Kocha wa Simba, Djuma alitamba kuwa style yake ya uchezaji ndiyo iliyofanikisha kuifunga Singida United 4-0. Lakini hii sio kweli kabisa, alicheza na wachezaji ambao wana uchovu wa hali ya juu.
Kocha wa Singida ni mtu ambae anataka mafanikio ya leoleo na ya harakaharaka ili kuwananga Yanga waliomtema. Haraka yake hiyo ilisababisha Pluijm achezeshe kikosi chake cha kwanza chenye wachezaji walewale katika kila mechi kwenye mashindano ya Mapinduzi cup yaliyomalizika hivi karibuni. Wakati timu nyingine (Simba, Yanga, Azam) waliyatumia mashindano yale pamoja na kupata ushindi lakini pia kuwapa nafasi wachezaji wote kwenye timu wapate nafasi ya kucheza. Hii ilisababisha wachezaji mihimu wa Singida wapate uchovu mkubwa uliowagharimu kwenye mechi yao na Simba hadi kufungwa 4-0 kuliko wenzao wa Simba ambao wachezaji wake walikuwa wakicheza kwa mzunguuko kwenye Mapinduzi cup hivyo kuwafanya wasiwe na uchovu mwingi wa kuendelea na premier league kama ulivyoona jana.
Mimi nakuhakikishia Simba itakapokutana na timu nyingine yenye wachezaji ambao hawakuwa Mapinduzi cup utaona kitakachotokea.