Kutoka AI: Freeman Mbowe ulichokifanya leo hakiakisi utu, mshikamano wala hekima

Mimi acha nishangae tu na haya maoni kuhusu Mbowe ambayo bado kuna watu ndani ya CHADEMA wanafikiri Mbowe bado anayo matumaini ndani ya chama hicho.

Hivi kweli ilihitaji kumwona Mbowe leo kwenye hafla hiyo ndipo watu wajue alipo Mbowe?

Yooote yaliyoonekana wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi hayakutosha kabisa kuwapa ufahamu juu ya dhamira ya Mbowe na hicho chama alichokiongoza na kutaka kukikabidhi kwa Samia?

Hamkujifunza chochote huko, hadi leo mje hapa kumzungumzia Mbowe katika maswala ya CHADEMA?

Manataka awaambie vipi kuhusu msimamo wake zaidi ya yote aliyokwishayaonyesha waziwazi muelewe!
 
 
Hakuna mradi wowote wenye maana ikiwa Wananchi wanatekwa na kuuawa huku maelfu wakibambikwa kesi za uongo za Uhaini na ugaidi
 
Mimi nadhani sio Mbowe tu ata makamanda ambao bado tunalipa kodi kwa serikali ya CCM,kutumia vitu kama bara bara,maji,umeme,hospitali zilizojengwa na serikali sio sahihi.Hii ni kua tunaunga mkono kinachoendelea.
MWISHO,TUMUOMBEE LISSU ili liishe maana tumefika mbali. MUNGU NI MWEMA SIKU ZOTE
 
Jamaa anachuki sana tangu apigwe chini.
 
Hakuna mradi wowote wenye maana ikiwa Wananchi wanatekwa na kuuawa huku maelfu wakibambikwa kesi za uongo za Uhaini na ugaidi
"Mradi"?

Hivi kuna mradi wowote ulioanzishwa na kutekelezwa na Samia hadi sasa?

Nakumbuka Bandari Benki ya dunia ilitoa mkopo kabla ya Samia, yeye alichofanya ni kuigawa bandari wanufaike wajomba zake DPW.

Kuna mradi upi wa Samia hadi sasa, Gesi ya Ntorya Mtwara aliyowagawia Oman? Umefikia wapi hadi sasa, maana hatusikii chochote juu ya mradi huo.
 
Mwaka 2005 nlimpigia kura ya kuwa Rais....

Mwenyezi Mungu anisamehe sana kwa kuwa sikujua nilikuwa nafanya nini kwa muda ule.....
Lissu kuwa Mwenyekiti nimetambua makosa yangu...nlimuamin mtu asieaminika
 
Nimeona post hadi Msigwa leo eti anamsifia Mbowe!

Hakika paka ametoka kwenye gunia lilikua ni suala la muda tu.

Ninakumbuka Lissu alipohojiwa na Sammy Awami wa BBC kabla ya uchaguzi mkuu wa CHADEMA alisema.

"Sina tatizo na mwenyekiti ila mwenyekiti amebadilika sana tangu alipotoka gerezani"..

Ni wazi gerezani huko Mbowe aliingia makubaliano tusiyoyajua hata makamu wake akawa hajui , na haikushangaza mtu aliyeitwa gaidi jioni akaibuka ikulu ametinga suti kabisa na kuonekana mwenye furaha kubwa.

Leo hii nauliza tena Msigwa ni wa kumsifia Mbowe waliyemtaja kama gaidi?

 
Mnamletea dharau wakati nyie wa kuja tu ,mnatoka porini halafu mwenzenu wa mjini. .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…