The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 4,249
- 11,592
Baada ya upande wa Jamhuri kuishia njiani kwa kuleta mashahidi 17 tu kati ya 30 waliopaswa kutoa ushahidi wao dhidi ya kesi iliyopewa Jina la "kesi ya uhaini" dhidi Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh Tundu Lissu, hatimaye leo Tundu Lissu ameanza kujitetea. Kwa kifupi sana, utetezi wako umejikita katika mambo mawili tu
1. Hana kesi ya kujibu, hakuna ushahidi wowote wa vielelezo kwa kosa wanalomshitaki nalo. Na kama ni hivi ajitetee kwa kipi?
2. Mahakama itamke kuwa anastahili kufidiwa kwa kuonewa na kushitakiwa kwa uongo na kuwekwa gerezani bure tu kwa siku zaidi ya 458..
Hii hapa chini full submission yake akithibitisha kuwa HANA KESI YOYOTE YA KUJIBU yaani "NO CASE TO ANSWER"
Mhe Lissu anaanza submission yake kwa kusema;
"....Waheshimiwa Majaji baada ya kusikiliza ushahidi wote wa upande wa mashtaka wa mashahidi wote 17, naomba kutoa hoja kwamba upande wa mashtaka umeshindwa kabisa kuthibitisha kwamba kuna prima facie case ya kuiwezesha Mahakama hii kumtaka mshtakiwa ajitetee.
Sasa Waheshimiwa majaji prima facie case ni kitu gani?
Waheshimiwa majaji prima facie case/ primafacie evidence ni ushahidi wa mashtaka unaotolewa na upande wa mashtaka ambao usipojibiwa kwa ushahidi wa utetezi mtu anafungwa au analipa fine ambapo kwa case kama ya uhaini mtu ananyongwa.
Kama upande wa mashtaka umetoa ushahidi ambao hata mtuhumiwa hawezi kujibia/ kujitetea then hakuna hatia (prima facie case)
A primafacie evidence siyo ushahidi wa mwisho katika case, ushahidi wa mwisho ni ule unaojumuisha ushahidi wa utetezi, hivyo Prima facie case ni ushahidi wa upande wa Jamhuri.
Msingi wa kisheria wa primafacie case to answer ni kifungu cha 312 (1) ambacho nimeshakisoma, hiki kimefanyiwa maamuzi mengi za Mahakama za juu ambacho kimetengeneza misingi ya kisheria ( Legal principles ) kuhusiana na nini kinapaswa kufanyanyika kuhusiana na hoja ya hakuna case ya kujibu.
Kesi ya East Africa ya Raumanlal Trambaklal Bhatt v Public 332 esp 334-335 hii ina umuhimu ule wa case ya Mkisa Biscuit kwa namna ilivyoweka msingi kisheria
(Mh Tundu Lissu anasoma citation ya Tramnaklal case)
Mahakama imesema, haitoshelezi tu kuwa ushahidi mwingi umetolewa bali ni lazima ushahidi huo mwingi uwe na uzito na credibility.
Waheshimiwa msingi huu Trambanaklal ulikubaliwa na Mahakama hiyo ya rufani katika case ya Murini vs Jamhuri 1967 EA 542, Uk 544, Mahakama ilinukuu approval uamuzi wake wa miaka kumi kabla wa case ya Tramnklal.
Waheshimiwa Majaji ni muhimu kukumbuka kuwa, mimi ni mshtakiwa pekee katika kesi hii na ikumbukwe katika kesi ya Khatibu Gandi inasema maneno ya mtu mmoja, hayatengenezi uhaini, na kwa ushahidi uliotolewa katika kesi hii haujathibisha nia yoyote ya kutenda kosa la uhaini.
Kama ndivyo hivi, on the basis kuwa kusipokuwa na primafacie case nitaitwa nijitetee kwa kipi?
Ni ushahidi gani nisipojitetea utanitia hatiani?
Na Je ushahidi ukoje kuhusu publication ya reasonable act?
Ni kwamba, lazima kuwe na ushahidi wa machapisho au matendo ya wazi.
Wakati wa pre trial Upande wa Mashtaka wanasema mimi nilichapisha maneno kwenye mtandao wa Jambo TV, hivyo uthibitisho wa haya maneno ulitakiwa uwepo Jambo Tv.
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba niwaelekeze ukurasa wa 185 wa record za Mahakama, upande wa mashtaka ulionyesha ushahidi wa nyaraka 9 na aina 2 za vielelezo ikiwemo Video clips, lakini hawajaleta hata moja.
Shahidi PW 17 ni shahidi pekee wa eye witness aliyenishuhudia kwenye mkutano, testimony ya mashahidi, shahidi PW 17 ndiyo shahidi mwenye ushahidi mzito, alisema yeye na wenzake watano ndiyo waliorecord na kurusha, amesema kwa maneno yake na kwa maandishi kupitia kielelezo D16 na ni shahidi wao, Kwahiyo kama ni tuhuma ya publication siyo ya kwangu mimi, bali ni ya huyo aliyepublish yaani huyo PW 17 naa amesema mpaka leo vipo kwake.!
Na ushahidi wa nani aliyechapisha hawajaujibu.
Waheshimiwa Majaji, walidai ooh wewe ndiye uliyeitisha Mkutano..
Lakini shahidi wao PW 17 amesema mwaliko waliupata kwa afisa habari wa Chadema anaitwa Brenda Rupia..
Na nikamuuliza uliniona mimi nikifanya maandalizi nikipanga viti akasema, hapana.
Kwenye hili suala la tatu hawajathibitisha kabisa kosa la kuchapisha maneno.
Naomba nimalizie,
Kama hakuna proof ya ku-commint treason act na hakuna intention, maana yake ni kuwa hakuna primafacie case, na kama hakuna primafacie case mkiruhusu nijitetee mtakuwa mnafanya makosa ya kisheria.
Sasa Waheshimiwa majaji msipokubali mnafanyaje?
Jibu ni kuwa mnafanya kile ambacho sheria imewataka mfanye kwa mujibu wa kifungu cha 312 (1) kufanya finding ya kuwa hakuna case ya kujibu.
Waheshimiwa Majaji naomba kama mtatoa huo uamuzi muutoe leo, kama mnaridhika na hoja hii, na kama mtaamua kuwa Kuna reason ruling na mkaamua kuwa mtatupa baadae, then, hakuna haja ya mimi kurudishwa Ukonga leo. Hili ni la pili;
La tatu; lipo kwenye kifungu cha 367 cha CPA (Sheria ya Makosa ya Mwenendo wa Jina), kama mashtaka ni ya uonevu ya kusingizia tu, then mnaweza kuamuru mtuhumiwa alipwe fidia
Kwa sbb haya maumivu yangu na familia yangu nani atafidia??
Na mashahidi wote 17 mmewasikia, hakuna hata mmoja aliyejaribu hata nusu inchi kuthibitisha kwa ushahidi madhubuti kuwa nimetenda kosa lolote la jinai..!
Hivyo naomba iamriwe kuwa sina kosa la kujibu pia ipangwe tarehe nije kuthibitisha madai/ fidia yangu.
Naomba niwape Waraka wa kikosi kazi wa Umoja wa Mataifa, uamuzi wa tarehe 23/2/2026 unaosema niachiwe mara moja na kulipwa fidia.
Hivyo Waheshimiwa Majaji msimamo ni kuwa hakuna primafacie case na kwakuwa hakuna Primafacie case, sheria inawataka muandike findings ya NO CASE TO ANSWER
Waheshimiwa majaji ya kwangu ni hayo tu.
(Mhe. Lissu anamaliza na kuketi.)
Jaji Ndunguru : Ehee Jamhuri mnasemaje?
Anasoma kosa kama lilivyoainishwa katika hati ya mashtaka na anaainsha maneno ya uhaini...
"WANASEMA KITU KIMOJA SAHIHI HAPA, WANASEMA TUTAHAMASISHA UASI, NI KWELI TUTAHAMASISHA UASI, TUTAKINUKISHA VIBAYA......"
Waheshimiwa Majaji DPP Vs Philipo Joseph Mtonda, 217 Rufaa ya jinai, Tanzlii 2021.... case hii ili cite case Tambaklal na ikarudia maneno ya hiyo Landmark cases ya Tambklal case.
Itaendelea.......
1. Hana kesi ya kujibu, hakuna ushahidi wowote wa vielelezo kwa kosa wanalomshitaki nalo. Na kama ni hivi ajitetee kwa kipi?
2. Mahakama itamke kuwa anastahili kufidiwa kwa kuonewa na kushitakiwa kwa uongo na kuwekwa gerezani bure tu kwa siku zaidi ya 458..
=============
Hii hapa chini full submission yake akithibitisha kuwa HANA KESI YOYOTE YA KUJIBU yaani "NO CASE TO ANSWER"
==============

==================
Upande wa Jamhuri naona bado umedinda tu. Wanataka jamaa ajitetee kwa kuwa kwa maoni yao ana kesi ya kujibu. Hii hapa submission yao ku - prove kuwa jamaa ana makosa, anatakiwa ajitetee...
====================
Wakili wa serikali Katuga anasimama anasema Upande wetu kwanini tunaona mshatikiwa ana kesi ya kujibu ni kutokana na makosa aliyoshtakiwa nayo kwa mujibu wa kifungu cha 39 (2) (d)Anasoma kosa kama lilivyoainishwa katika hati ya mashtaka na anaainsha maneno ya uhaini...