Ukichunguza kwa makini huyu mzee Mkapa ni kama ana gundu hivi. Yeye kila kampeni anayoshiriki lazima aanzishe maneno ambayo yanakuja kuki cost chama chake.
Nakumbuka Arumeru Mashariki wakati wa uchaguzi mdogo alitoa kauli ya Utata kuhusu Nyerere na iliki cost chama naye mwenyewe mpaka ikabidi aiombe radhi familia ya Mwalimu.
Juzi Jangwani tena kaita Watanzania wapumbavu na malofa, leo imekuwa kauli inayotumika kuzalisha chuki dhidi ya chama chake na watu wanamjibu kuwa ni kweli wao ni malofa kwa vile yeye na chama chake kila wafanyacho wao walikuwa wanakubali tuu.
Wazee hawaambiwi wana Laana, hivyo mimi siwezi sema. ila nadhani wapo wazee waliomzidi Mkapa umri wakiulizwa wanaweza sema bila kupepesa macho kuwa ANA LAANA.
View attachment 281739