Kutoka Bungeni: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wapitishwa kuwa Sheria

Kutoka Bungeni: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wapitishwa kuwa Sheria

Walowezi waliokuwa wakitawala Zimbabwe walitunga sheria mbaya kudhibiti wapigania uhuru. Lakini hatimaye uhuru ulipatikana. Baada ya uhuru waziri mmoja na walinzi wake walivamia shamba la mlowezi mmoja na mwenye shamba alipohoji walimuua. Wauaji Walifunguliwa mashtaka ya kuua mbele ya Jaji mweupe. Walijitetea kwa kutumia ile sheria ya kikoloni iliyolenga kuwadibiti wapigania uhuru ambapo kiongozi wa serikali alipewa kinga ya kutoshtakiwa anapofanya jambo lolote kwa nia ya kuwadhibiti wakorofi. Wakorofi waliolengwa na sheria wakati inatungwa walikuwa watu weusi. Mara wakorofi wakageuka kuwa wale waliotunga hiyo sheria! Wauaji walishinda kesi.
 
Mnamlaumu bure huyo Simbachawene si aliunga unga Elimu ya Open University hana chochote anachojua yupo kwenye jamii ya kundi la vilaza...
 
Bunge limepitisha sheria ya vyama vya siasa ambapo sasa vyama vya siasa vitapaswa kupeleka mahesabu kwa msajili.
Sasa vyama vya siasa vitatakiwa kutoa taarifa ya fedha wanazopewa na wafadhili.

Vyama haviruhusiwi kuwa na vikundi vya ulinzi

Wanafunzi wa vyuo vikuu hawatakiwi kushiriki siasa wawapo chuoni

Msajili wa vyama vya siasa anaruhusiwa kuingia katika mkutano wa chama chochote cha siasa na anaweza kusimamia uchaguzi wa chama chochote cha siasa.

Source ITV habari!

Mwanahabari mmoja nguli alipata kuwaasa wanavyuo kuwa walofanya siasa vyuoni hawatakaa wawe wanasiasa. Huu ni ubaguzi wa kijima sijapata kuona. Hii sheria bacterium mwezi kabla haijahojiwa mahakamani. Kwanini ccm inajidhalilisha kiasi hiki?
 
Huyu ni Katibu Wa wamiliki Wa baa
Baa yake inaitwa Titanic iko Vingunguti
Sijui kwa nini kibakwe walimpa ubunge
Sijui kwanini Kikwete alimpa uwaziri
Nchi hii jamani khaaaaa!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa hao ndo wenye nafuu waliobaki hujawaona walivyogonga meza huyu kichwa wao akishusha huu upuuzi
 
Nimesikiliza angalau kipande cha mchango wa Ndugu George Simbachawene kuhusu muswada wa sheria ya vyama vya siasa,nilichokigundua sasa ipo hoja inapazwa kwa kasi kuwa.....

1.Kufa kwa viwanda nchini Tanzania ni sababu ya uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu mfumo wa Vyama vingi nchini.

2.Kufa kwa Mashamba makubwa yaliyotoa ajora za kutosha ni kwa sababu ya uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu mfumo wa Vyama Vingi nchini.

3.Uwekezaji ambao haukuwa na tija kwa taifa letu kulisababishwa na uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu Vyama vingi.

4.Tatizo la ajira nchini ambalo linakuwa siku baada ya siku limesababishwa na mfumo wa Vyama vingi nchini.

5.Kashfa kubwa za Rushwa kama EPA,Escrow,Richmond,Meremeta,Dowans n.k zilisababishwa na nchi kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi.

6.Kufa kwa Shirika la Reli,Shirika la Ndege/Anga kulisababishwa na uamuzi wa mwaka 1992 wa kuanzisha mfumo wa Vyama vingi.

Ndiyo maana George Simbachawene anasema nchi kama China ina chama kimoja tu na uchumi wake sasa ni imara.

Simbachawene anatamani Tanzania tubaki na chama kimoja ili tujenge taifa lenye nguvu duniani.Sijui kwa nini George hajatumia mifano ya mataifa ambayo yameendelea na yana mfumo wa vyama Vingi?

George Simbachawene ambaye kama sikosei aliondoshwa kwenye Wizara ya Madini na Mh Rais kutokana na kutuhumiwa na Kamati ya Mh Rais ile ya Makanikia,anasema huko nyuma nchi ilikuwa kwenye presha muda wote na akataja harakati kama..

1.Movement for Change
2.Oparesheni Sangara n.k

Kwa mtazamo wa Ndugu Simbachawene,harakati hizi zilichangia kuchelewesha maendeleo nchini.

Nakumbuka harakati hizi zlikuwa zinapiga kelele dhidi ya hiki anacholia nacho Mh Rais Magufuli kila kukicha,wizi,Rushwa,kujilimbikizia mali,Uwekezaji wa hasara.

Je Simbachawene anataka kusema Vyama vya upinzani vingekaa kimya wakati Buzwagi wanawasainisha mawaziri wetu mikataba mibovu hotelini?

Je Simbachawene anasema Vyama vya Upinzani vingekaa kimya wakati baadhi ya Mawaziri,wafanyabiasha na watumishi wa Umma wanagawana pesa za Escrow kwenye sandarusi?

Je Simbachawene alitaka Vyama vya Siasa vikae kimya wakati wakazinwa Nyamongo wanateseka na maji yenye sumu kutoka mgodi wa North Mara,wanapigwa Risasi na wawekezaji?

Je Simbachawene alitaka Vyama vya upinzani vikae kimya wakati wawekezaji kwenye migodi walipojigeuza miungu watu(wasiguswe),walipokuwa wanawahakisha wenyeji kinyama tena usiku wa manane bila fidia?

Je Simbachawene alitaka Vyama vya upinzani vikae kimya wakati wawekezaji hawa walipokuwa wanachimba madini bila kulipa kodi?huku suala la mapato wakilifanya kuwa ni Siri kati yao na Serikali

Je Simbachawene alitaka vyama ya upinzani vikae kimya wakati Twiga wanahamishwa kwenda nje kwa ndege?wanyama wanauwa na wawindaji haramu?

Je Simbachawene alitaka watu wakae kimya huku kuna watumishi wa Umma walikuwa wanakula mishahara hewa?

Je Simbachawene alitaka wapinzani wakae kimya wakati baadhi ya Viongozi wetu wakuu walipoamua kujiuzia mpaka migodi ya madini?

Yaani haya yote,adhabu yake ni kuwazuia wanasiasa wasiseme chochote mpaka wakati wa uchaguzi na wakikaidi Msajili anawafuta katika wigo wa Siasa?

Kwa nini tusitunge Sheria ambazo zitakuja kuwafanya Watanzania wazidi kuwa wamoja zaidi bila kujali tofauti zao za kisiasa,kidini,kikabila na hata kimtazamo?

Kwa nini baadhi yetu kila siku tunawaza kutunga Sheria ambazo zinalenga kubinya haki za wengine?

Kwa nini tufikirie kutunga Sheria ambazo zinatengeneza hofu badala ya Ujasiri?

Mambo haya yanatafakarisha sana sana.
Mawazo ya chama kimoja ni muflisi na ya hovyo kabisa. Mfumo wa chama kimoja ndio ulituletea umasikini wa kutupwa
 
Hii sijui hata ni kitu gani Tanzania yetu inapitia kwa sasa. Mytu aliyefikia level ya uwaziri halafu huwezi kuchambua hata ABC za maendeleo ina maana umeturudisha nyuma kimaendeleo miaka yote uliyokuwa kwenye level ya uwaziri ndio maana akaondolewa pale halafu sheria na miradi aliyoipigania kwa wakati huo ama leo zinabadilishwa au miradi ile inaonekana haina maana tena. kumbe alitudanganya wakati anatuambia mradi wa gesi ukikamilika shida ya umeme itakuwa historia na umeme utashuka bei. ni UBATILI MTUPU kwa yale yanayotokea leo. Kumbe tungeiacha gesi tukaenda stiglaz goji.Ukitolea mfano wa CHINA wao wana commitment ambapo hata wangekuwa na vyama mia bado wangepiga hatua. kwa nini husemi JAPAN,MALAYSIA,SOUTH AFRICA na kwingine kwingi tu. Unaposema mfumo wa vyama vingi unakuchelewesha usilete maendeleo sio kweli kabisa. kwa sababu wewe chama tawala ndio una serikali mipango yote unapanga wewe, wapinzani kama ungewaelewa wangekusaidia sana kufikia malengo yako kwa sababu sauti zao za kukosoa ni taa ya kukuongoza wewe.Nakumbuka kati ya wabunge/waziri waliopinga na kusema mfumo wa elimu bure nchi hii hauwezekani na yeye alipinga. lakini leo ndio unatekelezwa na serikali.Nafikiri ni mmoja wa walioshiriki na kuupigia debe muswada wa TAKRIMA na ulipita ukawa sheria, hivi leo sheria hiyo bado ipo?, lakini alinishangaza pia wakati fulani akichangia hoja laisema kazi ya bunge ni kutunga sheria hivyo haipo haja ya kubishana. wao wapitishe sheria halafu wakija ona haifai wataibadilisha hapo NILISIKITIKA KABISA, bunge kupitisha sheria kwa matarajio ya kuja kuibadili baadae bila kufikiria madhara yatakayosababishwa na sheria hiyo pindi ikipitishwa na ikaanza kutumika. nchi hii siyo ya majaribio ya sheria.Mimi sheria hii siielewi kabisakabisa yaani MSAJILI ANAPEWA UWEZO WA KUMFUTA UANACHAMA MWANACHAMA WA CHAMA CHA SIASA!!!!!!, sasa vyama hivi vina haja ya gani ya kuwa vyama? kama hata uwezo wa kusimamia wanachama wao unakuwa nusunusu.NILICHOJIFUNZA TANGU MFUMOO HUU UANZE NCHI HII VYAMA VYA UPINZANI VIMEKUWA MSAADA MKUBWA SANA KWA SERIKALI NA WANANCHI KWA UJUMLA KATIKA KULETA MAENDELEO NA KUPATA TAARIFA MUHIMU ZA NCHI YETU. Ndio Maana akina KAFULILA leo ni RAS, Ndio maana RUGE na SING leo wako lupango. lakini pia Ndio maana leo Mh.JPM yuko hapo vinginevyo asingeingia hata kwenye kinyang'anyiro ndani ya chama kwa jinsi tulopokuwa tumefikia wakati ule. NAKUSHOKA HANGI BAGOSHA!!!
 
*Kutoka katika chanzo changu cha kuaminika (Kimada wangu anayefanya moja ya kazi ndani ya Mjengo)

Taarifa ni kuwa kuna Onyo lilitolewa na mmoja wa Maafisa wakubwa wa Chama (Jina Ninalihifadhi) kwenye kikao cha siri cha dakika 15-20 na baadhi ya Wabunge kama 17 wa Chama Tawala ambao pia kwa namna moja ama nyingine hawakuwa wakikubaliana na baadhi ya Vipengele vya Muswada ule uliopitishwa.

"Nimeambiwa niwaite niwape ujumbe, Yule atakayesaliti na kukiuka makubaliano yetu ya kupitisha Muswada huu, atashughulikiwa, siku zake pamoja nasi zitahesabika na Tusilaumiane kitakachomkuta"

ilikuwa ni moja ya kauli ya Afisa huyo kwenye kikao hicho kilichofanyika ndani ya moja ya vyumba vya mkutano bungeni Mapema Asubuhi siku ya Jumatatu.

Chanzo changu kinaendelea kusema kuwa Suala la Bundi kuonekana ndani ya Ukumbi wa Bunge lilipotokea lilizidi kuwatia Hofu na kuhusishwa na masuala ya Kishirikina hivyo kila mmoja wao kutepeta na kuunga mkono kukubaliana na kilichokuwepo ili tu kunusuru Maisha yao kwa kuogopa kurogwa na kutolewa Kafara kwa kuzingatia Ujumbe waliopewa na kuoanisha maana tuliyozoea ya Bundi kuonekana kuhusishwa na Bahati mbaya, Ugonjwa, au Kifo.

Ila hili la Bundi Pengine pia inaweza kuwa ni janja tu ya kuchezeana akili kwa kumkamata ndege huyu na kumtupia ndani ya Bunge ili kuwaogofya wahusika na kuwaaminisha juu ya ujumbe waliopewa.

Vinara wa Tunguli na Ulozi Bungeni hakyanani tena Hamuendi Mbinguni!
Habari hii inabaki kuwa udaku kama ulivyo udaku mwingine
 
Habari hii inabaki kuwa udaku kama ulivyo udaku mwingine
I wish kama angekuwa na Nerve ya kuwarekodi sauti ila pia nayo mngesema watu wameedit au mngewasingizia jamaa zenu wa Chadema kama kawaida.
 
I wish kama angekuwa na Nerve ya kuwarekodi sauti ila pia nayo mngesema watu wameedit au mngewasingizia jamaa zenu wa Chadema kama kawaida.
😀😀😀😀 unajua, hearsay kila mtu anaongea lake. Acha yabaki hivyo hivyo
 
Kama ni kweli basi sasa tumekuwa taifa la Kishirikina .............!!

By the way, kuna wakati data zilikuwa zinaonyesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuamini ushirikina duniani ...........!!
 
Kama ni kweli basi sasa tumekuwa taifa la Kishirikina .............!!

By the way, kuna wakati data zilikuwa zinaonyesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuamini ushirikina duniani ...........!!
Wanaweza kuwa hawajafanya ushirikina ila wamewatisha jamaa kuamini hivyo kwa ujumbe feki na kumuingiza bundi mjengoni ili yao yaende.
 
Back
Top Bottom