*Kutoka katika chanzo changu cha kuaminika (Kimada wangu anayefanya moja ya kazi ndani ya Mjengo)
Taarifa ni kuwa kuna Onyo lilitolewa na mmoja wa Maafisa wakubwa wa Chama (Jina Ninalihifadhi) kwenye kikao cha siri cha dakika 15-20 na baadhi ya Wabunge kama 17 wa Chama Tawala ambao pia kwa namna moja ama nyingine hawakuwa wakikubaliana na baadhi ya Vipengele vya Muswada ule uliopitishwa.
"Nimeambiwa niwaite niwape ujumbe, Yule atakayesaliti na kukiuka makubaliano yetu ya kupitisha Muswada huu, atashughulikiwa, siku zake pamoja nasi zitahesabika na Tusilaumiane kitakachomkuta"
ilikuwa ni moja ya kauli ya Afisa huyo kwenye kikao hicho kilichofanyika ndani ya moja ya vyumba vya mkutano bungeni Mapema Asubuhi siku ya Jumatatu.
Chanzo changu kinaendelea kusema kuwa Suala la Bundi kuonekana ndani ya Ukumbi wa Bunge lilipotokea lilizidi kuwatia Hofu na kuhusishwa na masuala ya Kishirikina hivyo kila mmoja wao kutepeta na kuunga mkono kukubaliana na kilichokuwepo ili tu kunusuru Maisha yao kwa kuogopa kurogwa na kutolewa Kafara kwa kuzingatia Ujumbe waliopewa na kuoanisha maana tuliyozoea ya Bundi kuonekana kuhusishwa na Bahati mbaya, Ugonjwa, au Kifo.
Ila hili la Bundi Pengine pia inaweza kuwa ni janja tu ya kuchezeana akili kwa kumkamata ndege huyu na kumtupia ndani ya Bunge ili kuwaogofya wahusika na kuwaaminisha juu ya ujumbe waliopewa.
Vinara wa Tunguli na Ulozi Bungeni hakyanani tena Hamuendi Mbinguni!