Notradamme,
Soma kisa hiki hapo chini:
...baada ya kuongea na mimi nikamuuliza swali,''Umejuaje kama mimi
ni Musilam? Dalili zipi zimekujulisha kuwa mimi ni Muislam?
Yule bwana akanijibu kuwa, ''Mimi nilikuwa napita nje ya hii ''telephone
booth'' na mazungumzo niliyokuwa nasikia ni ya upande mmoja tu na
nilikusikia kwanza ukizungumza Kiingereza kisha Kiswahili.
Nikajiambia lazima nisubiri hapa nje nimuone huyu kijana.
Jinsi ulivyokuwa unaongea ilinidhihirikia kuwa lazima mtu huyu atakuwa
Muislam...''
Hiki ni kisa changu na mtu mmoja kimji kidogo nje ya London kinaitwa
Tilbury.
Huyu bwana alinisikia nikizungumza na akajua kuwa mimi ni Muislam na
akawa na hamu ya kuzungumza na mimi.
Notredamme,
Mimi sikujui lakini nina hakika wewe si Muislam.
Najuaje?
Maneno yako hayakuelekea.
Ila sielewi kwa nini unajinasibisha na Uislam.
Sielewi kipi unakiona hakikukaa vyema kwenye imani yako kiasi cha kujitoa.
Nakupa kisa kingine.
Niko ndani ya tram Alexandria natoka Ramala Station nakwenda kwangu
Saint Stefano.
Behewa zima limejaa Waarabu.
Mswahili ni mimi peke yangu.
Mzee mmoja wa Kimisri akaniuliza kama mimi ni Muislam nikamjibu, ''Alhamdulilah.''
Hakuridhika akataka nimpe ushahidi.
Nikamuuliza, ''Ushahidi gani unataka nikupe?''
Akasema, ''Nisomee Qur'an.''
Nikasoma Surat Fatha.
Akacheka akasema hiyo sura mtu yoyote anaweza kuisoma akanambia, ''Nisomee
kitu chochote katikati ya mashaf.''
Behewa zima limenizunguka kutaka kujua kama kweli huyu mtu mweusi ni Musilam.
Ukitembea duniani utajifunza mengi sana.
Watu wengi hawajui zaidi ya pale wanapoishi.
Hawa Wamisri wanadhani dunia nzima wako Waarabu na Waislam ni Waarabu tu...
Nikamsomea kitu kutoka katika Qur'an nikaanza...''...ila ghasaki layli wa Qur'an l'fajr...
hawakuniachia nimalize behewa zima llilinyanyua mikono huku wakipiga kelele,
''Alhamdulilah, Alhamdulillah...''
Notradamme,
Jitulize nahisi wewe ni kijana mdogo sana.
Tulia ujifunze.
Nami nakuombea dua Allah akupe ilm na akulete katika Uislam.
Amin.
Notradamme,
Ikiwa wewe ni Muislam nakupa changamoto hiyo aya hapo juu niwekee maneno
yaliyotangulia.