Kutoka dimba la Taifa: Simba SC watakata! Wairarua Singida Utd goli 4 kwa nunge, wajikita kileleni kwa alama mbili zaidi

ongezea na kingoni Muite Usengwile Kwasi
 
Kocha wa Simba, Djuma alitamba kuwa style yake ya uchezaji ndiyo iliyofanikisha kuifunga Singida United 4-0. Lakini hii sio kweli kabisa, alicheza na wachezaji ambao wana uchovu wa hali ya juu.

Kocha wa Singida ni mtu ambae anataka mafanikio ya leoleo na ya harakaharaka ili kuwananga Yanga waliomtema. Haraka yake hiyo ilisababisha Pluijm achezeshe kikosi chake cha kwanza chenye wachezaji walewale katika kila mechi kwenye mashindano ya Mapinduzi cup yaliyomalizika hivi karibuni. Wakati timu nyingine (Simba, Yanga, Azam) waliyatumia mashindano yale pamoja na kupata ushindi lakini pia kuwapa nafasi wachezaji wote kwenye timu wapate nafasi ya kucheza. Hii ilisababisha wachezaji mihimu wa Singida wapate uchovu mkubwa uliowagharimu kwenye mechi yao na Simba hadi kufungwa 4-0 kuliko wenzao wa Simba ambao wachezaji wake walikuwa wakicheza kwa mzunguuko kwenye Mapinduzi cup hivyo kuwafanya wasiwe na uchovu mwingi wa kuendelea na premier league kama ulivyoona jana.

Mimi nakuhakikishia Simba itakapokutana na timu nyingine yenye wachezaji ambao hawakuwa Mapinduzi cup utaona kitakachotokea.
 
Naunga mkono hoja,Hans hajuagi kufanya rotation ya kikosi angalia hata akiw yanga swala la uchovu lilikuw linaonekana kwa wachezaj weng kutokana na kutumika katika michuano mbalimbali bila kupumzishwa.Hivo kilichomtokea jana kimenidhiirisha kuwa wachezaji wake ni wachovuu.
 
Kunywa sumu .mzeee...this is simba bwana
Na wengine ukiona simba inakukereketa basi kunywa sumu
 
Kwani Simba haikuwa mapinduzi cup?? Viroba sijui jangwani mmevificha wapi.
 
Hii kanuni pia ina apply kwa Mbao vs Yanga...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…