudi ila utampa kichwa ikiwa utaonesha hujiwezi kwake waziwazi.aliweka kituo yule jamaa.

Mzee wangu ,na jamaa yangu niwambie ukweli Mimi nipo sawa ,labda niwaoneshe uharibifu aliofanya mke wangu ikiwa ni njia ya kunikomesha baada ya kukosana naye,hakika amenitia hasara mno (huku wakiinuka akiwatembeza na kuwaonesha baadhi ya vitu vilivyoharibiwa na mkewe Zawadi.

Mmmh mwanangu,unajua unaishi na mwanamke mwenye roho mbaya sana,
Kwanini mgombane halafu avunje vitu,hofu yangu asije akakudhuru siku moja,mwanangu najua unampenda mwenzio lakini...............Baba yake Moses alishindwa kumalizia sentensi yake.

Baba najua,
Najua unamaanisha nini mke wangu kafanya jambo baya sana,nikipiga hesabu inazidi milioni tatu Kwa vitu alivyoharibu,lakini pia nyaraka za biashara nyingi kaharibu.aliongeza Moses.

Unaona,ipo siku mtagombana kisha atakuvizia usiku mmelala akuchome kisu,Kwa namna alivyofanya hivi halimshindi Jambo lolote.alizidi kukazia Baba yake Moses.

Moses alishtuka huku wakiangaliana na Baba yake Kwa muda.

Weeeee Acha Mzee, mke wangu hawezi nichoma kisu na akifanya hivyo nitamuua,
Nitamuua nakwambia Baba,mtaniona sifai.aling'ata midomo Kwa hasira Moses.

Mwananguuuu Acha kuhamaki,
Hivi Kwa mfano mmegombana halafu mkayamaliza Kwa kuondoa utata, halafu wewe ukajua mambo yameisha,halafu ukalala usingizi,halafu akachemsha maji na kukumwagia hajakuumiza bado mwanangu?

Au tu akachukua kitu kizito na kukupiga nacho kichwani hatujakuzika Moses?
aliongea Baba yake Moses kwa uchungu

au akaamua kukufungia ndani na kuchoma nyumba ?huoni itakuwa shida?
bro hebu mwelewe mshua ana maana gani usichukulie poa ohoooo.aliongeza jamaa yake Moses.

Mbona mnanitisha,
Ila sijawapinga yote yanawezekana niamini kabisa


Mazungumzo Yao yaliisha huku wakimshauri Moses aachane na zawadi lakini pia ni kuhusu msala wa Moses akituhumiwa kufanya biashara haramu.

Ujue Moses Una Jambo kubwa Sana umezushiwa ,watu wote tunajua wazi huna tabia hizo lakini wewe unalipuuza ,Mimi nililetewa barua pale ofisini nikampa mwanamke fulani ni jirani yenu, nikamwambia akuletee,lakini wewe kwenye simu hupatikani vilevile .alilaumu jamaa yake Moses.


Baada muda fulani wale watu waliondoka huku wakimsihi moses awe makini na mwanamke wake.

****************

Moses alishinda pale nyumbani kwake huku akipigapiga simu huku na huko ikiwa ni njia ya kujisahaulisha matatizo yake.

Lakini weee Acha Moses alijikuta anapiga simu Kwa mkewe ,simu akiiweka sikioni kisha ikapokelewa.

Habari za leo mume wangu,mzima.zawadi alisalimia huku Moses akiushangaa upole wa mkewe.

Mimi mzima mke wangu,ni mzima kabisa.aliropoka Moses.

Moses mume wangu, nakupenda sana lakini Jana ulinifanyia ukatili mkubwa mnounanipiga huku ukijua Hali yangu ilivyo?alilaumu zawadi .

Lakini uliharibu vitu humu ndani ?
aliongea Kwa upole Moses.

Ndiyo nililipiza ikiwa ni Sehemu ya kuufariji moyo kwa uliyonifanyia . alijibu Zawadi Kwa kujiamini kabisa kisha akakata simu.

Masikini Moses alijikuta akifurahi yaani alisahau yote aliyoambiwa na Baba yake,alikuwa tayari tusamehe kila kitu ila tu awe na mkewe Zawadi.

alijikuta njaa inauma kwakuwa presha na Mawazo vilishuka .alipata walau moja ya kumi ya furaha .mtego aliotegwa hakujua, Zawadi alijua anapendwa,alijua Moses hajiwezi kwake, Lakini hata hivyo, Zawadi alimpenda Moses Kwa dhati ,na upendo huu aliubaini kila anapokuwa mbali na Moses.

Je ni Nani anawachezea vijana wadogo kiasi cha kuiweka ndoa yao mashakani?

Endelea kufuatilia sehemu ijayo ina majibu.

Loading.........,.............
 
Ila wee jamaa miyeyusho Sana.

Lete stori maliza watu wasome habari nyingine.

Unaleta mambo ya Facebook Sasa.
 
Kafara Iko wapi Sasa!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…