Mimi nimeshangaa sana kama kweli tuna watu wanataka kuwa viongozi, vinywa vimejaa matusi, kwa saa nzima badala kueleza sera, ni matusi tu? Sidhani kama hawa watu wanaamini Mungu yupo. Mungu aliyewapa afya, nguvu na uzima kutukana matusi tu kila iitwapo leo? Watu wengine wapo hoi hospital hata kuongea hawawezi wanatamani pumzi,afya na uhai kwa ajili ya kumtukuza na kumuabudu Mungu tu? Yaani Mungu ni mjinga kuwapa watu pumzi ili watukane tu wenzao? Mbona watu wanakiburi hivi? Mbona wanaijifanya wao ni Mungu? Haya sisi tunamwachia Mungu mwenyewe awaadabishe. Vita vyetu sisi sio juu ya damu na nyama, ila ni katika roho.