Tatizo la kuwa na stress za maisha ndo kama hivi, unaongea kitu hata hueleweki alimradi tu nawe ionekane walau umecomment.
Kwa kukusaidia ili uondokane na huu msongo wa mawazo ambao umekuwa ukikusumbua kwa siku nyingi bila kupata tiba. Chukua haya ninayokwambia na utapona kabisa mpaka siku yako ya mwisho hapa duniani. Tiba hii ingia katika mwanga na toka haraka sana huko gizani. Ingia katika nuur ya Uisilamu utaishi maisha yenye amani tele.
Pole sana ninaelewa ni wengi sana wenye matatizo kama yako lakini kwa kukufahamisha zaidi wale wazungu ambao unawaamini sana sasa hivio wameitambua hii tiba ninayokuelezea hapa na kwa hakika mamia kwa mamia wanaingia katika diyn ya Haq ili kuondokana na stress zilizokuwa zikiwasumbua kwa muda mrefu sana. Hujachelewa amka sasa uingie katika Nuur. Usikubali kabisa kuendelea kuwa mfuasi wa wanaowaambia wafuasi wao kuwa dini yao hawawazi kuielewa mpaka wapate roho mtakatifu.
Huwezi samehewa dhambi kupitia kwa mtu kama hao viongozi wako wanavyokuelekezeni. Aidha kwa tafakur zaidi jaribu kutumia muda mchache kwa kutumia akili ambazo umejaaliwa na Muumba kuhoji ni vipi mungu akauliwa?, ni vipi mungu akadhalilishwa? ni vipi mungu alieumba mwanadamu halafu tena azaliwe na huyo mwanadamu aliyemuumba.
Karibu katika Mwanga....
JINI NI NINI?
Katika lugha ya kiarabu, neno jini linamaanisha
kitu kilichofichwa au kisichoonekana QURAN
1:7.1 Neno hili hutumiwa na Waarabu kwa ajili
ya kutaja jina fulani. Kwa Waarabu, Jini
anayevaa sura ya kike humwita Jinivya, hivyo
majini Ghul/Ghilan, nao hujifunua kwa sura ya
kike.
Katika imani ya Kiislamu, wao huamni kwamba
Majini hutofautiana na Mashetani. Majini
waliosilimu wao huitwa majini mazuri na hawa
wakiwa katika hali kujionyesha kwa wanadamu,
hao huitwa AJINU na wale walioacha kusilimu
mwaka 610 AD (Baada ya Kristo) katika safari
ya mtume Muhamad alipotoka Taifa , wao
wanaitwa Mashetani . Hivyo, wao wanapokuwa
katika hali ya kutoonekana huitwa ALBAHATWA
lakini pia Majini wote wanapokuwa katika hali
ya kutoonekana waweza kuitwa ALBAHATWA,
yaani PEPO.
Muislamu huamini kwamba kuna majini ya kike
na kiume. Lakini pia , huamini kuwa Majini
huoana na kuzaliana QURAN 55:56 na kuwa
Majini huzaa sana kuliko binadamu na kwamba,
Jini mmoja anaweza kuzaa watoto 300, na
kuwa Jini huzaa watoto 3 hadi 4 kwa mkupuo.
Somo QURAN 55:26-28 na kuwa Majini
wanaweza kuishi miaka 400-1,000 kisha
wanaweza kufa. Tofauti yao na binadamu ni
kwamba wao wanaishi miaka mingi kuliko
binadamu. Lakini pia, huamini kuwa wapo
Majini wanaokula, wanaomeza, wanaokunywa,
ila tofauti yao na wanadamu ni kwamba wao
hula kwa kutumia mkono wa kushoto. Pia
hiamini kuwa Majini wana uwezo wa kuzaa na
Wanadamu. Soma QURAN 17:64. Waislamu
huamini kwamba mtu anauwezo wa kuoa au
kuolewa na Jini bila kujua, na mwanadamu
anauwezo wa kumuua Jini. Soma QURAN
57:14-15
SURATULJINN
Ndani ya QURAN pia imo sura inayoitwa
Suratuljinn ( QURAN 72 ). Sura hiyo huitwa
hivyo kwa sababu ni sura ya Majini (Mapepo).
Kwa nini wanatajwa Majini katika imani ya
Kiislamu?
Majini wanatajwa sana katika dini ya Kiislamu
kwa kuwa ni waislam kwa kusilimu, kwa
kuiamini Quran tukufu aliyopewa mtume
Muhamad.. Majini walisilimu na kuwa Waislamu
mwaka 620 AD(Baada ya Yesu) 72:1-14
QURAN. Hivyo basi, unapotumia neon jinni
maana yake unatumia lugha ya Kiarabu
ukimaanisha Pepo mchafu. Ni kama Spoon/
kijiko, vyote ni kitu kimoja. Ndani ya Quran,
neon PEPO limetumika kama Paradiso,
mbinguni. Lakini pia, tunapata neon jingine
liitwalo AKHERA ila neon hilo halimaanishi
PARADISO, bali kwa lugha ya Kiarabu neon hili
AKHERA lina maana ya KUZIMU. Lakini pia
ukiangalia ndani ya SURALJINN ( QURAN
72:1-2, 8-9, 12 ) Mapepo hawa wanajieleza
waziwazi kabisa kuwa mwanzo waliishi
Mbinguni, walipogeuka kwa kuasi, walitegwa na
Mungu. Linganisha na maandiko haya katika
Biblia ( UFUNUO WA YOHANA 12:7-9; YUDA
1:6-8; UFUNUO 20:10; UFUNUO 21:8 ). Kwa
mujibu wa dini ya Kiislamu, hawa majini
( Mapepo ) waliotegwa na Mungu Mbinguni
wakiwa Malaika huko na kutupwa Duniani
baada ya kuasi huko, sasa, wakati wa mtume
Muhamad katika safari yake ya kurudi Taifa
mwaka 620 AD (baada ya Yesu) wapo
walioamini na kuona kuwa Quran ni ya ajabu ya
kuwatangazia neema ya kuabudu. Katika vol
8-9, husema , wanapojaribu kwenda Mbinguni
( walikotoka zamani ), hukuta ile Mbingu
imezungushiwa vimondo vya moto. Hivyo, hudai
kuwa mbingu yao iko Akhera, yaani Kuzimu,
maana Mbingu ya juu ina moto na hawana
uwezo wa kwenda huko. SOMA ( QURAN 72:9 ),
Mbingu ina utisho wa moto ila Akhera
( kuzimu ) hakuna shida kwao .
Hivyo basi, kulingana na jinsi Allah asemavyo
ndani ya Quran kuwa nimeumba binadamu na
majini ili muniabudu ( QURAN 57:58 ; 51:56) na
kuwa , mbinguni mwao Majini wamo waabuduo
(Majini waliosilimu mwaka 620 AD ,SOMA
QURAN 72:14, ambao ni wema wanaosafiri na
kurithi uzima wa milele upatikanao Akhera
( Kuzi mu ). Lengo kubwa la Shetani na Majini
ni kufanya urafiki na wanadamu wengi ili kwa
wingi huo apate watu wengi wa kwenda nao
JEHANAMU ( QURAN 6:128 ). Jambo la
muhimu kujua hapa ni kwamba moto wa milele
hakuwekewa Mwanadamu bali ni Shetani na
malaika zake wote ( Majini au mapepo ). Hawa,
hawana nafasi tena ya kuungama au kutubu.
Yesu Kristo hakuwa na urafiki wowote na
Shetani wala Mapepo ( Majini ), aliyaamuru
kutoka ndani ya watu waliokuwa wakiteswa
nayo ( MATHAYO 8:29: MARKO 5 N,K )
Wakati Yesu anaondoka hapa duniani,
alichukuliwa na wingu na kupaa kuelekea juu.
Mbinguni ni juu kama Quran inavyothibitisha.
Yesu aliweza kupaa na kuingia Mbinguni lakini
Majini ( Mapepo ) waliosilimu wakijaribu tu,
wanakutana na moto mkali. Tumeona kuwa
Majini ambao ni Waislamu kwa kusilimu,
wanaishi AKHERA yaani Kuzimu. Je, Waislamu
wengine unadhani wataishia wapi milele?