Na, Mwl, Osunga Pasaka Jr.
ZITTO KABWE ULITAKA HITLER AFANYEJE??
Nimepitia mitandao ya kijamii nikaona tweet ya huyu kijana akidai haya yalifanywa na Hitler?
Hivi kweli unamjua Hitler?
Mara baada ya vita vya kwanza vya dunia 1914-1918, Hitler pamoja na rafiki yake Austria walishindwa vibaya, hali iliyosababishwa na usaliti wa rafiki yao wa karibu Italy aliyeamua kuondoka kwenye vita kwa zawadi nono aliyoahidiwa.
Baada ya vita hivyo kilifuatia kikao cha amani pale Versaille, mji uliojirani na Paris Ufaransa.
Katika kikao hicho kilichokuwa cha upande mmoja (Tripple entete) kilichoshutumu ujeruman kama waanzilishi wa vita kiliweza kuja na maazimio yafuatayo:
a) Ujerumani kulipa uharibifu uliojitokeza zaidi ya dollar milioni 6.5
b) kurejesha Alsace na Lorraine kwa Ufaransa( kumbuka wakati wa Franco Prussian war)
c) Kutojihusisha na utengenezaji wa silaha za aina yoyote.
d) Kutokuwa mwanachama wa league of national (Ingawa alikubaliwa baadae).
Nk.
Baada ya vita hivyo Ujerumani ilikuwa chini ya Kaizer ambaye aliisababisha kuingia tena kwenye mtikisiko wa kiuchumi wa mwaka 1929-1933.
Hali hii ikasababisha mwanaume Hitler kuibuka na kusema Ujerumani imeshindwa vita vya dunia kwa sababu ya unafiki wa Wayahudi( kumbuka Wewe Zitto Ujeruman ndo nchi iliyokuwa ikitumia he badala ya she kama nyingine za dunia)
Aliibuka kuitangazia dunia kuwa Ujerumani bado ni strong state ( sense of nationalism) na kwa kuwa kulikuwa na vibaraka wa kiingereza na mataifa mengine ya mlengo wa kibepari aliamua kupitisha sheria hiyo kwa maslahi mapana ya nchi?
Nakuuliza ingekuwa Wewe ungeendelea kuwaacha akina Kaizer waharibu nchi?
Kipindi watu wako bungeni mnatembea Ulaya kuhubiri ushoga, na kulitukana taifa, Ingekuwa Hitler angewaacha????
Acha kusahau mapema Hitler unayemzungumzia ameipata Ujerumani iliyo imara baada ya kutengenezwa na mtu aliyeitwa Chancellor Ottoman Bismarck, ambaye aliamua kufuta kabisa bunge kwa sababu walikuwepo akina Zitto waliopinga Muungano wa Ujerumani nae alisema
"The great question of the day cannot reached by majority resolution but by blood and iron" akalifuta bunge na akafanikiwa 1870's kutengeneza Ujerumani ya Leo.
Zitto tafadhali brother usipende kutumia mifano ya nje ukifikiri Watanzania wrote hatusomi,
Nenda kajipange Upya, Spika ndugai leteni sheria ya kufuta wazururaji walioko huko ulaya muwafute kabisa........
Tunataka maendeleo siyo uzindaki.
Mwl.Osunga Jr.
0756231744