Katibu mkuu wa CCM alishasema mswada huu haupaswi kuondolewa hata nukta
Spika ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM , kazi iliyokuwepo ni kuhakikisha unapita. Limetokea
Hadithi za kukuza demokrasia ni za kitoto sana. Hivi kweli kuna mtu anaamini CCM na haya ya ununuzi, CCM na marufuku ya mikutano ya siasa hata Bunge, CCM na hizi kamata kamata ina nia ya demokrasia kweli!!
Mwalimu Nyerere anabaki kuwa kiongozi mwenye maono sana hata kwa wanaotofautiana naye
Mwalimu alisema,Rais wa Romania alidhani wanaompinga ni wachache, mwisho wakawa wengi na kumuondoa
Rais Mwinyi wakati wa white paper alisema ' Wengi wapewe, wachache wasikilizwe'
Usikivu wa hoja za wachache ndio uliozaa mafumo wa vyama vingi na kutupa utulivu wa miaka zaidi ya 25
Mswada huu wna taasisi na makundi ya kijamii. Kudhani kuwa ''Ndiyoo' ya wabunge wa CCM ni kitu muhimu ni kutoiangalia historia. Wabunge wa CCM wameupa mswada uhalali wa kuhalilisha kinachopingwa
Kuna mtu anaitwa Nalaila Kiula, alikuwa Mbunge wa CCM. Wakawepo akina EL na Sumaye achilia mbali akina Kingunge na Laurence. Orodha ni ndefu,inatosha kusema anayeonekana vyema ni Nape Nnauye
Huyu bwana alikuwa katibu mwenezi akihangaikia chama na hata kuvunja mifupa.
Akiwa Mbunge alipewa uwaziri alioutumia kuleta sheria nyingi na marufuku zisizo za kisheria kama Bunge live
Nape akaaminisha umma lengo ni kuokoa gharama za uendeshaji na kukuza 'demokrasia''
Upigaji debe wake haukusikiliza sauti za wachache kwasababu alikuwa karibu na keki.
Ilichukua asubuhi moja tu akapoteza nafasi yake na mchana wa siku hiyo akakutana ana kwa ana na 'bastola' ikisotwa kwake
Leo ni mmoja wa watu 'wasio na thamani ndani ya chama' licha ya utiifu wake uliopitiliza na kuwa mahaba
Hawa CCM walioko ndani ya Bunge wanachofanya ni kulinda kuteuliwa ili wawe Wabunge tena
Wanaamini bila kufanya hivyo hawatapa 'msaada' wa kisiasa
Wasichokumbuka ni kuwa sheria ikiwa kitabuni inalala, siku ikifika sheria hiyo inaamka na hasira kali
Hii ni Tanzania yetu sote, kuna vizazi vijavyo ! Swali, tunajenga nchi ya namna gani na kwa ajili ya nani?
Hawa wabunge wa CCM wanajua utata wa mswada kwa masilahi yao ya muda mfupi na madhara ya muda mrefu . Nimekumbuka ule msemo '' you can't eat your cake, and have it too''
JokaKuu Pascal Mayalla Mlenge