Pre GE2025 Kutofautiana kauli na mtizamo wa Katibu Mkuu na Mwenezi CCM kunaashiria nini kuelekea Uchaguzi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
1.Mwenezi hajapata somo la "Leadership"
2.Njia alizopita hadi kufikia hapo alipo zinampa kiburi,kutokuwa na utii kwa viongozi wa juu yake!
3.Katibu Mkuu yupo sahihi.
4.Siku za nyuma vijana waliandaliwa kwa ajili ya propaganda mtandaoni,sasa ndio wanaotumika kusifia kila afanyalo mwenezi hata pale anapokuwa yupo njia ya utaratibu!
 
Zero Brain yeye anaendeleza yale ya awamu iliyopita ya Baba yake!
 
Mamlaka ya kuagiza waziri wa Tamisemi kumfuata KAZI mkurugenzi wa Pangani yameainishwa kifungu kipi katika KATIBA ya chama Cha MAPINDUZI CCM?
Tangia lini umesikia kuwa waziri anamfukuza kazi mkurugenzi? Kazi ya waziri ni kumsimamisha kazi ,kuunda tume ya kiuchunguzi na kutoa ushauri kwa mamlaka ya uteuzi ambaye ni Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan.

Chama cha Mapinduzi ndicho kilichounda serikali.ndicho kilicho hadi ilani yake ambayo ndio kama mkataba na watanzania kwa miaka mitano.huo mkataba ukapewa serikali ili kuutekeleza kama ulivyo kwa kuzingatia muda husika.kwa hiyo chama kina haki asilimia zote za kutaka kujuwa namna mkataba unavyotekelezwa,aina ya huduma wanazopewa wananchi,kasi ya kupeleka huduma na ufanisi wake. Lakini pia kufuatilia na kujuwa wale wanaokwamisha utekelezaji wa mkataba wake na wananchi. Na ikibainika mahali popote pale kuna mtu anakwamisha utekelezaji wa mkataba wake na wananchi ni lazima itoe maagizo kwa serikali yake kutaka kupata majibu na kutia maagizo ya nani na nani awekwe pembeni kwa maslahi ya chama.kumbuka anayeenda kuomba kura kwa wananchi ni chama na siyo serikali.
 
Wananchi wanamlipa mshahara Mwenezi wa chama?
 
Nisaidie kuyajua mamlaka ya Katibu Mwenezi wa CCM yaliyoainishwa na Katiba ya chama.
 
Mheshimiwa Makonda ni mtetezi wa wanyonge.ni sauti ya wanyonge.ni Kiongozi anayezungumza yake yaliyo katika vifua na mioyo ya watanzania.ndio maana unaona namna watu wanavyofurika na kumiminika katika mikutano yake ili kupeleka kero zao .
Wanyonge Gani walipinga kura kumchagua Mwenezi wa chama Cha MAPINDUZI?
 
Ndio wanamlipa kupitia chama chake.maana chama chochote chenye wabunge bungeni kinapata Ruzuku ambapo hiyo Ruzuku ni kodi za watanzania.
Kwahiyo John Mrema, Mwenezi wa CDM anaweza Kutoa maelekezo Kwa waziri wa Tamisemi ikiwa chama chake kitapewa ridhaa kuongoza?
 
KM ni mkubwa Kwa Mwenezi hivyo warudi vikaoni na Kutoka na mwelekeo wa pamoja.

Mbali na hapo, ni kuharibiana tu.
 
Kwahiyo John Mrema, Mwenezi wa CDM anaweza Kutoa maelekezo Kwa waziri wa Tamisemi ikiwa chama chake kitapewa ridhaa kuongoza?
CHADEMA haina hiyo nafasi wala haijikupata hiyo nafasi na wala hatuwezi kujadili hilo suala maana Ni CCM Pekee iliyo na uwezo wa kuiongoza Tanzania
 
Ndo nasemaje,

Ikiwa uelekeo wa Mwenezi uko sahihi, kwanini wasikae kikao na kupitisha uelekeo huo uwe wa chama kizima?
Hawawezi.
Siku malalamiko yakiwa mengi kwenye staili mojawapo kati ya hizo. Wanampiga chini muhusika na kusema yule Mwingine aliebaki ndio msimamo wa chama.

Ni kama wametegeshea kote kote.
 
Ongea Polepole,

Maana unaowasema vibaya ni viongozi wako!!!🙄
 
Mheshimiwa Makonda ni mtetezi wa wanyonge.ni sauti ya wanyonge.ni Kiongozi anayezungumza yake yaliyo katika vifua na mioyo ya watanzania.ndio maana unaona namna watu wanavyofurika na kumiminika katika mikutano yake ili kupeleka kero zao .
Ikiwa Mwenezi ni mtetezi wa unaowaita wanyonge,

KM ni mtetezi wa akina nani?

Pia nani mkubwa wa mwenzie?

Na kwann hawaongozani?

Karibu🙏
 
Siasa za DAB ndizo wanazozihitaji wanyonge.

Nchimbi ni moja ya viongozi wenye falsafa za CCM ILIYOCHOKWA.
 
Sasa Yaani Mkurugenzi kasimamishwa kazu kisa makonda huku tunakoelekea DUH
Ila hii Sio haki hata kidogo..
Mwene ZIIII leo kawa Mwenyezi Dah sasa mkurugenz kakosea Wapi?
Rabbon
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…