Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

hao wenye mabango kama wanamtukana Mwanaume eti Mgumba hakuna Mwanaume Mgumba as long as anadindisha maana hata wao baba zao si wao , ila Baba zao wanaweza kumpanda Mama yao tyu! poleni sana Malofa nyie huo ni upumbavu tu
 
Sisi huku Katavi ndiyo tumeunganishwa na Uwanja wa Jangwani kupitia ITV; jenrereta inaunguruma kama kazi, tumeshatumia lita 20 bado zingine 55 zipo. Leo ni kusikiliza hoja tu toka UKAWA ili tulinganishe na CCM halafu tuchukue uamuzi sahihi.
 
Tunataka mabadiliko whether they will bring positive result or not.Ukizidiwa na kiu unaweza hata kunywa mkojo wako mweyewe.They have failed for 50+ yrs.We want changes.....
mabadiliko mnayoyataka ni aina ya mwizi au kuondoa wizi?
huyo EL anayeimba mabadiliko ni wapi alikozeekea?
ni wizi gani wa ccm au ufisadi gani wa ccm ambao haumhusu yeye kwa namna moja au nyingine?
mbowe anapotaka short cut ya kwenda ikulu hata kama amewasaliti wapenda mageuzi ya kweli tutamuamini vipi?
kwa ubabe wa mbowe na lowasa na kiburi cha pesa walichotuonyesha tutawaamini vipi wakishashika dola?
mtei alianzisha cdm,akamuachia Bob nyange makani R.I.P,ambaye alikuwa shemeji yake na kisha mikoba ikakabidhiwa mkwe wake Freeman mbowe....je ina maana maamuzi ya ukoo ndio yanayotuamulia mustakabali wa cdm na future yake?

tafakari na sio kuimba mabadiliko bila vision na target
 
Watu wachache sanaaaa,hapo wako walio letwa kutoka uchagani ? pia kuna wana ccm waliokuja kusikiliza porojo,kuna watoto na kuna vibaka wote wanatafuta riziki.

Kama wa UKAWA walivyoenda kusikiliza porojo za CCM last week
 
Kujaza watu hakumaanishi wote wanakuunga mkono , Kuna watu walikuwepo kwa CCM na leo wapo kwa Ukawa , watu wamekwenda kusikiliza SERA siyo kupiga kura za wazi za ndio

By the way hatuna utamaduni wa kutoka out ndiyo outing zetu hizo Wabongo ,mi mwenyewe hapa nafunga ofisi naelekea but kumoyo kura ya Ndiyo kwa Pombeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Eeh leo sindono ndo itakuingia vzr ...karibu jangwani(ukawa)
 
mods hamtutendei haki huyu aliyeweka hii post haleti update yoyote, ule uzi wa TandaleOne uko wapi?
 
Last edited by a moderator:
Mmmhhhh mpaka natetemeka aisee hii ni zaidi ya tsunami na mafuriko sijui tuite gharika?
 
Wakuu salaam. Nikiwa mtanzania wa kawaida kabisa ambaye napima mambo ya kisiasa kwa vigezo vya msingi kuliko ushabiki, hatimaye nimejiwekea mambo machache tu na ya kawaida kabisa ambayo UKAWA na Lowassa wanatakiwa kuyafafanua leo ili nijenge imani kwao. Mambo haya ni :

1. Kwa kuwa Lowasa kati ya mwaka 1997 na 2000 alikuwa akiiongoza wizara ya kuondoa umasikini, alifanya nini kinachompambanua kwamba anachukia umasikini? Hapa mfumo si hoja yenye tija sana kwa sababu mifumo mibovu ina kawaida ya kuwajenga viongozi bora kwani hujipambanua wazi wazi.

2. Kati ya mwaka 1993 na 1995 Lowassa alikuwa akiiongoza wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi, alifanya jambo gani la kumtofautisha na watendaji wengine? Wananchi wamkumbuke kwa lipi katika wizara hiyo ambayo ilikuwa maalum kuhakikisha wananchi wanapata makazi bora na kuondoka katika dimbwi la umasikinttti.

3. Mwaka 2000 - 2005 huyu mheshimiwa aliongoza wizara ya maji na mifugo. Ninachotaka kujua ni kwa nini katika kipindi chake cha uongozi migogoro ya wakulima na wafugaji ilizaliwa. Ni dhahiri kuwa ni wakati huu wafugaji walipata nguvu ya kuvamia maeneo ya wakulima na kusababisha tatizo ambalo limekuwa sugu hata leo.

UKAWA kwa upande wao naomba watueleze ni kwa nini tuendelee kuwaamini iwapo wamerudi kukanusha yale waliyotuaminisha hata tukawapenda.

1. Vita dhidi ya ufisadi. CHADEMA walijipambanua kama wapiganaji wa kweli dhidi ya ufisadi. Hii ndio sera ambayo bila ubishi iliwapatia umaarufu mkubwa.

CHADEMA wasimame na kukiri hadharani leo kwamba yale waliyotuaminisha kwa muda mrefu juu ya ufisadi ni uongo. Haitoshi tu kusema Lowassa hakuwahi kutueleza ukweli kuhusu Richmond. Hii ni ushahidi kuwa Chadema si chama makini hata kidogo. Kinaendesha siasa za kitapeli kwa malengo binafsi.

Tena msamaha huu uende mbali zaidi kukiri kuwa yale mliyokuwa mkijidai kuwa ni ushahidi mzito mlionao ulikuwa uongo ili kupata huruma ya wananchi.

2. CHADEMA ikiri na kuomba radhi kwa watanzania kwa kitendo chake cha kukiuka misingi kiliyojiapiza kuisimamia na kukanyaga demokrasia. Msamaha uombwe dhidi ya dharau na kejeli walizofanyiwa waliokipigania chama hata kukifikisha hapo kilipo. Mchakato wa kupata wagombea katika ngazi za urais na ubunge umegubikwa na sintofahamu kiasi cha kusababisha mgawanyiko wa kisiasa. Intelijensia ya CHADEMA imekuwa juu ya matakwa ya wananchi.

3. CHADEMA iombe radhi kwa utapeli wa kisiasa ilioufanya dhidi ya mauaji ya Olasiti. Ule mkanda unaoonyesha wauaji wakitekeleza mauaji hayo umeota mbawa. Hizi ni siasa za kitapeli. Kutafuta huruma za wananchi kwa hila.

4. CHADEMA wafafanue mipaka ya mashirikiano yao na CUF hasa linapokuja suala tata na nyeti kwa maslahi ya nchi la sera ya ULIBERALI. Watanzania tumeaminishwa na CHADEMA kwamba CUF wanasimamia ushoga na wanauunga mkono. Naomba CHADEMA waelezee msimamo wao, ama waombe radhi kwa kuwazushia uongo CUF.

Haya ni baadhi ya masuala ya msingi sana ambayo natarajia mkutano wa leo wa UKAWA utayatolea ufafanuzi.

Tujadili kwa hoja, matusi mwiko. Lizaboni, RIZ1, et al


Tangu 1961 ASP/TANU then CCM ,Wamefanya nini kuondokana na matatizo yote uliyoorodhesha hapo?
 
ingekuwa Diamond kavaa nguo za kijani wangeanza kutema vinyesi humu, ila kwa vile ni mashabiki wa Ukawa utaskia kila mtu ana haki...hivi hiyo freedom of expression ipo tu kwa wapenzi wa Ukawa??!! acheni Unafki
 
Makundi mengi ya watu yamefanya mchakato wa kuchangishana pesa wenyewe kwa wenyewe bila kushurutishwa ili wafike jangwani kwa pamoja.Au hamjui kuwa leo jangwani ni zaidi ya beach?Vijana wa mjini wamekodi magari wenyewe na huu ni utamaduni wa dar hasa siku za sikukuu so sioni ajabu cuz hata washkaji zangu walikuwa wanapitisha daftari kwa kila anayetaka kufika beach ya jangwani.
 
Back
Top Bottom