Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Wakuu salaam. Nikiwa mtanzania wa kawaida kabisa ambaye napima mambo ya kisiasa kwa vigezo vya msingi kuliko ushabiki, hatimaye nimejiwekea mambo machache tu na ya kawaida kabisa ambayo UKAWA na Lowassa wanatakiwa kuyafafanua leo ili nijenge imani kwao. Mambo haya ni :

1. Kwa kuwa Lowasa kati ya mwaka 1997 na 2000 alikuwa akiiongoza wizara ya kuondoa umasikini, alifanya nini kinachompambanua kwamba anachukia umasikini? Hapa mfumo si hoja yenye tija sana kwa sababu mifumo mibovu ina kawaida ya kuwajenga viongozi bora kwani hujipambanua wazi wazi.

2. Kati ya mwaka 1993 na 1995 Lowassa alikuwa akiiongoza wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi, alifanya jambo gani la kumtofautisha na watendaji wengine? Wananchi wamkumbuke kwa lipi katika wizara hiyo ambayo ilikuwa maalum kuhakikisha wananchi wanapata makazi bora na kuondoka katika dimbwi la umasikinttti.

3. Mwaka 2000 - 2005 huyu mheshimiwa aliongoza wizara ya maji na mifugo. Ninachotaka kujua ni kwa nini katika kipindi chake cha uongozi migogoro ya wakulima na wafugaji ilizaliwa. Ni dhahiri kuwa ni wakati huu wafugaji walipata nguvu ya kuvamia maeneo ya wakulima na kusababisha tatizo ambalo limekuwa sugu hata leo.

UKAWA kwa upande wao naomba watueleze ni kwa nini tuendelee kuwaamini iwapo wamerudi kukanusha yale waliyotuaminisha hata tukawapenda.

1. Vita dhidi ya ufisadi. CHADEMA walijipambanua kama wapiganaji wa kweli dhidi ya ufisadi. Hii ndio sera ambayo bila ubishi iliwapatia umaarufu mkubwa.

CHADEMA wasimame na kukiri hadharani leo kwamba yale waliyotuaminisha kwa muda mrefu juu ya ufisadi ni uongo. Haitoshi tu kusema Lowassa hakuwahi kutueleza ukweli kuhusu Richmond. Hii ni ushahidi kuwa Chadema si chama makini hata kidogo. Kinaendesha siasa za kitapeli kwa malengo binafsi.

Tena msamaha huu uende mbali zaidi kukiri kuwa yale mliyokuwa mkijidai kuwa ni ushahidi mzito mlionao ulikuwa uongo ili kupata huruma ya wananchi.

2. CHADEMA ikiri na kuomba radhi kwa watanzania kwa kitendo chake cha kukiuka misingi kiliyojiapiza kuisimamia na kukanyaga demokrasia. Msamaha uombwe dhidi ya dharau na kejeli walizofanyiwa waliokipigania chama hata kukifikisha hapo kilipo. Mchakato wa kupata wagombea katika ngazi za urais na ubunge umegubikwa na sintofahamu kiasi cha kusababisha mgawanyiko wa kisiasa. Intelijensia ya CHADEMA imekuwa juu ya matakwa ya wananchi.

3. CHADEMA iombe radhi kwa utapeli wa kisiasa ilioufanya dhidi ya mauaji ya Olasiti. Ule mkanda unaoonyesha wauaji wakitekeleza mauaji hayo umeota mbawa. Hizi ni siasa za kitapeli. Kutafuta huruma za wananchi kwa hila.

4. CHADEMA wafafanue mipaka ya mashirikiano yao na CUF hasa linapokuja suala tata na nyeti kwa maslahi ya nchi la sera ya ULIBERALI. Watanzania tumeaminishwa na CHADEMA kwamba CUF wanasimamia ushoga na wanauunga mkono. Naomba CHADEMA waelezee msimamo wao, ama waombe radhi kwa kuwazushia uongo CUF.

Haya ni baadhi ya masuala ya msingi sana ambayo natarajia mkutano wa leo wa UKAWA utayatolea ufafanuzi.

Tujadili kwa hoja, matusi mwiko. Lizaboni, RIZ1, et al

Hapa watu wanajadili matukio ya Jangwani, hayo maswali yako kayaanzishie thread watakujibu wenzako. Shut up!
 
Hata leo mzee LOWASA hujavaa GWANDA? Aaaaaa mimi umeniangusha sana.
 
Huku Tabora wamekata umeme lakini nilikuwa nimejiandaa kikamilifu kwa siku ya leo nipo zangu home nimewasha generator naangalia kama kawa hii nyomi sidhani kama CCM watakuwa na lolote la kusema zaidi ya kupanic na kutafuta mbinu nyingine ya kuhujumu UKAWA ingawa kila wakifanyacho kinakuwa wazi kabla ya kutekelezwa.
 
Najaribu kuwaza kauli ya rais kikwete kwamba picha za mikutano ya. Lowasa zinaeditiwa, leo niko natazama TV ili nione wanaustadi kiasi gani kuedit hizi picha nakosa majibu, naona ni picha halisi, sasa je rais wetu ni mwongo??????
 
..umeme umekatwa mji mzima dar....kama kuna wenye umeme waseme hapa....alafu chanel 10 walikua wanaonyesha ufunguzi wa ccm leo...yaani parallel na ufunguzi live wa UKAWA...nimegundua sasa chanel 10 wamenunuliwa na ccm....will never watch them dogs....
 
TANESCOCCM wamefanya yao. makamanda mliopo jangwani endeleeni kutupa updates. hapa mtaani tumedhibitiwa na TANESCOCCM. lakini hata hivyo, malofa na wapumbavu tutafuatilia mkutano wa ukombozi kutoka jangwani kupitia kwenye viredeo vyetu vya mkulima.
 
3X6A6342.jpg

3X6A6344.jpg

3X6A6351.jpg

moods unganisha hizi picha pale juu
 
Duh...DJ aliweka Audio ya zito akihutubia bungeni MC akawa makini na ku mute. Kwa wepesi ule wa MC kuingilia lila na kulipoteza, seems MC alikosa imani na huyu DJ tangu Mwanzo.
 
Back
Top Bottom